Je, huku ndiko kuokoka?

Je, huku ndiko kuokoka?

endelea na mambo yako acha kumfuatilia mwamume mwenzako kihivyo
wewe unamuona hayuko sawa ,na yeye itakuwa hivyo hivyo hamtafikia mwafaka
Kwanza siyo mwanaume na pili nimekwakmbia ni ndugu yangu siyo rafiki wala mtu baki ndo maana niko worried
 
Mpende Bwana Mungu wako kwa Nguvu zako zote, Moyo wako wote na AKILI ZAKO ZOTE.
Tatizo lipo hapo nilipopigia mstari. Wengi wanaodai kuokoka, HAWATUMII akili.

Ndiyo maana unaweza kuta mtu kabla ya kuokoka mambo yake yalikuwa mazuri na baada ya kuokoka tu mambo humuendea sivyo. Ni kwa sababu baada ya kuokoka kwake, aliamua kuenda na vyote isipokuwa akili.

Hili ni somo ambalo wapendwa wengi wanatakiwa kulielewa.
 
Kuna ndugu yangu flani huu ni mwaka wa tatu anadai ameokoka, anasali sana, anafunga sana. Lakini tatizo langu kwake ni kwamba anajitenga na watu kasoro familia na marafiki wa karibu wa huyo anayedai ni mama wake wa kiroho. Ila waliobaki anasema ni wachawi. Story zake kila siku anasema wamempiga flani katika maombi, yani story zake ni za kuwapiga watu katika maombi tu.

Mara fulani kafa ile ajali ilikuwa imetegeshewa sisi ili Mungu katuokoa ikampata fulani. Kuna kipindi alipkuwa anaiona anasema oooh mara sijui ndugu yetu gani alikuwa kanifuata ananiroga basi anaanza kuniombea nanivuta nywele na masikio.

Nikaona isiwe tabu nikawa simtembelei sana. Yani kila failure ya maisha yake anasema karogwa japo mambo mengi kafail kwa kutofuata ushauri na kufanya kama inavyotakiwa.

Sasa jana tumekorofishana baada ya kuniambia kuwa sijui mwanangu karogwa, anahitaji kuombewa nitoe sadaka awekewe wakifu eti anadai wakati wanasali na mama yake wa kiroho wameambiwa hivyo na Mungu.

Ikabidi nijaribu kumwelewesha kwamba, mimi mambo yake mengi siyaamini. Nikamwambia kajitenga na kila rafiki yake kwasababu ya kuamini kila mtu mchawi, hadi mijusi anaiua anasema inatumwa na wachawi wanaitumia kupeleleza.

nikajaribu kureason naye nikamwambia mimi naona failure ya maisha yake nyingi zimetokana na yeye mwenyewe ajifunze kutokana na makosa kuliko kutafuta scapegoat.

Kuna kipindi kila mara alikuwa anaanguka akiwa anaomba eti roho mtakatifu amempanda anasema kuongea na kutoa utabiri ambao kwa maono yangu haukuwahi kutokea. Nikamwambia kipindi hicho nilianza kuwa na mashaka kuwa huenda kapata tatizo la kisaikolojia.

Nilivyo mwambia hivyo akasema Mungu anisamehe akanikatia simu. Nimebaki ninasikitika muda mwingine ninawaza au mimi ndiye nimepotoka nina imani haba. Maana mimi naona anapotea anatumia muda mwingi akiomba saana pasipo kujishughulisha wala kuwaza atatokaje.
Yaani hili ni tatizo kwa walokole woteee...
1. Wanaamini kwenye kumwombea mtu yampate mabaya, as long as anaamini ametenda dhambi dhidi yao au kanisa analosali
2. Mchungaji au nabii ni zaidi ya mume/mke... yaani mke/mume anaweza akamtuma kitu, asifanye akafanya alichoambiwa na mchungaji/nabii
3. Manabii/wachungaji huwa wanataka sana kama mmoja wa wanandoa ameokoa, basi na aliyebakia lazima aokoke... yaani watafanya lolote ilimradi hilo litokee
4. Kwao asiye mlokole ni mzinzi, mtenda dhambi, mwizi etc..
5. Yeyote asiye mlokole, akipatwa na lolote baya au janga, WAO HUAMINI NI MAPIGO YA MUNGU KWAKE... YAANI ANAPIGWA ILI AOKOKE, na akiendelea kutoktaka kuokoka basi ataendelea kupigwa.
6. Ambaye hajaokoa, ataambiwa mengi sana juu ya maono. Mara mali zako zitapotea, utaibiwa, utatapanya... YAANI MUNGU ANAKUCHAPA KWA KUKULETEA ALAYE NA SULUHU YAKE WANAAMINI NI KUOKOKA

Kuna wakati mpaka huwa nashangaa... Yaani maisha ya ambaye hajaokoka, ni mema kuliko ya visasi waliyonayo waliita wameokoa... YAANI YEYE AKIAMINI TU UMEMKOSEA, WENGINE HUWAOMBEA WENZA WAO VIFO VIBAYA SANA....

Mungu atatusaidie wallah
 
Biblia inasema katika hosea 4:6

My people are destroyed for lack of knowledge: because thou hast rejected knowledge,

Huyo boya hajielewi biblia yenyewe inawashangaa kinoma.
WANAKUJA MODS KUKUPA MWONGOZO KWA EXPERIENCE YAO KUBWA HUMU NDANI!!!
uyo ni mmoja wa waliokanyaga mafuta, naisi yeye aliyaoga kabisa na mengine akanywa ana upako kilo 2 na robo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo inaonekana kuna matatizo ya kisaikolojia ya paranoid schizophrenic na delusions of grandeur.

Anahitaji msaada wa kisaikolojia

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Inabidi serikali ikae na umoja wa wachawi kuona namna gani technolojia yao inavyoweza kusaidia taifa. Kama hadi mijusi inaweza kutumwa kupeleleza, maana yake tunaweza kupiga hatua sana kiintelijensia endapo tukiwashirikisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo la mijusi hata ndugu yangu analo na yeye anasali kwa gwaji boy. Na ndugu zake wote anawaona kama wachawi pia. Kabla ya kuokoka alikuwa na maendeleo na upendo kwa ndugu sana na marafiki. Hata ikatokea kipindi alitakaga kufukuzwa kazini kwa kupeleka masuala ya imani ya gwaji boy kazi ni. Kila mtumishi mwenzake alikuwa hamuamini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu,
Kuokoka zamani walimaanisha hawana dhambi(hata Yesu akija sasa wanaenda peponi)
Kuokoka zama hizi wanamaanisha Kubadili Dini kuwa mprotestant,
Imani moja maana tofauti
Kuna ndugu yangu flani huu ni mwaka wa tatu anadai ameokoka, anasali sana, anafunga sana. Lakini tatizo langu kwake ni kwamba anajitenga na watu kasoro familia na marafiki wa karibu wa huyo anayedai ni mama wake wa kiroho. Ila waliobaki anasema ni wachawi. Story zake kila siku anasema wamempiga flani katika maombi, yani story zake ni za kuwapiga watu katika maombi tu.

Mara fulani kafa ile ajali ilikuwa imetegeshewa sisi ili Mungu katuokoa ikampata fulani. Kuna kipindi alipkuwa anaiona anasema oooh mara sijui ndugu yetu gani alikuwa kanifuata ananiroga basi anaanza kuniombea nanivuta nywele na masikio.

Nikaona isiwe tabu nikawa simtembelei sana. Yani kila failure ya maisha yake anasema karogwa japo mambo mengi kafail kwa kutofuata ushauri na kufanya kama inavyotakiwa.

Sasa jana tumekorofishana baada ya kuniambia kuwa sijui mwanangu karogwa, anahitaji kuombewa nitoe sadaka awekewe wakifu eti anadai wakati wanasali na mama yake wa kiroho wameambiwa hivyo na Mungu.

Ikabidi nijaribu kumwelewesha kwamba, mimi mambo yake mengi siyaamini. Nikamwambia kajitenga na kila rafiki yake kwasababu ya kuamini kila mtu mchawi, hadi mijusi anaiua anasema inatumwa na wachawi wanaitumia kupeleleza.

nikajaribu kureason naye nikamwambia mimi naona failure ya maisha yake nyingi zimetokana na yeye mwenyewe ajifunze kutokana na makosa kuliko kutafuta scapegoat.

Kuna kipindi kila mara alikuwa anaanguka akiwa anaomba eti roho mtakatifu amempanda anasema kuongea na kutoa utabiri ambao kwa maono yangu haukuwahi kutokea. Nikamwambia kipindi hicho nilianza kuwa na mashaka kuwa huenda kapata tatizo la kisaikolojia.

Nilivyo mwambia hivyo akasema Mungu anisamehe akanikatia simu. Nimebaki ninasikitika muda mwingine ninawaza au mimi ndiye nimepotoka nina imani haba. Maana mimi naona anapotea anatumia muda mwingi akiomba saana pasipo kujishughulisha wala kuwaza atatokaje.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna watu wanajiona wako sahihi/wana haki kama walokole.
ukienda kinyume na wao "Una pepo"
 
Walokole wengi wako hivyo ni aina fulani ya ugonjwa wa akili na ushirikina
 
Hatujamsaidia chochote maana Kama ni kumshauri mnaweza mkabishana siku nzima na kuishia kununiana,kwahiyo tunamuachia Mungu amfungue akili...Hayo yanakuwaga ni mapepo huenda ndugu yako ana mapepo maana siye huyu tunaonaga Kama hayupo sawa kabisaa,ni mwajiriwa ila Kuna kipindi alitaka aache kazi akidai anarogwa huko kazini..

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi hapa ndio nawadharau wolokole na watu wa namna hiyo ,Unasali sana una MUNGU ndani yako ukiomba kidogo unanena kwa lugha pia unanena na MUNGU katika maono lakini unalogwa,narudia tena unalogwa

Ni MUNGU gani huyo hata wasio amini hawawezi kuvutwa hizo ni sarakasi Kama za kwenye ushirikina kwamba kunakuzidiana kwenye matunguri

Siku nikipata nafasi ntakileta kisa changu juu ya mmoja tuliyekutana shuleni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: ABJ
..Aisee mleta uzi, nduguyo kafanana kabisa na jirani yangu...
 
Ndugu Nafaka,

Kuna ndugu yangu flani huu ni mwaka wa tatu anadai ameokoka, anasali sana, anafunga sana. Lakini tatizo langu kwake ni kwamba anajitenga na watu kasoro familia na marafiki wa karibu wa huyo anayedai ni mama wake wa kiroho. Ila waliobaki anasema ni wachawi. Story zake kila siku anasema wamempiga flani katika maombi, yani story zake ni za kuwapiga watu katika maombi tu.

Kufunga, kuomba na kudai watu wamekuroga sio Kuokoka. Kabla sijaenda mbali naomba ninukuu maneno ya Kristo mwenyewe:

"Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. - Mathayo 7:21-23

Hapo Yesu Kristo mwenyewe yuko wazi kuwa si kufunga tu, hata kutenda miujiza siyo kigezo kuwa mtu ameokoka. Labda tujiulize pamoja, tunaposema mtu ameokoka, maana yake nini?

Kuokoka kwa lugha ya kawaida ni kuepuka ajali au kitu kibaya kilichokuwa kikupate. Naomba kwa ufupi nikueleze tu juu ya kuokoka kwa muktadha wa Kikristo.
1. Mungu aliumba dunia kamilifu: Hakukuwa na maumivu, kuugua, uchawi wala kifo, mafuriko, matetemeko na kila mabaya tuyaonayo leo. Ukisoma kitabu cha Mwanzo sura ya 1 na 2 utaona Mungu anaumba dunia kamilifu kwa ajili ya Adam na mkewe kuishi.

2. Mwanadamu aliasi na kuleta uharibifu: Ukisoma sura ya 3 ya kitabu cha Mwanzo, Adamu hayupo mkewe katoka kupuyanga anakutana na shetani katika umbo la nyoka. Shetani anamjaribu na kumdanganya Hawa. Kwa tamaa yake anakula lile tunda ambalo Mungu aliwazuia wasile. Anamshawishi na mumewe wanakula. Uasi (dhambi) unaingia katika ulimwengu mkamilifu. Kwa sababu ya dhambi ulimwengu unaingia katika kufa. Magonjwa, miiba, kula kwa jasho, kuzaa kwa uchungu, uharibifu wa mazingira na mengine mabaya yanaingia ulimwenguni na kwa sababu hiyo maisha yanakuwa mabaya. Kifo kinaingia katika ulimwengu.

Kabla ya uasi huu, shetani alikuwa amekwisha kuasi na kusomewa hukumu yake. Muda wa kuitekeleza unakuwa bado na ndio maana alipata nafasi ya kumdanganya Hawa. Mwanadamu anaungana na shetani kwenye adhabu yake maana kosa lao lilikuwa ni moja, nalo ni uasi. Mwanadamu wa kwanza na uzao wake wakawa katika hatari ya wote kuishia Jehanamu ya mateso mengi sana. Hatari hii ni kw sababu mshahara wa uasi (dhambi) ni mauti. Rejea Warumi 6:23

3. Mungu anaahidi Ukombozi wa Wanadamu
Jehanamu haikutengenezwa kwa sababu ya wanadamu. Yesu anasema "Kisha atawaambia na wale walioko katika mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake" Mathayo 25:41. Wanadamu wanaenda Jehanamu kama kenge kwenye msafara wa mamba. Tumejiunganisha kwa kiherehere chetu tu.

Kwa sababu Mungu hakumuumba mwanadamu ili ateseke na kwa sababu alimpenda sana mwanadamu, alipanga kumuokoa toka kwenye janga la Jehanamu alilojitakia. Lakini tatizo ni kuwa Mungu ni Mtakatifu sana na wa haki. Kwa sababu hiyo, lazima ahakikishe kila dhambi inapata hukumu stahili. Dhambi dhidi ya Mungu asiye na mwanzo wala mwisho inadai hukumu isiyo na mwisho, ya milele. Kwa hiyo Mungu asingeweza kufumbia macho dhambi za mwanadamu awaye yeyote.

Lakini Upendo wake ulidai lazima afanye kitu kutusaidia wanadamu ambao tulishakuwa hopeless. Ndipo sasa akaamua aje mwenyewe katika mwili wa Mwanadamu, ili aishi maisha yasiyo na hatia, na kwa sababu hiyo hakupaswa kufa. Maana kifo ni matokeo ya dhambi. Akaishi bila kutenda dhambi.

Akajitoa afe, ili abebe hukumu ya dhambi za wanadamu. Dhambi dhidi ya Mungu asiye na mwisho zinadai hukumu ya Milele. Lakini Mungu wa milele, katika utu wa Kristo Yesu anaweza kulipia deni la milele ndani ya muda ule mfupi. Kwa hiyo Mungu muumbaji akaruhusu adhabu ya dhambi imuangukie, ili aweze kutusamehe dhambi bila kupungua kuwa Mwenye haki.

Ni kama ambavyo mahakama imewahukumu wale viongozi wa Chadema mil 350. Fikiria kwamba wasingekuwa na uwezo wa kulipa, wangeenda gerezani. Sasa fikiria baada ya hukumu, jaji angeamua kuwalipia mil 350 zote! Maana yake wangekuwa huru japo wamehukumiwa kuwa wamevunja sheria.

Ndio maana katika kitabu cha 1 Petro 3:18 Biblia inasema
"Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; akauawa kimwili, lakini akahuishwa kiroho"

Kwa hiyo Yesu alikuja ili kutuokoa na hatari ya Jehanamu. Sasa nitamalizia na mambo mawili ya msingi: Ni vipi mtu anaokolewa/anaokoka na mwisho ushuhuda wa mtu aliyeokolewa.

4. Namna Gani Tunaokolewa?
Waefeso 2:8-9 inasema "Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu"

Kwa maana rahisi, wokovu ni zawadi au kipawa. Zawadi hauifanyii kazi au itakuwa ni ijara na si zawadi. Mungu ametulipia dhambi zote bure. Lakini Mungu hamlazimishi mtu kuipokea zawadi kama hataki. Kama ilivyo kwa zawadi zote, lazima inapotolewa ipokelewe. Kama watu wanakufa kwa njaa, halafu akajitokeza mtu na kutoa zawadi bure ya chakula lakini watu wakaikataa basi watakufa. si kwa sababu hakukuwa na chakula, bali kwa sababu wahusika wameikataa. Vivyo hivyo na zawadi ya Mungu ya uzima wa milele.

Kuokoka ni rahisi sana na Biblia iko wazi kuwa:
"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. 19 Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu" Yohana 3:16 - 20

"Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika" Warumi 10:9-11

"Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto" Ufunuo 20:15

Kwa hiyo wokovu unakuja kwa kumwamini Yesu Kristo kuwa ni Bwana Mungu, aliyekuja katika mwili ili afe kwa ajili ya dhambi zako. Unapaswa kutubu (Kugeuka na kuziacha njia zako za awali) na kumlilia Kristo kwa ajili ya msamaha wa dhambi. Baada ya hapo Bwana atakusamehe na kukupa moyo mpya wenye nia mpya, ambayo ni kuyafanya mapenzi ya Mungu.

5. Utamtambua vipi mtu aliyeokolewa?
2 Wakorintho 5:15-17 inatufundisha kuwa "tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao. Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena. Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama! Yamekuwa mapya"

"Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wakiwa wamevaa mavazi ya kondoo, lakini kwa ndani ni mbwamwitu wakali. Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua" Mathayo 7:15-20

Kwa hiyo ishara ya mtu aliyeokoka kwanza ni kubadilika. Anakuwa mtu tofauti na uliyemjua. Anakuwa obsessed na yule aliyemuokoa na anamtumikia kwa bidii. Kumbuka aliyemuokoa ni Yesu na sio nabii so and so au mchungaji nanilihii au paroko whoever. Mambo mabaya anayaacha, na anakuwa anatamani kufanya yale yanayompendeza Mungu. Marafiki wabaya, lazima ataachana nao. Note hapa sio kujitenga na watu. Kama alikuwa mwizi kwa mfano, kampani yake ya wezi atajitenga nayo kwa sababu atakuwa ha fit tena. Lakini hatawachukia na kuwaona mashetani. Hii ni kwa sababu anajua alikuwa mwovu kama wao na ni Neema ya Mungu tu imemuokoa. Atawapenda na kuwaombea na kwenye mazingira yanayofaa atataka akae nao awaeleze habari za Yesu anayeweza kuwaokoa toka kwenye utumwa wa dhambi.

Atajitahidi kukaa karibu na ndugu na kuwashirikisha upendo wa Mungu na sio kujitenga. Ataungana na wenzake katika ibada na mafundisho. Lakini atarudi kwao na kwa walio wake (ndugu jamaa na marafiki) apate kuwahubiria habari njema. Maana Yesu aliposema enendeni ulimwenguni mkaihubiri injili hakumaanisha kwa waliokwisha kuokoka, bala ambao bado wanahitaji nuru ya wokovu.

Kuwapenda na kuwahubiria watu ndio msingi hasa wa mtu aliyeokoka. Nimejaribu kujibu kwa kifupi sana. Kama utapenda nipe anuani yako au namna naweza kukutumia kijitabu kidogo cha kukusaidia kuelewa zaidi, bure. Hii ni ofa kwa yeyote anayependa. Nitumie details inbox nitakutumia kaba mwezi huu haujaisha, Mungu akitupa uhai!

Mungu akubariki!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom