Je huu ni upendo wa dhati?

BILGERT

JF-Expert Member
Feb 27, 2015
6,534
11,001
Habar ya jion wakuu,ni takriban mwezi umepita,baada ya kufahamiana na huyu binti kwenye mtandao wa kijamii (Facebook).
Cha ajabu tumejikuta tumeanzisha mahusiano na hatimaye kubadilishana namba za simu.
Yeye ni mwalimu yupo mkoa mmoja pande za huko kaskazini,ana umri wa miaka 25.
Mimi nko mkoa mwingine kikaz pia.Cha kustaajabisha huyu dada kwa kweli ni mzur,ila anasema kuwa hajapa wa kumuoa..anasema aliokuwa nao,wote wamemzingua.
Hivo nmeona nimfarij na tumejikuta tukianza mahusiano japo ni ya mbali,ila kwa jinsi tunavozid kuwasiliana..ninaona waz kuwa ni mtu ambaye kadhamiria haswa..sio utani.
Na amedhamiria kuja kunitembelea hivi punde ili hatimaye tuweze fahamiana rasmi.


Asa mimi najiuliza,ni kweli huyu binti ana malengo thabiti? Au kuna kitu anakitafuta kwangu?
Je,ni kweli huyu binti kwa jinsi alivyo mzur,inawezekana kukosa mtu mwenye future naye?

Nmetafakar mno,nkakosa majibu.nkaona ni vyema niwashirikishe wenzangu,mna mtazamo gan juu ya hili.


Nb.nina gal friend ingawa hatuja plan future yoyote.
 
Mkuu kuwa makini sana..Lolote linaweza kutokea whether Good or Bad..Jipange na ujiandae kisaikolojia
 
Sio mbaya mkikutana utapata nafasi ya kumfaham zaidi ndio utaweza kujudge kama atakua hafai utampiga chini
 
Ndg cha msingi ucjiulize maswal mengi uzur sio ndio chanzo cha kuwa na watu ila ni tabia ya mtu cha msingi mchunguze kanae kwa kipindi furani yy anakuja kwako siku moja na ww nenda kwake chunguza kimya kimya usipaniki na usiwe mwepesi kuuliza ukwel utaupata kwn uwezi mfahamu binadamu kwa cku 1 ila mtakavyo kaa kwa muda furani kwenye mahusiano ndio utamjuwa yukoje ila usimfikilie vibaya
 
Ndg cha msingi ucjiulize maswal mengi uzur sio ndio chanzo cha kuwa na watu ila ni tabia ya mtu cha msingi mchunguze kanae kwa kipindi furani yy anakuja kwako siku moja na ww nenda kwake chunguza kimya kimya usipaniki na usiwe mwepesi kuuliza ukwel utaupata kwn uwezi mfahamu binadamu kwa cku 1 ila mtakavyo kaa kwa muda furani kwenye mahusiano ndio utamjuwa yukoje ila usimfikilie vibaya
Shukrani mkuu..nmekusoma vyema.
 
Endelea na girlfriend uliyenaye,unayemuona mixer kumfahamu alafu panga nae future

Yule wa facebook achana nae
 
Unachohisi kwamba anakupenda ni kile kitendo cha yeye kutoka huko mbali na kukutembelea wewe,.. Hii inakushawishi uone hwenda anayo nia ya dhati.....
Pili dhamana ya kazi yake imekufanya uhisi kwamba hana tatizo la pesa, bali anahitaji la dhati la kuolewa.....
Jiulize Sasa...,
1. Ulishajua hao waliopita kwake walishindwa kwasababu zipi, zidi ya uzuri alionao?
2. Unaaminije kama kweli huyo ni mtumishi ameajiriwa?
Kitu gani kimemshawishi kwako na kukuamini wewe ambae hakujui umuoe, bila kuwa mwoga wa kuyarudia yale yalompitia huko Nyuma, ilihali wewe hakujui?
Kuwa makini sana..... Uzuri usikuponze ndg yangu...
 
Wanaume wenye akili timamu wote duniani wanaanza kuyapa thamani mahusiano ambyo angalau yana miezi sita sasa wewe jifanye unajua kupendwa....minadhani just enjoy na mcalculate huyo demu baada ya kuonana nae ujue kwanza ana akili timamu au mna mihemko...it takes time kumbuka mmekutana FB bora hata ingekuwa Jf kidogo nafuu..
 
Umemueleza Ukweli Wewe ni Nani!?? Unafanya shughuli gani na malengo yako kimaisha huenda kaona kuna fursa kwako... Zaidi Hata Username yako inasadifu mkuu
 
Back
Top Bottom