Song of Solomon
JF-Expert Member
- Aug 5, 2021
- 2,750
- 5,641
NILIKUWA nimeishiwa sana, njaa inaniuma kwa bahati nikakutana na mchungaji wangu mtaani.
Nikamueleza tatizo langu na kumuomba japo elfu mbili nikanunue chips mayai.
Kwa masikitiko makubwa mchungaji akanambia hana hata senti au lazima angenisaidia mimi mwanakondoo wake, lakini akaniwekea mikono kichwani na kuniombea Mungu afanye muujiza nipate pesa ya kula.
Alipomaliza kuniombea wakati anaondoka akatoa kitambaa mfukoni ajifute jasho, na pale pale noti ya shilingi alfu kumi ikadondoka kutoka mfukoni mwake.
Mchungaji hakuiona akaendelea na safari.
Swali Je, nimshtue Mchungaji au ndiyo muujiza alioniombea umetukia?
Mawazo yenu waungwana.