Je, huu ni ufuatiliaji wa uwajibikaji au udhalilishaji kwa bullying na intimidation?.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,002
2,000
Wanabodi,

Kwanza naomba kukiri kuunga mkono kwa dhati, juhudi zote na hatua zote zinazochukuliwa na rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya tano katika vita dhidi ya rushwa, ufisadi, utakatishaji fedha, uzembe, ubadhirifu na wizi wa rasilimali zetu na kusimamia uwajibikaji, ila katika utekelezaji wa juhudi hizo, sometimes kunatokea hapa na pale utekelezaji huo ukafanywa ndivyo sivyo, yaani doing the right thing, at the right time, but not doing it right. Hili ni bandiko la ukosoaji, nasisitiza Rais Magufuli na serikali yake wakosolewe kwa hoja sio kwa viroja ...
Mwito Kwa Wana JamiiForums Kuhusu Ukosoaji wa Rais Magufuli | Page ...

Jee Kuna Tofauti Kati ya Mtu Anayeitwa Dr. JPJ Magufuli na Rais Dr. JPJ Magufuli?.

Yes, kuna tofauti kati ya hawa watu wawili, kuna mtu anayeitwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli ambaye ni binadamu, mtu, Mtanzania mwenzetu na kuna Dr. John Pombe Joseph Magufuli ambaye ni rais wa JMT. These two people, they are two in one. Kwa vile rais Magufuli, licha ya kuwa ni mtu anayeitwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli, yeye ni binadamu, a human being, anaweza kufanya makosa yoyote ya kibinaadamu, na makosa hayo yakavumilika, yakastahimilika, yakaeleweka, na yakasameheka, kwasababu binadamu ni kiumbe dhaifu and no one is perfect.

Lakini mtu huyu huyo Dr. John Pombe Joseph Magufuli ni rais wa nchi, huyu sasa sio mtu, huyu ni taasisi, an institution inayoitwa Presidential Institution, taasisi hii inaishi Ikulu ambapo ni mahali patakatifu, hivyo ni purported to be perfect, haiwezi kukosea, hivyo rais Magufuli anaposema neno lolote, anapofanya jambo lolote as a president of the United Republic of Tanzania, anategemewa kuwa perfect kama malaika, mtukufu, au mtakatifu, hawezi kukosea ndio maana hawezi kushitakiwa, he is expected to be doing the right thing, at the right time and do it right always!. Makosa yoyote madogo madogo ya kibinaadamu, yanaweza kuwa tolerated yakifanywa na mtu mwingine yoyote, kwasababu ni binadamu, but makosa yoyote madogo madogo hayawezi kufanywa na rais wetu kwasababu ni institution, hivyo every other person can do any mistakes and be tolerated but not our president!.

Angalia kilichofanyika hapa:


Isn't This Bullying and Intimidation?.
Hapa nauliza tuu, kilichofanyika hapa, isn't this bullying na intimidation?. Kwa vile rais Magufuli yeye binafsi is very good in numbers, actually I think he is genius kwenye kutunza kumbukumbu za numbers za takwimu, namkumbuka jinsi alipokuwa waziri wa mifugo, kichwani kwake, alikuwa na idadi kamili ya ng'ombe, mbuzi, na kondoo!, tena nikasikia kuwa eti alikuwa anajua hadi idadi ya samaki wetu, ndio maana akaidaka ile meli ya samaki wa Magufuli!.

Alipokuwa Waziri wa Ujenzi, alikuwa na figures za urefu wa barabara zote za TANROADS na zimejengwa kwa kiasi gani. Then, kwa vile rais wetu, is soo good with numbers, sasa anataka kulazimisha kila kiongozi wa umma, awe kama yeye, must be very good with numbers and datas kama yeye!, hivyo hata akirupushwa tuu kutoka usingizini na kuulizwa figures, zozote, atajibu sahihi kutoka kichwani. Mfano ukimuuliza rais Magufuli hata kutoka usingizini, kuhusu idadi ya nyumba za serikali zilizouzwa, zilikuwa ngapi, zimeuzwa kwa kina nani na kwa bei gani atakutajia!. Lakini sio watu wote wana uwezo kama huo!.

Is This Fair?, hii ni Haki kweli, Huu Sio Udhalilishaji?.

Hili ni swali tuu nauliza, is this fair?, hii ni haki?, jee hii sio some sort of intimidation na udhalilishaji wa kiongozi wa umma mbele ya public ya watu?.

Hizi intimidations niliwahi kuzizungumza hapa. Anachofanya Waziri Mkuu, sio sawa, sio haki, sio good governance ...

Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya ...

Kusema ukweli, kuna vitu rais wetu huwa anavisema, havikupaswa kusemwa na rais, na kuna vitu anavifanya, havikupaswa kufanywa na rais, kama wasaidizi wake mpo, na mnaona, na imejiridhisha he is doing the right thing, hivyo wote tuendelee kumshangilia tuu rais wetu, lakini kwa baadhi yetu sisi ambao ni wakweli daima, tunakua hatujitendei haki nafsi zetu kama wote tutanyamaza na kuangalia tuu, hivyo sisi wengine mwisho wa uwezo wetu ni kusema tuu, na kuandika, hivyo kuweka kumbukumbu, kwa sababu hizi bullying na intimidations kwenye mambo madogo zikiachwa, mbele ya safari tutakuja kushuhudia makubwa zaidi, ndipo watu wataanza kushangaa, sisi tutawavutia tuu kumbukumbu kuwajulisha tuliona lini na tukasema. Huu mtindo wa watu kuona baadhi ya mambo yanafanywa ndivyo sivyo na kuyanyamazia tukidhani ndio kumsaidia rais wetu kumbe hatumsaidii na sometimes hata tunamchoresha before the eyes of the right thinking members of the society.

Tumbua Tumbua, Ziara za Kushutukiza na Utoaji Nje Siri za Serikali
Niliwahi kupinga utekelezaji wa baadhi ya tumbua tumbua, na kulalamikia double standards kwenye utumbuaji, wengine walifanya makosa madogo tuu wakatumbuliwa na wengine wanafanya makosa makubwa and are spared!. Kwenye ziara za kushtukiza, nikasema baadhi ni intimidating, hivyo kutajenga nidhamu ya woga, lakini pia nikapinga hii ya rais kusema chochote hata vitu ambavyo hakupaswa kusema kama disclosure of tapping telephone conversations, au kuwaanika secret agents etc, nilishauri Jee Aachwe Aseme Tuu, By "Taking The Bitter With The Sweet", Or ...

Marais Wengine Hufanya Vipi?
Nikiwa ripota wa newsroom, nimewahi kushiriki ziara nyingi za rais za ndani ya nchi na nje ya nchi. Wakati rais akifanya ziara popote, wahusika wote watakaohusiana na ziara hiyo huarifiwa. Rais akiishawasili hufanyiwa briefing, na kila jioni hufanya postmortem, hivyo kuna mambo mengine ni mambo ya ndani kuuliza kule kwenye briefings, na sio kila kitu kuuliza mbele ya kadamnasi ya watu, huu ni udhalilishaji na kuaibishana.

Rais Magufuli ni Mwalimu, Jee Aendeshe Nchi Kwa Mtindo wa Mwalimu na Mwanafunzi, au Mwalimu na Walimu Wenzake?
Rais Magufuli ni Mwalimu by professional, hivyo mtindo wake wa uulizaji maswali watendaji wake, anatumia ule mtindo wa uulizaji maswali wa mwalimu darasani kwa wanafunzi wake. Mtindo huu ni mzuri kwa waalimu na wanafunzi, kwasabu lengo ni kupima uelewa wa wanafunzi, hivyo uulizaji maswali wa rais Magufuli kwa baadhi ya watendaji wake ni uulizaji maswali wa mwalimu na wanafunzi wake na sio Mwalimu Mkuu na waalimu wenzake. Kuna maeneo kiukweli rais Magufuli anauliza maswali kwa ukali wa kupindukia kwa watendaji wake as if ni mwalimu na wanafunzi wake wakati in reality watendaji wake ni wasaidizi wake, hivyo rais Magufuli anapaswa kuwa treat kama walimu wenzake na sio kama watoto, wanafunzi wake. Mwalimu mkuu hawezi kumuaibisha mwalimu mwingine yoyote mbele ya wanafunzi wake. Hivyo japo ni kweli rais wa nchi kimamlaka ni mtu mkubwa sana, lakini as human being, hata rais ni binadamu tuu kama binadamu mwingine yoyote, kila binadamu anastahili utu na heshima, hivyo tufike mahali, rais wetu, aheshimiwe kwa urais wake na sio aogopwe kwa kutisha watendaji wake. Asijichukulie yeye ni mwalimu mkuu, na wengine wote ni wanafunzi wake, ajichukulie yeye ni mwalimu mkuu, na viongozi wengine ni waalimu wenzake wenye kustahili heshima na kuthaminiwa utu wao, huwezi kuwagombeza wasaidizi wako wakiwemo mawaziri au wakurugenzi kama watoto wadogo mbele ya makamera, huku ni kuwadhalilisha, hii bullying na intimidation!.

Jee, Kumtetea Huyu Mama ni Kulea Uzembe?.
Mimi ni muumini wa haki bin haki, kama ilivyo kwa rais Magufuli, haitegemewi yeye awe ni malaika, vivyo hivyo, hata kwa hao watendaji sii malaika, na kiukweli ni wakosaji, ila kilichofanyika jana, ni kama kile kile alichomfanyia Gavana wa BOT, rais anakuwa ameelezwa info fulani na watendaji wake, kisha anafanya ziara ya kushtukiza, na kumvaa Gavana, thank God, Gavana alikuwa imara na huku anajua analindwa na security of tenure. Hili la viongozi kupewa info halafu kuwashtukiza watendaji ili kuwaaibisha, niliwahi kulizungumza hapa Anachofanya Waziri Mkuu, sio sawa, sio haki, sio good governance ...

A Way Forward:
Kwa vile rais wetu pia ni binadamu, naendelea kuwasisitiza wale wasaidizi wake, waendelee kumsaidia rais wetu, kutenganisha the two interchangeable personalities within him kati ya mtu anayeitwa Dr John Pombe Joseph Magufuli ambaye ni binadamu, na Mhe, Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli ambaye ni mtukufu, na anaishi mahali patakatifu. Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public ...

Dr. Magufuli kama Magufuli, anaweza kuwaza lolote, kufanya lolote popote, au anaweza kusema chochote popote hata kutumia lugha chafu au kutukana watu wapumbavu, lakini Rais Mhe. Dr. Magufuli, hawezi kufanya lolote or kusema chochote, he got to do only the right thing at the right time and do it right!.

Namtakia ziara njema.

Paskali
 

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
16,800
2,000
Daaah ningekua mimi na kazi naacha... Mama wa watu anajikanyaga ka mtoto asee!!

Kuna kitu hujui, kuna LEADER na MANAGER!! Magufuli is not a leader, he is a manager!! Na angefaa sana angekua waziri mkuu!! Rais huwezi fanya upuuzi kama ule!! Inadhihirisha ni kiasi gan magu alivyo na stress na hapo ndio kapata pa kuzitolea!!

Sasa embu jiulize yule mama ataweza kufanya kazi kwa ufanisi tena kweli?? Psychologically atakua okey tena??
 

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
33,972
2,000
Hapa kazi tu.

Wakurugenzi hao wamejidhalilisha wenyewe,Halmashauri na mamlaka ya uteuzi.

Katika muktadha wa ziara ya kiongozi mkuu katika eneo lako haitarajiwi ukakosa data zote muhimu au maeneo mahsusi ya miradi iliyoletewa fedha na Serikali kuu.

DED kama accounting officer ana wajibu wa kujua kila senti iingiayo na kutoka halmashauri kwa kichwa kwani ni kazi yake ya kila siku na ni maswali anayoyajibu kwa wawakilishi wa wananchi au wananchi moja kwa moja.

Isitoshe mkurugenzi ana vikao vya kila juma au kila siku au kila mwezi vinavyombrief kuhusu maswala ya miradi ya maendeleo na fedha zinazotarajiwa kupatikana au zilizopatikana kutoka vyanzo vyote.yaani kuhusu fedha ya miradi kwa mkurugenzi ni sawa na sala ya baba yetu na muumini wa kikiristu.

Unapokuwa na mkurugenzi asitefahamu ni kiasi gani cha fedha za road fund zimefika kwenye halmashauri yake hutegemei kama ataweza kusimamia mradi wa barabara husika na mambo ndipo yanapokwamia na lawama au matusi yatarudi kwa mh Rais.

DED kama accounting officer aka afisa masuhuri wa halmashauri huandikiwa kwa barua kiasi cha fedha za mradi zinazoingia halmashauri sometimes days or weeks before disbursement ya hizo funds.

DED hupelekewa na mweka hazina statement au taarifa ya fedha yoyote inayoingia halmashauri.
Pia fedha yoyote inayoingia halmashauri hujadilowa kwenye vikao vya kamati za mipango na fedha na hatimaye baraz zima la madiwani ambalo katibu wake ni DED.

Kwa maoni yangu hakuna excuse ya DED kushindwa kujua figure ya fedha nyingi za mradi wa barabara zaidi ya kiwango kikuu cha uzembe.

Kama DED hajui ni kiasi gani cha fedha za mradi wa road fund ambayo ni nyingi how come anaweza kujua deni au fedha ya mtumishi(say nauli ya likizo) kama mdogo mfano mwalimu wa shule ya msingi aliyeko kwenye halmashauri yake???

Wakurugenzi hawa waneonesha kiwango kikubwa cha irresponsibility na wamestahili adhabu waliyopata.

Hilo ni funzo kwetu sote especially watumishi wa umma.

JPM ni no nonesense President, every subordinate must have known him better and therefore he/she should be super prepared .

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
47,262
2,000
Mkuu Paschal hao wakurugenzi kuna taarifa kuwa walikuwa wanafanyakazi kwa kushirikiana wa madiwani wa Chadema bila kubaguana, tatizo mzee hataki kuona watu waccm wanaelewana na wapinzani, mkuu umewahi kuona maswali kama hayo ameulizwa Bashite, Ally Happy, Mnyeti, Gumbo?

Hawa walikuwa wanatafutwa kwa muda mrefu, Mkurugenzi anawakuu wa idara kuna Engineer wa barabara kwa nini asiulizwe yeye?
 

Nakapanya

JF-Expert Member
May 22, 2012
2,099
2,000
Na utaratibu huu unaigwa hata na wasaidizi wake na unaendelea kwa spidi ya ajabu.

Ajabu katika awamu hii; ukitaka kupandishwa cheo basi fanya mambo hata kama ni ya hovyo lakini yenye kumpendeza mkuu...hapo utafanikiwa..ukitaka usitumbuliwe mnyenyekee mfalme na mwana mfalme....hapo utapona

PUBLICITY STUNTS
 

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
34,474
2,000
Naomba ieleweke kwamba sitetei wakurugenzi wa Bukoba kutumbuliwa kwa sababu sababu za kutenguliwa kwao sizifahamu.

Hoja yangu itajikita jinsi Rais Magufuli, naweza kusema anavyowapelekesha viongozi majukwaani kwa maswali ambayo yanahitaji Takwimu ambazo muda mwingine kiongozi anaweza kutokuwa nazo kichwani

Case Study iliyotokea Bukoba leo sio jambo la kuacha lipite.

Kwa wasiofahamu baadhi ya maswali ya kawaida kabisa wanayoulizwa mawaziri bungeni huandakiwa majibu mapema kabisa kabla ya kusomwa bungeni.

Waziri au mabosi wanapoalikwa kuhojiwa jambo fulani katika interview za vyombo vya habari hupewa area of concentration

Ni viongozi wachache sana wenye uwezo wa "kumeza" takwimu, angalau wakuu wa idara ndio angalau wanakuwa na takwimu

Ikumbukwe pia kwamba hata mgombea mmoja wa urais alituambia Sadam alikuwa rais wa Kuwait. Hata katika mikutano mbalimbali kuna kiongozi alihutubia kwamba awamu ya kwanza ilipoanza bei ya sukari ilikuwa 5000. Mambo ambayo sio kweli. Tukamezea kwa kuna tunaamini kuna kupitia

Hiyo busara itumike viongozi wakubwa wanapowahoji viongozi wa chini hasa mbele ya majukwaa
 

Eudorite

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
1,134
2,000
Bwana Pascali. Swali aliloulizwa yule mama mara tatu mfululizo tena kwa kuonywa juu ya majibu yake kwa Rais si swali baya kwa MKURUGENZI.

Haiwezekani mkurugenzi asijue ameletewa pesa kiasi gani kwa ajili ya BARABARA na akiba iliyopo ni kiasi gani.

Mkurugenzi anatakiwa afahamu akiba ya pesa zote alizonazo kila siku. Anatakiwa afahamu mapato na matumizi on daily basis.

Tatizo ni kuteua wakurugenzi ambao hawajawahi fanya kazi serikalini hivyo kutojua nini cha kufanya ofisini. Badala yake anataka mhasibu ndiye amsemee kwa bosi wake kwamba kuna pesa kiasi gani.

Isitoshe, Pesa za Halmashauri hazipo kwenye makundi mengi. Sana sana ni pesa ya barabara, Maji, Afya, Makusanyo ya ndani na miradi mingineyo ya hapa na pale.
 

farusofia

JF-Expert Member
Sep 18, 2017
541
500
We paskali tena ukiwa verified membe of jamii forum haogopi kufuatwa.

Haya yote wanayajua, wanajua protokali jinsi gani mambo yanatakiwa yafanyike, lakini kama mkuu wa kaya hataki kuwasikiliza je wamsaidie vipi, au unataka wamshikie mtutu halafu waishie kupotezwa, tuache kama yalivyo, then majibu yatapatikana, but this is the REAL personality of our Presidaa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom