Je, huu ni ufuatiliaji wa uwajibikaji au udhalilishaji kwa bullying na intimidation?

Bwana Pascali. Swali aliloulizwa yule mama mara tatu mfululizo tena kwa kuonywa juu ya majibu yake kwa Rais si swali baya kwa MKURUGENZI.

Haiwezekani mkurugenzi asijue ameletewa pesa kiasi gani kwa ajili ya BARABARA na akiba iliyopo ni kiasi gani.

Mkurugenzi anatakiwa afahamu akiba ya pesa zote alizonazo kila siku. Anatakiwa afahamu mapato na matumizi on daily basis.

Tatizo ni kuteua wakurugenzi ambao hawajawahi fanya kazi serikalini hivyo kutojua nini cha kufanya ofisini. Badala yake anataka mhasibu ndiye amsemee kwa bosi wake kwamba kuna pesa kiasi gani.

Isitoshe, Pesa za Halmashauri hazipo kwenye makundi mengi. Sana sana ni pesa ya barabara, Maji, Afya, Makusanyo ya ndani na miradi mingineyo ya hapa na pale.
WW mbwiga ndio maana huwa kuna vikao vya ndani hapo hadharani mnaulizana maswali ili iweje, kama ni sawa na sisi tuna maswali mengi tu yakumuuliza yeye hadharani kulingana na wadhifa wake aruhusu aone kama hataaibika, Muwe mnafikiria angekuwa mama yako yule ww sasa hivi ungekuwa na hali gani? Furahieni tu ngoja na ww siku ukiulizwa.
 
hivi alisema hajui au hajakariri kichwani? achene kupotosha na kushabikia udhalilishaji wa viongozi wenu?
Ukijua una haja ya kukariri tena? Siyo wote wenye kukariri wanajuwa, mara nyingi wenye kukariri hawajui na ndiyo maana wanakariri.

Mwenye kujuwa hakariri, bali anakumbuka, na mimi nimeshangazwa yeye kushindwa kukumbuka fedha za mradi ambao ni muhimu sana. Kichwa yako haielewi nini hapo?
 
Pascal sikujui ila nakukumbuka niko chuo kikuu ulipotangaza DSTV kwamba seif alishinda uchaguzi 1995.
Mayalla angekuwa mkurugenzi mawasiliano ikulu kama ukawa wangeshinda inamsumbua hadi Leo.Yeye ndie alikuwa mmojawapo wa waandishi wapiga filimbi wa hamelini wa Ukawa kipindi cha kampeni
 
Hahahahaha!! Nimecheka , CCM walimuweka tu nyie mkamchagua, hapo CCM lawama anaipata wapi?!!
Walikuwa watu kibao wa kuwachagua ilikuwaje mkamchagua huyo?!!!
Mkuu acha tu, yaani kuanzia diwani mpaka rais nilichagua UKAWA basi tu kura hazikumtosha niliyempigia
 
Sina uhakika sana kuhusu hilo la kuwa targeted kisiasa. Lakini kwa upande mwingine ni wazembe.

Au pengine hawajui vipambele muhimu ndo maana tunakwama...

Anashindwa kufahamu pesa za barabara?

Mradi muhimu kabisa?

A very important infrastructure?

Pesa zimekuja, zimefika hadi kwenye idara yeye asijue? Tena mkurugenzi?

Anataka mwaka hazina ndo aulizwe? Au sijui mkuu wa idara?

Ambao wao wanapewa pesa hizo baada ya mkurugenzi kuidhinisha?

Hakukuwepo na vikao vya uamuzi wa fund allocation kuelekea idara mbali mbali?

Kwakweli mimi binafsi nilishangazwa sana kwa uzembe wao mkubwa.

I would’ve fired them too!
Wewe ni CCM kweli kweli, kwa taarifa yako siku hizi barabara za vijijini zipo chini ya TARURA, ng'ombe wa CCM asiyekuwa na mkia.
 
Acheni ujinga kabisaa!!mkurugenzi gani ambaye hajui ni kiasi gani cha fedha ameletewa na zimebaki kiasi gani??Alishajua Boss anakuja kwa nini asiandike kwenye karatasi hata kama hajui kumemooraizi?? Acheni kutetea wavivu aisee!!
 
Wanabodi,

Kwanza naomba kukiri kuunga mkono kwa dhati, juhudi zote na hatua zote zinazochukuliwa na rais Magufuli katika vita dhidi ya rushwa, ufisadi, wizi wa rasilimali zetu na kusimamia uwajibikaji, ila katika utekelezaji wa juhudi hizo, sometimes kunatokea hapa na pale utekelezaji huo ukafanywa ndivyo sivyo, yaani doing the right thing, and the right time, but not doing it right.

Jee Kuna Tofauti Kati ya Mtu Anaitwa Dr. J.P.j. Magufuli na Rais Magufuli?.
Yes, kuna tofauti kati ya hawa watu wawili, they are two in one. Kwa vile rais Magufuli, licha ya kuwa ni mtu anayeitwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli, a human being, anaweza kufanya makosa ya kibinaadamu, lakini pia yeye ni taasisi inayoitwa Presidential Institution, taasisi hii inaishi Ikulu ambapo ni mahali patakatifu, hivyo ni purported to be perfect, haiwezi kukosea, hivyo rais Magufuli anategemewa kuwa perfect kama mtukufu, au mtakatifu, by doing the right thing, at the right time and do it right!. Makosa yoyote madogo madogo ya kibinaadamu, yanaweza kuwa tolerated yakifanywa na mtu mwingine yoyote, but not our president.

Angalia kilichofanyika hapa:



Isn't This Bullying and Intimidation?.
Hapa nauliza tuu, isn't this bullying na intimidation?. Kwa vile rais Magufuli yeye binafsi is very good in numbers, actually I think he is genius kwenye kutunza kumbukumbu za numbers za takwimu, namkumbuka jinsi alipokuwa waziri wa mifugo, kichwani kwake, alikuwa na idadi kamili ya ng'ombe, mbuzi, na kondoo!, tena nikasikia kuwa eti alikuwa anajua hadi idadi ya samaki wetu, ndio maana akaidaka ile meli ya samaki wa Magufuli!.

Alipokuwa Waziri wa Ujenzi, alikuwa na figures za urefu wa barabara zote za TANROADS na zimejengwa kwa kiasi gani. Then, kwa vile rais wetu, is just soo good with numbers, sasa anataka kulazimisha kila kiongozi wa umma, must be very good with numbers and datas kama yeye!, hivyo hata akirupushwa tuu kutoka usingizini na kuulizwa figures, zozote, atajibu sahihi kutoka kichwani. Mfano ukimuuliza rais Magufuli hata kutoka usingizini, kuhusu idadi ya nyumba za serikali zilizouzwa, zilikuwa ngapi, zimeuzwa kwa kina nani na kwa bei gani atakutajia!. Lakini sio watu wote wana uwezo kama huo!.

Is This Fair?, Huu Sio Udhalilishaji?.
Hili ni swali tuu nauliza, is this fair?, hii ni haki?, jee hii sio some sort of intimidation na udhalilishaji wa kiongozi wa umma mbele ya public ya watu?. Hizi intimidations niliwahi kuzizungumza hapa. Anachofanya Waziri Mkuu, sio sawa, sio haki, sio good governance ...
Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya ...
Kusema ukweli, kuna vitu rais wetu huwa anavisema, havikupaswa kusemwa na rais, na kuna vitu anavifanya, havikupaswa kufanywa na rais, kama wasaidizi wake mpo, na mnaona, na imejiridhisha he is doing the right thing, hivyo wote tuendelee kumshangilia tuu rais wetu, kwa baadhi yetu sisi ambao ni wakweli daima, tunakua hatujitendei haki nafsi zetu, hivyo mwisho wa uwezo wetu ni kusema tuu, kwa sababu hizi bullying na intimidations kwenye mambo madogo zikiachwa, mbele ya safari tutakushuhudia makubwa zaidi, tukidhani ndio kumsaidia rais wetu kumbe tunamchoresha!.

Tumbua Tumbua, Ziara za Kushutukiza na Utoaji Nje Siri za Serikali.
Niliwahi kupinga utekelezaji wa baadhi ya Tumbua tumbua, na kulalamikia double standards. Kwenye ziara za kushtukiza, nikasema ni intimidating, hivyo kutajenga nidhamu ya woga, lakini pia nikapinga hii ya rais kusema chochote hata vitu ambavyo hakupaswa kusema kama disclosure of tapping telephone conversations, au kuwaanika secret agents etc, nilishauri

Marais Wengine Hufanya Vipi?.
Nikiwa ripota wa newsroom, nimewahi kushiriki ziara nyingi za rais za ndani ya nchi na nje ya nchi. Wakati rais akifanya ziara popote, wahusika wote watakaohusiana na ziara hiyo huarifiwa. Rais akiishawasili hufanyiwa briefing, na kila jioni hufanya postmortem, hivyo kuna mambo mengine ni mambo ya ndani kuuliza kule kwenye briefings, na sio kila kitu kuuliza mbele ya kadamnasi ya watu, huu ni udhalilishaji na kuaibishana.

Rais Magufuli ni Mwalimu, Jee Aendeshe Nchi Kwa Mtindo wa Mwalimu na Mwanafunzi, au Mwalimu na Walimu Wenzake?.
Rais Magufuli ni Mwalimu by professional, hivyo mtindo wake wa uulizaji maswali watendaji wake, anatumia ule mtindo wa uulizaji maswali wa mwalimu darasani kwa wanafunzi wake. Mtindo huu ni mzuri kwa waalimu na wanafunzi, lakini mwalimu mkuu hawezi kumuaibisha mwalimu mwingine yoyote mbele ya wanafunzi wake. Hivyo japo ni kweli rais wa nchi kimamlaka ni mtu mkubwa sana, lakini as human being, hata rais ni binadamu tuu kama binadamu mwingine yoyote, kila binadamu anastahili utu na heshima, hivyo tufike mahali, rais wetu, aheshimiwe kwa urais wake na sio aogopwe kwa kutisha watendaji wake. Asijichukulie yeye ni mwalimu mkuu, na wengine wote ni wanafunzi wake, ajichukulie yeye ni mwalimu mkuu, na viongozi wengine ni waalimu wenzake wenye kustahili utu na heshima.

Jee, Kumtetea Huyu Mama ni Kulea Uzembe?.
Mimi ni muumini wa haki bin haki, kama ilivyo kwa rais Magufuli, haitegemewi yeye awe ni malaika, vivyo hivyo, hata kwa hao watendaji sii malaika, na kiukweli ni wakosaji, ila kilichofanyika jana, ni kama kile kile alichomfanyia Gavana wa BOT, rais anakuwa ameelezwa info Fulani na watendaji wake, kisha anafanya ziara ya kushtukiza, na kumvaa Gavana, thank God, Gavana analindwa na security of tenure. Hili la viongozi kupewa info halafu kuwashtukiza watendaji ili kuwaaibisha, niliwahi kulizungumza hapa Anachofanya Waziri Mkuu, sio sawa, sio haki, sio good governance ...

A Way Forward:
Kwa vile rais wetu pia ni binadamu, naendelea kuwasisitiza wale wasaidizi wake, waendelee kumsaidia rais wetu, kutenganisha the two interchangeable personalities within him kati ya mtu anayeitwa Dr John Pombe Joseph Magufuli ambaye ni binadamu, na Mhe, Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli ambaye ni mtukufu, na anaishi mahali patakatifu.

Dr. Magufuli kama Magufuli, anaweza kuwaza lolote, kufanya lolote popote, au anaweza kusema chochote popote, lakini Rais Mhe. Dr. Magufuli, hawezi kufanya lolote or kusema chochote, he got to do only the right thing at the right time and do it right!.

Namtakia ziara njema.

Paskali

Paskali, Umeandika hivi
"Marais Wengine Hufanya Vipi?.
Nikiwa ripota wa newsroom, nimewahi kushiriki ziara nyingi za rais za ndani ya nchi na nje ya nchi. Wakati rais akifanya ziara popote, wahusika wote watakaohusiana na ziara hiyo huarifiwa. Rais akiishawasili hufanyiwa briefing, na kila jioni hufanya postmortem, hivyo kuna mambo mengine ni mambo ya ndani kuuliza kule kwenye briefings, na sio kila kitu kuuliza mbele ya kadamnasi ya watu, huu ni udhalilishaji na kuaibishana."


Binafsi nina swali rahisi tu! Unataka tuendelee kufanyakazi kwa mtindo huu miaka yote? Marais wengine ulioambatana nao, walifanikiwa kwa kiasi gani kujibu matatizo yetu? Kumbuka, tuna umri wa zaidi ya miaka 50. Takriban nusu ikiwa ni chini ya Rais Nyerere na nusu chini ya Marais Mwinyi, Mkapa na Kikwete. Hii nusu ya marais watatu umesikia wapi ikitolewa kama mfano wa mafanikio hadi ufikie tamaa ya huyu wa sasa afanye kazi kama wao?

Unafikia hatua ya kutetea Mkurugenzi Mzembe!! Hii ni karibu mwisho wa mwaka wa bajeti, yeye hajui hata bajeti ya sekta zake!! Mwaka mzima alikuwa anafanya nini? Hakuwa akisoma kitabu chake cha bajeti??

Tutaendelea pale tunapotenda tofauti na mazoea.
 
We paskali tena ukiwa verified membe of jamii forum haogopi kufuatwa.

Haya yote wanayajua, wanajua protokali jinsi gani mambo yanatakiwa yafanyike, lakini kama mkuu wa kaya hataki kuwasikiliza je wamsaidie vipi, au unataka wamshikie mtutu halafu waishie kupotezwa, tuache kama yalivyo, then majibu yatapatikana, but this is the REAL personality of our Presidaa
Acha mazoea Ndugu. Protokali haijasaidia taifa hili hata siku moja. Na tukidekeza mtindo huo ndo tunaishia kuambiwa kila mradi ni mali ya mtoto wa rais. Kila kona, kila mkoa, kila biashara. That was rubbish!
 
Hivi wewe si juzi juzi tu ulipayuka humu kulaani jarida la The Economist lilipomuita Magufuli "bulldozer"; iweje wewe leo umuite "bully" na "intimidator" na iwe sawa?
Ukweli ukisemwa na wageni ni fedheha ila ukisemwa na wenyeji ni sawa?
Hukumwelewa, rudi ukamsome tena!
 
Wewe ni CCM kweli kweli, kwa taarifa yako siku hizi barabara za vijijini zipo chini ya TARURA, ng'ombe wa CCM asiyekuwa na mkia.
Sasa mkuu hapo umejibu kitu gani kama ulijibu ukiwa na nia ya kupata response?

Wewe mkuu wa Babati, umeamuwa kunifananisha na ng’ombe kwasababu wewe ni mfugaji?

Sitaki kwenda unakotaka, ukinilazimisha usinilaumu. Maana tusi baya kwangu kuliko hata hilo la kuniita ng’ombe, ni kuniita mimi ni ccm.

Chunga ulimi mkuu, endelea kutupa mawe ukiwa kwenye gorofa la vioo.

Eti barabara ziko chini ya TARURA, na pesa zilizopelekwa zilikuwa chini ya nani wewe kanume kenge?
 
Back
Top Bottom