Je, huu ni ufuatiliaji wa uwajibikaji au udhalilishaji kwa bullying na intimidation?.

hyperbolic

JF-Expert Member
Feb 12, 2017
458
1,000
Analazimisha watu wakariri data, sidhani kama uwezo wa kukariri humaanisha ungozi bora, amemdharirisha ssna mama wa watu kiukweli
 

Mwana

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
5,382
2,000
Analazimisha watu wakariri data, sidhani kama uwezo wa kukariri humaanisha ungozi bora, amemdharirisha ssna mama wa watu kiukweli
Kwa mtu yoyote anayejua kazi ya Mkurugenzi Mtendaji ataelewa kwa nini Rais amemtoa. Road Fund usiijie?!?!? Are you serious. Wewe Mkurugenzi Mtendaji unashindwa na Meya Kwli. Bid No. Mama Ni mzembe asitake huruma. No
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,061
2,000
Sasa mkuu hapo umejibu kitu gani kama ulijibu ukiwa na nia ya kupata response?

Wewe mkuu wa Babati, umeamuwa kunifananisha na ng’ombe kwasababu wewe ni mfugaji?

Sitaki kwenda unakotaka, ukinilazimisha usinilaumu. Maana tusi baya kwangu kuliko hata hilo la kuniita ng’ombe, ni kuniita mimi ni ccm.

Chunga ulimi mkuu, endelea kutupa mawe ukiwa kwenye gorofa la vioo.

Eti barabara ziko chini ya TARURA, na pesa zilizopelekwa zilikuwa chini ya nani wewe kanume kenge?
Pole sana CCM
 

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,145
2,000
Nimesoma CV ya huyu Mama Mkurugenzi elimu yake inaonyesha alikuwa ana jibu anachokijua, watu wenye elimu nzuri watashindwa kufanya kazi kwenye serikali ya awamu ya tano.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,303
2,000
Nimeangalia hii video, nikalikumbuka bandiko hili, wajameni hii sio bullying and intimidation?, huu sio udhalilishaji huu?. Yaani waziri anagombezwa kama mtoto mdogo mbele ya kadamnasi ya watu!, is this fair kweli?

 

Dongo La Kiemba

JF-Expert Member
Nov 5, 2013
1,809
2,000
Nimeangalia hii video, nikalikumbuka bandiko hili, wajameni hii sio bullying and intimidation?, huu sio udhalilishaji huu?. Yaani waziri anagombezwa kama mtoto mdogo mbele ya kadamnasi ya watu!, is this fair kweli?

P

Mbona kusifiwa mbele ya watu iko sawa! Unajuaje kama hajamkanya sirini! Rais ndio mwenye dhamana afu wateule wake mnataka wamwangushe! Wasikanywe!!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Kinjeketile

JF-Expert Member
Dec 24, 2013
982
1,000
Nimeangalia hii video, nikalikumbuka bandiko hili, wajameni hii sio bullying and intimidation?, huu sio udhalilishaji huu?. Yaani waziri anagombezwa kama mtoto mdogo mbele ya kadamnasi ya watu!, is this fair kweli?

P

Hili ndiyo eneo pekee ambalo Jiwe analimuda na kuchukulia manyota na maujiko kutoka kwa wanyonge na masikini.

Ukiondoa ubabe,kutishia watu na kufanya maamuzi ya kukurupuka unafikiri kuna chochote kinachoweza kumpatia ujiko na manyota kutoka kwa masikini na wanyonge?
 

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
10,838
2,000
Nimeangalia hii video, nikalikumbuka bandiko hili, wajameni hii sio bullying and intimidation?, huu sio udhalilishaji huu?. Yaani waziri anagombezwa kama mtoto mdogo mbele ya kadamnasi ya watu!, is this fair kweli?

P
Ur So intelligent, Jiwe has created fear amongst his cabinet member and Tanzanian in general, he use the same to rule and not to lead.
Jize zima lenye mavuzi tena unakuta linampita JIWE kwa umri linakuwa jinga kiasi hicho, kweli kabisa lingejiuzulu likatumie mafao yake na wajukuu zake?
Shit hole Country [Trump]
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,303
2,000
Nimeangalia hii video, nikalikumbuka bandiko hili, wajameni hii sio bullying and intimidation?, huu sio udhalilishaji huu?. Yaani waziri anagombezwa kama mtoto mdogo mbele ya kadamnasi ya watu!, is this fair kweli?

P
Haingii akilin Kutukana watu, kukejeli, kudhihaki watu ambao kiuhalisia wapo walikuzidi Umri tena mbele ya Macho, hao unaowafanya ivo wana wake zao, wana watoto ndugu ,rafiki najamaa.

Mimi nadhani ni Jeuri zisizo na Msingi wowote, Haukuanza wewe kuwa Rais, mbona wapo watangulizi wako lkn Hawakuwahi kua ivo na wao walideal pia na mambo kama hayo...

Nawasihi viongozi wa Dini, Acheni kujisumbua kupiga magoti kila siku kumuombea MTU ambaye anachokifanya anakijua, nakm anajua niudhaifu basi kwann hakubali udhaifu wa wengine?.. Dini gan inahimiza kiongozi utukane ,ukejel n.k?

Nani ameomba Mvua inyeshe iharibu madaraja, nani anaomba wagonjwa , nani anawambia wagonjwa wakaee nyumban muda mrefu wakiona hali mbaya ndo wanakuja Hosp, MTU km huyo akisepa, basi anatafutwa Mtoa huduma, nani?

Najua Kiongozi una kariba ya Narcissism , kutafuta Sifa mbele ya Watu hata kwa kutukana , maamuzi yasokua na busara ,maamuzi ya mihemko , Kwako Kusifiwa hata kwa jambo Baya ni sahihi na Utampa Cheo muhusika.

Matokeo yake, Umefanya Watawala na viongozi wengi kuanzia makatibu, maDC maRC wamekua na lugha Chafu, Jeuri, kejeli ,dhihaka , kutukana watu ovyoovyo , na wanatukana pasipo kujali Utu wa mtendwa.

MZEE SAIDI MECKY SADIK , alifanya jambo LA Maana sana, Kujiudhuru huo uRC,, haiwezekan sababu tu ya Cheo mshahara basi Umvunjie MTU utu wake tena macho ni pa Watu na mbele ya Vyombo vya habari,..ni mazingira gan unayompa? Huwezi mtukana mtu Mzima Mzee mwenzako Ambaye Ulipoletewa Faili lake ulizipitia wewe mwenyewe, ukamchambua, NA ukaona anafaa, ukampa Uongozi .... Leo udhaifu utokeee, Umseme kama mtoto Mdogo ..nani Mnafiki hapa?

WEWE MWENYEWE ULIWAHI KUA WAZIRI WA UJENZI, UVUVI N.K...MBONA KUNA MADUDU MENGI ULIYAFANYA??? IVI WATANGULIZI WAKO WANGEAMUA KUKUSHUGULIKIA KWA MATUSI, NGUVU, DHIHAKA, JEURI ,KEJELI ZA WAZIWAZI.... WEWE UNGEFIKA HAPA ULIPO?

Ktk safari yako ya Maisha kisiasa , nikweli wewe ulikua Mkamilifu kiasi cha Leo hii wewe kua mkosoaji wakila kitu pale tu panapotokea udhaifu hata ktk mambo yasohitaji siasa?

Ukweli nikwamba, Unahitajika Kumuomba Mungu akupe Hekima na Busara ili uweze kuhesabika kiongozi bora moyoni mwa watu.

Kama suala ni kufukuza, wewe sindo mwenye mamlaka bana, Fukuza tu bila hata kumtukana tu..Fukuza bila hata kumvunjia MTU heshima na kumpa Aibu isofutika ndani ya jamii....HAO UNAOWAFANYIA IVO, KUMBUKA MAISHA YAO NIBADO YANATAKIWA KUENDELEA.

Mungu akusaidie na ubadilike..
Karibu..
P
 

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,513
2,000
Wanabodi,

Kwanza naomba kukiri kuunga mkono kwa dhati, juhudi zote na hatua zote zinazochukuliwa na rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya tano katika vita dhidi ya rushwa, ufisadi, utakatishaji fedha, uzembe, ubadhirifu na wizi wa rasilimali zetu na kusimamia uwajibikaji, ila katika utekelezaji wa juhudi hizo, sometimes kunatokea hapa na pale utekelezaji huo ukafanywa ndivyo sivyo, yaani doing the right thing, at the right time, but not doing it right. Hili ni bandiko la ukosoaji, nasisitiza Rais Magufuli na serikali yake wakosolewe kwa hoja sio kwa viroja ...
Mwito Kwa Wana JamiiForums Kuhusu Ukosoaji wa Rais Magufuli | Page ...

Jee Kuna Tofauti Kati ya Mtu Anayeitwa Dr. JPJ Magufuli na Rais Dr. JPJ Magufuli?.

Yes, kuna tofauti kati ya hawa watu wawili, kuna mtu anayeitwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli ambaye ni binadamu, mtu, Mtanzania mwenzetu na kuna Dr. John Pombe Joseph Magufuli ambaye ni rais wa JMT. These two people, they are two in one. Kwa vile rais Magufuli, licha ya kuwa ni mtu anayeitwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli, yeye ni binadamu, a human being, anaweza kufanya makosa yoyote ya kibinaadamu, na makosa hayo yakavumilika, yakastahimilika, yakaeleweka, na yakasameheka, kwasababu binadamu ni kiumbe dhaifu and no one is perfect.

Lakini mtu huyu huyo Dr. John Pombe Joseph Magufuli ni rais wa nchi, huyu sasa sio mtu, huyu ni taasisi, an institution inayoitwa Presidential Institution, taasisi hii inaishi Ikulu ambapo ni mahali patakatifu, hivyo ni purported to be perfect, haiwezi kukosea, hivyo rais Magufuli anaposema neno lolote, anapofanya jambo lolote as a president of the United Republic of Tanzania, anategemewa kuwa perfect kama malaika, mtukufu, au mtakatifu, hawezi kukosea ndio maana hawezi kushitakiwa, he is expected to be doing the right thing, at the right time and do it right always!. Makosa yoyote madogo madogo ya kibinaadamu, yanaweza kuwa tolerated yakifanywa na mtu mwingine yoyote, kwasababu ni binadamu, but makosa yoyote madogo madogo hayawezi kufanywa na rais wetu kwasababu ni institution, hivyo every other person can do any mistakes and be tolerated but not our president!.

Angalia kilichofanyika hapa:


Isn't This Bullying and Intimidation?.
Hapa nauliza tuu, kilichofanyika hapa, isn't this bullying na intimidation?. Kwa vile rais Magufuli yeye binafsi is very good in numbers, actually I think he is genius kwenye kutunza kumbukumbu za numbers za takwimu, namkumbuka jinsi alipokuwa waziri wa mifugo, kichwani kwake, alikuwa na idadi kamili ya ng'ombe, mbuzi, na kondoo!, tena nikasikia kuwa eti alikuwa anajua hadi idadi ya samaki wetu, ndio maana akaidaka ile meli ya samaki wa Magufuli!.

Alipokuwa Waziri wa Ujenzi, alikuwa na figures za urefu wa barabara zote za TANROADS na zimejengwa kwa kiasi gani. Then, kwa vile rais wetu, is soo good with numbers, sasa anataka kulazimisha kila kiongozi wa umma, awe kama yeye, must be very good with numbers and datas kama yeye!, hivyo hata akirupushwa tuu kutoka usingizini na kuulizwa figures, zozote, atajibu sahihi kutoka kichwani. Mfano ukimuuliza rais Magufuli hata kutoka usingizini, kuhusu idadi ya nyumba za serikali zilizouzwa, zilikuwa ngapi, zimeuzwa kwa kina nani na kwa bei gani atakutajia!. Lakini sio watu wote wana uwezo kama huo!.

Is This Fair?, hii ni Haki kweli, Huu Sio Udhalilishaji?.

Hili ni swali tuu nauliza, is this fair?, hii ni haki?, jee hii sio some sort of intimidation na udhalilishaji wa kiongozi wa umma mbele ya public ya watu?.

Hizi intimidations niliwahi kuzizungumza hapa. Anachofanya Waziri Mkuu, sio sawa, sio haki, sio good governance ...

Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya ...

Kusema ukweli, kuna vitu rais wetu huwa anavisema, havikupaswa kusemwa na rais, na kuna vitu anavifanya, havikupaswa kufanywa na rais, kama wasaidizi wake mpo, na mnaona, na imejiridhisha he is doing the right thing, hivyo wote tuendelee kumshangilia tuu rais wetu, lakini kwa baadhi yetu sisi ambao ni wakweli daima, tunakua hatujitendei haki nafsi zetu kama wote tutanyamaza na kuangalia tuu, hivyo sisi wengine mwisho wa uwezo wetu ni kusema tuu, na kuandika, hivyo kuweka kumbukumbu, kwa sababu hizi bullying na intimidations kwenye mambo madogo zikiachwa, mbele ya safari tutakuja kushuhudia makubwa zaidi, ndipo watu wataanza kushangaa, sisi tutawavutia tuu kumbukumbu kuwajulisha tuliona lini na tukasema. Huu mtindo wa watu kuona baadhi ya mambo yanafanywa ndivyo sivyo na kuyanyamazia tukidhani ndio kumsaidia rais wetu kumbe hatumsaidii na sometimes hata tunamchoresha before the eyes of the right thinking members of the society.

Tumbua Tumbua, Ziara za Kushutukiza na Utoaji Nje Siri za Serikali
Niliwahi kupinga utekelezaji wa baadhi ya tumbua tumbua, na kulalamikia double standards kwenye utumbuaji, wengine walifanya makosa madogo tuu wakatumbuliwa na wengine wanafanya makosa makubwa and are spared!. Kwenye ziara za kushtukiza, nikasema baadhi ni intimidating, hivyo kutajenga nidhamu ya woga, lakini pia nikapinga hii ya rais kusema chochote hata vitu ambavyo hakupaswa kusema kama disclosure of tapping telephone conversations, au kuwaanika secret agents etc, nilishauri Jee Aachwe Aseme Tuu, By "Taking The Bitter With The Sweet", Or ...

Marais Wengine Hufanya Vipi?
Nikiwa ripota wa newsroom, nimewahi kushiriki ziara nyingi za rais za ndani ya nchi na nje ya nchi. Wakati rais akifanya ziara popote, wahusika wote watakaohusiana na ziara hiyo huarifiwa. Rais akiishawasili hufanyiwa briefing, na kila jioni hufanya postmortem, hivyo kuna mambo mengine ni mambo ya ndani kuuliza kule kwenye briefings, na sio kila kitu kuuliza mbele ya kadamnasi ya watu, huu ni udhalilishaji na kuaibishana.

Rais Magufuli ni Mwalimu, Jee Aendeshe Nchi Kwa Mtindo wa Mwalimu na Mwanafunzi, au Mwalimu na Walimu Wenzake?
Rais Magufuli ni Mwalimu by professional, hivyo mtindo wake wa uulizaji maswali watendaji wake, anatumia ule mtindo wa uulizaji maswali wa mwalimu darasani kwa wanafunzi wake. Mtindo huu ni mzuri kwa waalimu na wanafunzi, kwasabu lengo ni kupima uelewa wa wanafunzi, hivyo uulizaji maswali wa rais Magufuli kwa baadhi ya watendaji wake ni uulizaji maswali wa mwalimu na wanafunzi wake na sio Mwalimu Mkuu na waalimu wenzake. Kuna maeneo kiukweli rais Magufuli anauliza maswali kwa ukali wa kupindukia kwa watendaji wake as if ni mwalimu na wanafunzi wake wakati in reality watendaji wake ni wasaidizi wake, hivyo rais Magufuli anapaswa kuwa treat kama walimu wenzake na sio kama watoto, wanafunzi wake. Mwalimu mkuu hawezi kumuaibisha mwalimu mwingine yoyote mbele ya wanafunzi wake. Hivyo japo ni kweli rais wa nchi kimamlaka ni mtu mkubwa sana, lakini as human being, hata rais ni binadamu tuu kama binadamu mwingine yoyote, kila binadamu anastahili utu na heshima, hivyo tufike mahali, rais wetu, aheshimiwe kwa urais wake na sio aogopwe kwa kutisha watendaji wake. Asijichukulie yeye ni mwalimu mkuu, na wengine wote ni wanafunzi wake, ajichukulie yeye ni mwalimu mkuu, na viongozi wengine ni waalimu wenzake wenye kustahili heshima na kuthaminiwa utu wao, huwezi kuwagombeza wasaidizi wako wakiwemo mawaziri au wakurugenzi kama watoto wadogo mbele ya makamera, huku ni kuwadhalilisha, hii bullying na intimidation!.

Jee, Kumtetea Huyu Mama ni Kulea Uzembe?.
Mimi ni muumini wa haki bin haki, kama ilivyo kwa rais Magufuli, haitegemewi yeye awe ni malaika, vivyo hivyo, hata kwa hao watendaji sii malaika, na kiukweli ni wakosaji, ila kilichofanyika jana, ni kama kile kile alichomfanyia Gavana wa BOT, rais anakuwa ameelezwa info fulani na watendaji wake, kisha anafanya ziara ya kushtukiza, na kumvaa Gavana, thank God, Gavana alikuwa imara na huku anajua analindwa na security of tenure. Hili la viongozi kupewa info halafu kuwashtukiza watendaji ili kuwaaibisha, niliwahi kulizungumza hapa Anachofanya Waziri Mkuu, sio sawa, sio haki, sio good governance ...

A Way Forward:
Kwa vile rais wetu pia ni binadamu, naendelea kuwasisitiza wale wasaidizi wake, waendelee kumsaidia rais wetu, kutenganisha the two interchangeable personalities within him kati ya mtu anayeitwa Dr John Pombe Joseph Magufuli ambaye ni binadamu, na Mhe, Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli ambaye ni mtukufu, na anaishi mahali patakatifu. Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public ...

Dr. Magufuli kama Magufuli, anaweza kuwaza lolote, kufanya lolote popote, au anaweza kusema chochote popote hata kutumia lugha chafu au kutukana watu wapumbavu, lakini Rais Mhe. Dr. Magufuli, hawezi kufanya lolote or kusema chochote, he got to do only the right thing at the right time and do it right!.

Namtakia ziara njema.

Paskali
Kwanza niwekewazi mkurugenzi ambaye unapokea taarifa kwa watendaji wako wa chini vipi unakuwa huna taarifa ya nini kinaendelea? Kila siku mnavikao au mnakunywa chai tu? Jambo la msingi ni wateule wa JPM ni matatizo ila naamini baada ya 2020 atakuwa amaejifunza
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom