Je historia hii inatufundisha chochote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je historia hii inatufundisha chochote

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Jun 19, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Jun 19, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  HISTORIA ILIYOTUPWA

  Nimerudi tena katika mambo ya historia leo naangalia baadhi ya vitu katika historia vilivyotupwa au kupotoshwa kwa makusudi kabisa kutokana na watu kuwa na maslahi yao au mengine binafsi katika historia hizi .

  Nafikiri umeshawahi kusikia kitu kinaitwa Trojan ( Trojan Horse ) katika ulimwengu wa ICT hili ni jina la Virus aliyeshambulia sana na kutesa enzi zake hata sasa hivi bado anatesa katika baadhi ya sehemu ingawa imeshadhibitiwa

  Kwa ufupi Trojan ni mji wa zamani kidogo katika ugiriki uliyokuwa maarufu sana kwa biashara na ustaarabu wa ugiriki wakati Fulani waliwahi kupigana vita na mji mwingine uliokuwa unaitwa Troy kwa muda wa miaka 7 na zaidi , watu wengi toka eneo la Trojan walikuwa wakatili na wauaji kama Kirusi chenyewe kinavyoitwa Trojan sasa hivi haieleweki mtu aliyetengeneza kirusi hichi alikusudia nini kihistoria .

  Angalia filamu moja inayoitwa Troy iliigizwa mwaka jana nchini marekani utaelewa zaidi kuhusu kilichotokea katika mji huo wa troy

  Kama wewe ni Mpenda kuchoma CD zako kwa computer lazima utakuwa umewahi kutumia programu moja inayoitwa Nero kwa ajili ya shuguli zako hizo za burn CD , nero alikuwa mtawala wa Roma wa enzi za kali , na ni mmoja wa watawala aliyekuwa na nguvu kuliko wote katika himaya za roma wakati huo

  Nero aliacha historia moja kubwa tu enzi zake , yeye ndio alikuwa kiongozi a kwanza kuhalalisha wasambazaji wa injili wauwawe ndio alimkata shingo mtakatifu Peter na Paul , sio hiyo tu hata mama yake aliwahi kuuwawa na Nero mwenyewe .

  Wengi wetu tunapenda kutumia nero kuburn cd kama nilivyosema hapo mwanzo na wengi wetu tunapenda kuumia P2P programu maarufu kwa ajili ya kuchota nyimbo vitabu na programu zingine katika mitandao ya interne inayoitwa Ares katika ugiriki ya zamani ares alijulikana kama Mungu wa vita .

  Kwa wale waliokuwa na mapenzi ya kujua historia ya Freemasony vizuri kwanza inabidi waanzie historia ya Ugiriki ya zamani , Misri . Israel , Halafu Roma , kisha Uingereza yaani London na Marekani , Angalia kwa makini utakuta katika Movement zote zilizowahi kuhangaisha mataifa hayo zilihusiana na kubomolewa au kuchomwa kitu Fulani katika Himaya hizo

  Ugiriki ya zamani , katika vita kati ya Troy na Trojan , watu wengi sana walichomwa moto na majengo yao kuchomwa moto ili kupoteza mambo Fulani Fulani katika historia zao , kabla ya Hapo kulikuwa na Maktaba ya Alexandria iliyokuwa na vitabu vingi sana hii maktaba ilichomwa yote mabaki yake alitumwa katika bahari moja yakawa na rangi nyekundu ndio maana mpaka leo wanaita Red Sea .

  Ukienda Israel mpaka leo kuna kisa cha kuchomwa moto Jengo moja la ibada ambalo mpaka leo linagembewa kati ya wakristo na waisilamu lilichomwa na kuharibiwa inasemekana wayahudi wanataka kujenga jengo jipya eneo hilo .

  Enzi za roma wakati ukristo unaenea sana kulitokea moto mkubwa ambao ilichoma maeneo mengi sana wakati nero akiwa mtawala , moto huu ulimfanya nero akimbie himaya kwa muda kuogopa na ulichangia sana katika kudidimiza nguvu za Nero katika utawala wake .

  Moto huu ulihamia London mji mkuu wa London enzi hizo , nao uliwahi kuchomwa moto enzi hizo bila sababu zozote za msingi , kisha ukahamia Ikulu ya white house nayo iliwahi kuchomwa moto wakati Fulani .

  Hii yote ni historia je ina chochote cha kutufunza kwa maisha ya sasa na baadaye baada ya kusoma hisoria hizo , Angalia shambulio na septemba 11 yale ni mambo ya moto kila kitu ni moto moto
   
 2. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Siku zote Historia ni mwalimu.
  Yeye anaye dharau historia, hawezi kujenga future nzuri.
   
Loading...