julius mahinya
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 1,152
- 384
- Thread starter
- #41
Nashukuru kiasi kwa maelezo kiasi napo husisha matumizi ya vifaa vya mawasiliano na uungwana ni palemtu ana fungua thread ilo changiwa na watu kadhaa labda page 6, anakutana na page ya sita anatoa mawazo kulingana na michango ilioko kwenye hiyo page moja lakini akimaanisha ndio michango yote iko hivyo! mfano anatukana kwa kuwa amekuta katika page hiyo walio wengi wamedharau stori! ukitaka kujua kwanini kafanya hivyo anadai kamastori ingekuwa ya maana mbona hakuna alie kushauri, ukipitia kila page unakuta watu wameshauri vya kutosha! wasiojua matumizi ya vifaa na wakiwa na sifa ya kuiga misimamo ya maoni hutoa maoni yao kulingana na michango ya ukurasa walo ukuta!1. Thread ya kweli utaijuwaje wakati mleta mada hajaweka namna ya kumfanya mtu ajuwe thread ni ya kweli...??? SI UUNGWANA KUMLAZIMISHA MTU AAMINI UKITAKACHO WAKATI HUNA DATA KUMUAMINISHA ULISEMALO
2. Sijaona uhusiano uliopo kati ya uzoefu wa matumizi ya laptop na matusi. Matusi hayatokani na uzoefu. Wazoefu na wasio wazoefu hayo makitu wapo wanaotukana na wapo wasiotukana. SI UUNGWANA KUDHANI KOMPYUTA NA SIMU NDO VINAWAFANYA WATU WATUKANE. Hii ni tabia binafsi ya mtu na haitokani na kujuwa au kutokujuwa kompyuta au simu
3. Kuchangia nje ya mada si vizuri na si uungwa. Lakini lazima vile vile tuangalie nini kinapelekea hili kutokea. Kuna watu wamejenga makundi humu JF. Mwingine huwa hachangii mpaka aone fulani kachangia, sasa huyo fulani akiuliza tu kitu kinachohusu kundi lao, ndo mtiririko kuelekea nje ya mada unaanzia hapo.
4. Hili la kuleta stori za uongo, linashabihiana na hoja yako ya kwanza. Si uungwana kuleta habari ya uongo. Hivi na wewe unajuwaje kama huu ni uongo? Maana kuna wengine kujieleza ni issue, tena kwa kuandika ni balaa kabisa...
mwisho wa yote... UNAPOLETA MADA HAPA JF, USIJE UKAKAA USUBIRIE KIANDIKWE UNACHOPENDA KIANDIKWE. Na ndiyo maana ya mijadala. Unaleta hoja, halafu unasikiliza michango inasema nini.
SI UUNGWANA KULETA MADA HALAFU UTAKE UNAVYOVIPENDA TU NDO VIANDIKWE. Kuna namna nyingi ya kukupa mawazo m'badala na namna nyingine zinakera.... Lakini ndo hivyo, UKIONA HUTAKI KUKERWA USIPOSTI KITU HUMU. Lakini kumbuka huko kuvumilia wengine na kero zao, ndo kunakufunza uvumilivu....
NDUGU YAKO TU WA TUMBO MOJA MNAKERANA, SEMBUSE MWANA JF USIEMFHAMU NA UNA UHAKKA JINA ANALOLITUMIA SI LAKE..!!! Si uungwana bana kudhani kila anayekukera ni adui yako.
Kujua ukweli wa stori nakubali ni ngumu lakini kuwaasa wahusika ni jambo la busara! kama mtu huamini ni ya kweli nani kakualika kuchangia?