Je, huku ndiko kuokoka?

Je, huku ndiko kuokoka?

Ukiona mtu anafanya maombi binadamu mwenzake akutwe na mabaya huyo ni mpinga Kristo! Watu wanapakiwa vitu vichwani hadi wanakuwa kama vichaa! Unakuta mtu anakemea mijusi! Hivi kama ukiona mjusi kemea! paka anapita kemea! Hivi una Mungu gani? Hapo si unaishi kwa nguvu zako za kukemea kila kitu unachohisi tu!

Watu wanalazimisha sana kumsikia Roho Mtakatifu hadi shetani anawaletea sauti yake wanaishia kuamini tu na kutabiri, kuhisi kila kitu ni kibaya.

Kama wewe ni Mkatoliki ishi simple prayer life, maisha ya kisakramenti na utii kwa Kanisa! Neema ya Mungu haitakupungukia na ulinzi wa Mungu utakuwa nao bila kuhitaji kushindana hadi na mijusi!

Nafahamu yapo mamlaka tuliyopewa kama Wakristo lakini si kutumia hovyo kama vichaa! Damu ya Yesu inamwagwa hovyo hovyo tu hata mbu akikung'ata!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi hapa ndio nawadharau wolokole na watu wa namna hiyo ,Unasali sana una MUNGU ndani yako ukiomba kidogo unanena kwa lugha pia unanena na MUNGU katika maono lakini unalogwa,narudia tena unalogwa

Ni MUNGU gani huyo hata wasio amini hawawezi kuvutwa hizo ni sarakasi Kama za kwenye ushirikina kwamba kunakuzidiana kwenye matunguri

Siku nikipata nafasi ntakileta kisa changu juu ya mmoja tuliyekutana shuleni

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtu aliyeokolewa harogeki.
 
yaani muda mwingine unatamani hata uzabe kibao...

Sent using Jamii Forums mobile app
Walokole wengi siku hizi hutumia trick ya kumpumbaza mtu kwanza na kumfanya ajione hayuko salama au kufeli/matatizo yake kumeletwa na nguvu za giza. Akishakuwa kwenye hiyo hali ya wasiwasi ndiyo inakuwa rahisi kum-manipulate kadiri wanavyotaka. Jambo amablo mtu wa kawaida analiona liko wazi mtu akishakuwa kwenye hali hiyo analiona kitofauti kabisa.
 
Mimi hapa ndio nawadharau wolokole na watu wa namna hiyo ,Unasali sana una MUNGU ndani yako ukiomba kidogo unanena kwa lugha pia unanena na MUNGU katika maono lakini unalogwa,narudia tena unalogwa

Ni MUNGU gani huyo hata wasio amini hawawezi kuvutwa hizo ni sarakasi Kama za kwenye ushirikina kwamba kunakuzidiana kwenye matunguri

Siku nikipata nafasi ntakileta kisa changu juu ya mmoja tuliyekutana shuleni

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani we acha tu ndiyo maana Mimi nacheka tu...
Sawa ukipata muda uletee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu Nafaka,



Kufunga, kuomba na kudai watu wamekuroga sio Kuokoka. Kabla sijaenda mbali naomba ninukuu maneno ya Kristo mwenyewe:

"Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. - Mathayo 7:21-23

Hapo Yesu Kristo mwenyewe yuko wazi kuwa si kufunga tu, hata kutenda miujiza siyo kigezo kuwa mtu ameokoka. Labda tujiulize pamoja, tunaposema mtu ameokoka, maana yake nini?

Kuokoka kwa lugha ya kawaida ni kuepuka ajali au kitu kibaya kilichokuwa kikupate. Naomba kwa ufupi nikueleze tu juu ya kuokoka kwa muktadha wa Kikristo.
1. Mungu aliumba dunia kamilifu: Hakukuwa na maumivu, kuugua, uchawi wala kifo, mafuriko, matetemeko na kila mabaya tuyaonayo leo. Ukisoma kitabu cha Mwanzo sura ya 1 na 2 utaona Mungu anaumba dunia kamilifu kwa ajili ya Adam na mkewe kuishi.

2. Mwanadamu aliasi na kuleta uharibifu: Ukisoma sura ya 3 ya kitabu cha Mwanzo, Adamu hayupo mkewe katoka kupuyanga anakutana na shetani katika umbo la nyoka. Shetani anamjaribu na kumdanganya Hawa. Kwa tamaa yake anakula lile tunda ambalo Mungu aliwazuia wasile. Anamshawishi na mumewe wanakula. Uasi (dhambi) unaingia katika ulimwengu mkamilifu. Kwa sababu ya dhambi ulimwengu unaingia katika kufa. Magonjwa, miiba, kula kwa jasho, kuzaa kwa uchungu, uharibifu wa mazingira na mengine mabaya yanaingia ulimwenguni na kwa sababu hiyo maisha yanakuwa mabaya. Kifo kinaingia katika ulimwengu.

Kabla ya uasi huu, shetani alikuwa amekwisha kuasi na kusomewa hukumu yake. Muda wa kuitekeleza unakuwa bado na ndio maana alipata nafasi ya kumdanganya Hawa. Mwanadamu anaungana na shetani kwenye adhabu yake maana kosa lao lilikuwa ni moja, nalo ni uasi. Mwanadamu wa kwanza na uzao wake wakawa katika hatari ya wote kuishia Jehanamu ya mateso mengi sana. Hatari hii ni kw sababu mshahara wa uasi (dhambi) ni mauti. Rejea Warumi 6:23

3. Mungu anaahidi Ukombozi wa Wanadamu
Jehanamu haikutengenezwa kwa sababu ya wanadamu. Yesu anasema "Kisha atawaambia na wale walioko katika mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake" Mathayo 25:41. Wanadamu wanaenda Jehanamu kama kenge kwenye msafara wa mamba. Tumejiunganisha kwa kiherehere chetu tu.

Kwa sababu Mungu hakumuumba mwanadamu ili ateseke na kwa sababu alimpenda sana mwanadamu, alipanga kumuokoa toka kwenye janga la Jehanamu alilojitakia. Lakini tatizo ni kuwa Mungu ni Mtakatifu sana na wa haki. Kwa sababu hiyo, lazima ahakikishe kila dhambi inapata hukumu stahili. Dhambi dhidi ya Mungu asiye na mwanzo wala mwisho inadai hukumu isiyo na mwisho, ya milele. Kwa hiyo Mungu asingeweza kufumbia macho dhambi za mwanadamu awaye yeyote.

Lakini Upendo wake ulidai lazima afanye kitu kutusaidia wanadamu ambao tulishakuwa hopeless. Ndipo sasa akaamua aje mwenyewe katika mwili wa Mwanadamu, ili aishi maisha yasiyo na hatia, na kwa sababu hiyo hakupaswa kufa. Maana kifo ni matokeo ya dhambi. Akaishi bila kutenda dhambi.

Akajitoa afe, ili abebe hukumu ya dhambi za wanadamu. Dhambi dhidi ya Mungu asiye na mwisho zinadai hukumu ya Milele. Lakini Mungu wa milele, katika utu wa Kristo Yesu anaweza kulipia deni la milele ndani ya muda ule mfupi. Kwa hiyo Mungu muumbaji akaruhusu adhabu ya dhambi imuangukie, ili aweze kutusamehe dhambi bila kupungua kuwa Mwenye haki.

Ni kama ambavyo mahakama imewahukumu wale viongozi wa Chadema mil 350. Fikiria kwamba wasingekuwa na uwezo wa kulipa, wangeenda gerezani. Sasa fikiria baada ya hukumu, jaji angeamua kuwalipia mil 350 zote! Maana yake wangekuwa huru japo wamehukumiwa kuwa wamevunja sheria.

Ndio maana katika kitabu cha 1 Petro 3:18 Biblia inasema
"Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; akauawa kimwili, lakini akahuishwa kiroho"

Kwa hiyo Yesu alikuja ili kutuokoa na hatari ya Jehanamu. Sasa nitamalizia na mambo mawili ya msingi: Ni vipi mtu anaokolewa/anaokoka na mwisho ushuhuda wa mtu aliyeokolewa.

4. Namna Gani Tunaokolewa?
Waefeso 2:8-9 inasema "Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu"

Kwa maana rahisi, wokovu ni zawadi au kipawa. Zawadi hauifanyii kazi au itakuwa ni ijara na si zawadi. Mungu ametulipia dhambi zote bure. Lakini Mungu hamlazimishi mtu kuipokea zawadi kama hataki. Kama ilivyo kwa zawadi zote, lazima inapotolewa ipokelewe. Kama watu wanakufa kwa njaa, halafu akajitokeza mtu na kutoa zawadi bure ya chakula lakini watu wakaikataa basi watakufa. si kwa sababu hakukuwa na chakula, bali kwa sababu wahusika wameikataa. Vivyo hivyo na zawadi ya Mungu ya uzima wa milele.

Kuokoka ni rahisi sana na Biblia iko wazi kuwa:
"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. 19 Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu" Yohana 3:16 - 20

"Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika" Warumi 10:9-11

"Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto" Ufunuo 20:15

Kwa hiyo wokovu unakuja kwa kumwamini Yesu Kristo kuwa ni Bwana Mungu, aliyekuja katika mwili ili afe kwa ajili ya dhambi zako. Unapaswa kutubu (Kugeuka na kuziacha njia zako za awali) na kumlilia Kristo kwa ajili ya msamaha wa dhambi. Baada ya hapo Bwana atakusamehe na kukupa moyo mpya wenye nia mpya, ambayo ni kuyafanya mapenzi ya Mungu.

5. Utamtambua vipi mtu aliyeokolewa?
2 Wakorintho 5:15-17 inatufundisha kuwa "tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao. Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena. Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama! Yamekuwa mapya"

"Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wakiwa wamevaa mavazi ya kondoo, lakini kwa ndani ni mbwamwitu wakali. Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua" Mathayo 7:15-20

Kwa hiyo ishara ya mtu aliyeokoka kwanza ni kubadilika. Anakuwa mtu tofauti na uliyemjua. Anakuwa obsessed na yule aliyemuokoa na anamtumikia kwa bidii. Kumbuka aliyemuokoa ni Yesu na sio nabii so and so au mchungaji nanilihii au paroko whoever. Mambo mabaya anayaacha, na anakuwa anatamani kufanya yale yanayompendeza Mungu. Marafiki wabaya, lazima ataachana nao. Note hapa sio kujitenga na watu. Kama alikuwa mwizi kwa mfano, kampani yake ya wezi atajitenga nayo kwa sababu atakuwa ha fit tena. Lakini hatawachukia na kuwaona mashetani. Hii ni kwa sababu anajua alikuwa mwovu kama wao na ni Neema ya Mungu tu imemuokoa. Atawapenda na kuwaombea na kwenye mazingira yanayofaa atataka akae nao awaeleze habari za Yesu anayeweza kuwaokoa toka kwenye utumwa wa dhambi.

Atajitahidi kukaa karibu na ndugu na kuwashirikisha upendo wa Mungu na sio kujitenga. Ataungana na wenzake katika ibada na mafundisho. Lakini atarudi kwao na kwa walio wake (ndugu jamaa na marafiki) apate kuwahubiria habari njema. Maana Yesu aliposema enendeni ulimwenguni mkaihubiri injili hakumaanisha kwa waliokwisha kuokoka, bala ambao bado wanahitaji nuru ya wokovu.

Kuwapenda na kuwahubiria watu ndio msingi hasa wa mtu aliyeokoka. Nimejaribu kujibu kwa kifupi sana. Kama utapenda nipe anuani yako au namna naweza kukutumia kijitabu kidogo cha kukusaidia kuelewa zaidi, bure. Hii ni ofa kwa yeyote anayependa. Nitumie details inbox nitakutumia kaba mwezi huu haujaisha, Mungu akitupa uhai!

Mungu akubariki!

Nitumie kwa address ;
Francis Mwangomba Athumani
P.o Box 13327
Dar es Salaam

NB: Natanguliza shukrani na Mungu akubariki zaidi kwa kujitoa kwako kufanya kazi yake ya kusambaza neno lake.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nitumie kwa address ;
Francis Mwangomba Athumani
P.o Box 13327
Dar es Salaam

NB: Natanguliza shukrani na Mungu akubariki zaidi kwa kujitoa kwako kufanya kazi yake ya kusambaza neno lake.


Sent from my iPhone using JamiiForums
Noted. Nitatuma mwisho wa mwezi huu.
 
Walokole wengi siku hizi hutumia trick ya kumpumbaza mtu kwanza na kumfanya ajione hayuko salama au kufeli/matatizo yake kumeletwa na nguvu za giza. Akishakuwa kwenye hiyo hali ya wasiwasi ndiyo inakuwa rahisi kum-manipulate kadiri wanavyotaka. Jambo amablo mtu wa kawaida analiona liko wazi mtu akishakuwa kwenye hali hiyo analiona kitofauti kabisa.

"Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia? Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye. Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi" Mathayo 24:3-4
 
Pole sana ndugu yangu kumbe tupo wengi? Kuna ndugu yetu huwezi amini ni msomi ana masers ya IT ya mwaka 2008 hakutaka kufanya kazi alikuwa akishinda kwa mama Mchungaji wakiomba kwa mikesha tu alikonda haswa kama mgonjwa wa tb na alikuwa na nyumba anaishi peke yake kumbe alishajiandaa kutoa nyumba sadaka kwa mama Mchungaji. Kibaya zaidi akiumwa hawamtibu hadi ndugu tukaamua kufunga safari kwenda mwanza kumtoa huko kumleta Nyumbani kwa nguvu kwani alikuwa hataki kusikia habari za Nyumbani hatawazazi wake na ndugu zake wote aliwaita mapepo MTU akifa anadai ni adui yake kafa. Ndugu wakimuita au msiba ikitokea haendi ata kama ni kwao anadai mungu hajampa kibali baada ya muda tukampatia kazi simple ili afunguke akili basi akawa hatumi matumizi hata mia anapeleka sadaka zote kwa mama wakiroho . baada ya ndugu kupambana tena kwa kichapo huku wengine wakitembea kumuombea Mungu akasikia kilio chetu . hivi sasa amerudi kanisani kwake na amekusanya pesa zake amejenga na pia anatuma matumizi Nyumbani na anawatembelea ndugu zake wote kwa kweli Mungu ni muweza. Hawa wamama wa kiroho wengi ni wachawi wanawateka wasomi na kula pesa na Mali zao wanakuharibu akili unawapa hadi nyumba yako. Ndio hawa wanajiita sasa manabii kumbe matapeli. Ndugu yangu naomba pambaneni mkomboeni ndugu yenu msichoke simameni kidete hata bakora mtandikeni IPO siku mapepo yatakimbia nakuhakikishia utashinda manake ndicho kitu tulichokifanya tulitaka hadi kuchoma nyumba ya huyo Mchungaji haki vile alisalimu amri alikoma harudii. Nakutakia kila LA kheri kapambaneni baba hao manabii wengi wachawii
Kuna ndugu yangu flani huu ni mwaka wa tatu anadai ameokoka, anasali sana, anafunga sana. Lakini tatizo langu kwake ni kwamba anajitenga na watu kasoro familia na marafiki wa karibu wa huyo anayedai ni mama wake wa kiroho. Ila waliobaki anasema ni wachawi. Story zake kila siku anasema wamempiga flani katika maombi, yani story zake ni za kuwapiga watu katika maombi tu.

Mara fulani kafa ile ajali ilikuwa imetegeshewa sisi ili Mungu katuokoa ikampata fulani. Kuna kipindi alipkuwa anaiona anasema oooh mara sijui ndugu yetu gani alikuwa kanifuata ananiroga basi anaanza kuniombea nanivuta nywele na masikio.

Nikaona isiwe tabu nikawa simtembelei sana. Yani kila failure ya maisha yake anasema karogwa japo mambo mengi kafail kwa kutofuata ushauri na kufanya kama inavyotakiwa.

Sasa jana tumekorofishana baada ya kuniambia kuwa sijui mwanangu karogwa, anahitaji kuombewa nitoe sadaka awekewe wakifu eti anadai wakati wanasali na mama yake wa kiroho wameambiwa hivyo na Mungu.

Ikabidi nijaribu kumwelewesha kwamba, mimi mambo yake mengi siyaamini. Nikamwambia kajitenga na kila rafiki yake kwasababu ya kuamini kila mtu mchawi, hadi mijusi anaiua anasema inatumwa na wachawi wanaitumia kupeleleza.

nikajaribu kureason naye nikamwambia mimi naona failure ya maisha yake nyingi zimetokana na yeye mwenyewe ajifunze kutokana na makosa kuliko kutafuta scapegoat.

Kuna kipindi kila mara alikuwa anaanguka akiwa anaomba eti roho mtakatifu amempanda anasema kuongea na kutoa utabiri ambao kwa maono yangu haukuwahi kutokea. Nikamwambia kipindi hicho nilianza kuwa na mashaka kuwa huenda kapata tatizo la kisaikolojia.

Nilivyo mwambia hivyo akasema Mungu anisamehe akanikatia simu. Nimebaki ninasikitika muda mwingine ninawaza au mimi ndiye nimepotoka nina imani haba. Maana mimi naona anapotea anatumia muda mwingi akiomba saana pasipo kujishughulisha wala kuwaza atatokaje.
 
Umemsaidiaje maana yani sijui hata nimsaidieje yani... huyo anayemwita mamake wa kiroho ana mtoto wa kike ni hustler sana yani mtafutaji hakai kusali tu akisubiri Mungu amletee tu bila kujishughulisha. Lakini ndugu yangu yeye muda wowote anaitwa na huyo mama wa kiroho yani muda wowote anampelekesha
Mmh,Huyo mama kuna namna! Chunguza taratibu,huku ukinuombea Hugo ndugu yako,kakamatwa nafsi na ufahamu!! Hakuna ulokole wa hivyo!mi nimeokoka lkn hiyo nakataa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shetani muongo sana!
Muombeeni ufahamu wake,halafu iteni nafsi yake popote ilipowekwa,mtaona! Km inekamatwa mtajua
Hatujamsaidia chochote maana Kama ni kumshauri mnaweza mkabishana siku nzima na kuishia kununiana,kwahiyo tunamuachia Mungu amfungue akili...Hayo yanakuwaga ni mapepo huenda ndugu yako ana mapepo maana siye huyu tunaonaga Kama hayupo sawa kabisaa,ni mwajiriwa ila Kuna kipindi alitaka aache kazi akidai anarogwa huko kazini..

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmh,Huyo mama kuna namna! Chunguza taratibu,huku ukinuombea Hugo ndugu yako,kakamatwa nafsi na ufahamu!! Hakuna ulokole wa hivyo!mi nimeokoka lkn hiyo nakataa!

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo mama hana kanisa wala nini alikuwa kawateka wote watatu yani ndugu zangu wote watatu walikuwa wakiishi pamoja mmoja amechomoka kabisa mwingine naye kachomoka sasa kabaki huyu yani huyu kawa kama ndo kamkamata sana
 
Wengi tu mkuu.
naamini kila mtu keshakutana nao wateule wa bwana
Sawa basi ila ujue si kila anayedai ameokoka ni mkweli. Wengi hudhani akisali kanisa fula au akizaliwa damilia wazazi wameokoka na yeye anakuwa automagically. Wengine ni matapeli na wengine ni watapeliwa.

Una hakika walikuwa wameokoka? Unayoyasema hayafanani na wokovu...
 
2Corinth..5:17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
Therefore if any man be in Christ, he is a new creature: old things are passed away; behold, all things are become new.

Huo ndiyo wokovu wa kweli, mwingine ni bandia.
 
Nyie mnaokejeli walokole Mungu atawakana kama mnavyomkana hapa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom