Je huu ni ungwana!

Je huu ni ungwana!

Habari wana Jukwaa la MAHUSIANO, MAPENZI NA URAFIKI?
Naomba radhi kwa nitakao wagusa! Nimeamua kuimarisha uhusiano ndani ya jukwaa hili ili tusiwe na tabia hizi zisizo za kiungwana!
Napenda kuwauliza maswali kadhaa ili tuone kama huu ni ungwana,
1.Anakuja mtu na thread ya kweli watu wanamtukana kuwa katunga hata kama stori ni ya kweli, Je huu ni ungwana?
2.Anakuja mtu kuchangia hana uzoefu wa matumizi ya simu au laptop anakutana na ukurasa mmoja anatusi kuwa Jukwaa limevamiwa na anadharau wachangiaji hadi alie leta topic, Je huu ni ungwana?
3.Mtu kuchangia nje ya mada, je huu ni ungwana?
4.Kudanganya wana Jukwaa kwa kuleta stori za uongo je huu ni ungwana?

Najua yapo maswali mengi ya kujiuliza kama wanaotenda ndani ya jukwaa hili wanatenda ungwana kwa wahusika, Tujifunze na kusoma alama za nyakati, tuwape elimu wahusika kama haamini stori hajaalikwa kuchangia, nawaomba mtoe ushirikiano kuwapa hawa jamaa elimu kupitia uzi huu!
Kama huna ungwana mahusiano, mapenzi na urafiki sahau! hivyo ni bora kuhama jukwaa kuliko kukera wana jukwaa!
Nawasilisha hoja!

1. Thread ya kweli utaijuwaje wakati mleta mada hajaweka namna ya kumfanya mtu ajuwe thread ni ya kweli...??? SI UUNGWANA KUMLAZIMISHA MTU AAMINI UKITAKACHO WAKATI HUNA DATA KUMUAMINISHA ULISEMALO

2. Sijaona uhusiano uliopo kati ya uzoefu wa matumizi ya laptop na matusi. Matusi hayatokani na uzoefu. Wazoefu na wasio wazoefu hayo makitu wapo wanaotukana na wapo wasiotukana. SI UUNGWANA KUDHANI KOMPYUTA NA SIMU NDO VINAWAFANYA WATU WATUKANE. Hii ni tabia binafsi ya mtu na haitokani na kujuwa au kutokujuwa kompyuta au simu

3. Kuchangia nje ya mada si vizuri na si uungwa. Lakini lazima vile vile tuangalie nini kinapelekea hili kutokea. Kuna watu wamejenga makundi humu JF. Mwingine huwa hachangii mpaka aone fulani kachangia, sasa huyo fulani akiuliza tu kitu kinachohusu kundi lao, ndo mtiririko kuelekea nje ya mada unaanzia hapo.

4. Hili la kuleta stori za uongo, linashabihiana na hoja yako ya kwanza. Si uungwana kuleta habari ya uongo. Hivi na wewe unajuwaje kama huu ni uongo? Maana kuna wengine kujieleza ni issue, tena kwa kuandika ni balaa kabisa...

mwisho wa yote... UNAPOLETA MADA HAPA JF, USIJE UKAKAA USUBIRIE KIANDIKWE UNACHOPENDA KIANDIKWE. Na ndiyo maana ya mijadala. Unaleta hoja, halafu unasikiliza michango inasema nini.

SI UUNGWANA KULETA MADA HALAFU UTAKE UNAVYOVIPENDA TU NDO VIANDIKWE. Kuna namna nyingi ya kukupa mawazo m'badala na namna nyingine zinakera.... Lakini ndo hivyo, UKIONA HUTAKI KUKERWA USIPOSTI KITU HUMU. Lakini kumbuka huko kuvumilia wengine na kero zao, ndo kunakufunza uvumilivu....

NDUGU YAKO TU WA TUMBO MOJA MNAKERANA, SEMBUSE MWANA JF USIEMFHAMU NA UNA UHAKKA JINA ANALOLITUMIA SI LAKE..!!! Si uungwana bana kudhani kila anayekukera ni adui yako.
 
Back
Top Bottom