Je hiki ni kipeo cha uwezo wa mawaziri wetu kufikiri?

pingiring'ombe

JF-Expert Member
Apr 3, 2008
386
1
Heshima mbele wakuu. Nimekuwa nikifikiria sana juu ya upeo wa mawaziri wetu ambao wana dhamana ya kuliongoza Taifa letu kwenda kwenye Maisha Bora kwa kila Mtanzania. Hapa ntatoa mifano miwili tu (iliyonigusa na current ones)
1. Nilisikiliza mahojiano kati ya mheshimiwa mkuu sana wa habari na MMKJ kupitia KHL News (nafikiri wengi wetu tulisikia alivyojibu maswali ya MMKJ) Kwa kweli kama upeo wa mheshimiwa huyu ndio huu kazi tunayo.

2. Nimesoma Mtanzania Daima la jana trh 17 nikakuta "maajabu mengine ya waheshimiwa wetu. Safari hii ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Selina Kombani. Kombani kasema migomo ya inayoendelea Tanzania (Walimu, vyuo, mabenki et al) inafadhiliwa na wazungu “Mlishaona wapi Wazungu wakishiriki maandamano, lakini hapa nchini, Wazungu wamekuwa wakishiriki maandamano na hawa ndio wafadhili wa yote haya,” alisema Kombani.

Wakuu, kwa kweli mimi nimekata tamaa KABISA na hawa viongozi wetu. Nyerere alisema moja ya vitu muhimu kwa maendeleo ya nchi ni viongozi bora (Hapa ndipo Tanzania ina tatizo: Nafikiri tuna Bora Viongozi).

Wakuu, need change of wich without? Tanzania will remain the same NO MATTER WHAT...
 
Hilo ni somo la mwisho kwa watu waliotegemea maajabu au miujiza kutoka kwa watu ambao wenyewe ni maajabu! ...Unategemea nini zaidi, "garbage in garbage out"!!!
 
Hilo ni somo la mwisho kwa watu waliotegemea maajabu au miujiza kutoka kwa watu ambao wenyewe ni maajabu! ...Unategemea nini zaidi, "garbage in garbage out"!!!
Sasa twende kwa Ngeleja, waziri kijana ambaye tangu alipoteuliwa amejitahidi sana kuwa makini katika nyendo zake kiasi kwamba wengi waliamini kuwa huenda ni mmoja wa viongozi vijana ambao Rais Jakaya Kikwete hakukosea kuwapa nyadhifa walizonazo.

Kinyume chake, Ngeleja ameamua kwa makusudi tu kujifunua kwa Watanzania kuwa hata yeye hana hizo sifa ambazo baadhi tulikuwa tumeanza kumpa. Na nadhani Rais Kikwete anapaswa kuwa makini zaidi na huyu kwa sababu alichokifanya, mimi ninakiona ni cha hatari na kama hakitakemewa basi kinaweza kuidhalilisha serikali machoni mwa watu kwa kuonekana ni serikali yenye viongozi wanaofurahia vifo.

Pamoja mtizamo huo, kwa mtizamo wangu mwingine, Ngeleja amenifurahisha kwa sababu amenifanya nielewe ni kwa nini baadhi ya majimbo hayapatiwi huduma muhimu kwa wakati licha ya wawakilishi wake kuomba kwa nguvu zote bungeni. Kauli ya Ngeleja kuwa watamuenzi marehemu Richard Nyaulawa kwa kupekeka umeme jimboni kwake imenifanya niamini kuwa kumbe serikali ilikuwa na uwezo wa kupeleka umeme jimboni humo wakati wowote, lakini ilikuwa inasubiri afe ndipo wapeleke kama njia moja wapo ya kumuenzi.

Hili linafurahisha jamani au sijui wenzangu mnaonaje. Yaani jamaa wanasubiri mpaka huyo aliyekuwa akipiga kelele za kuomba huko kwake wapatiwe umeme afe, ndipo inaamua kuupeleka kama njia mojayapo ya kumuenzi.

Ngeleja amenifurahisha kwa sababu amenifanya niamini kuwa serikali ina fedha nyingi mahali ambazo imeziweka tu, na inapoamua kuzitumia inazitoa, inazitumia kadri inavyotaka. Ninaamini hivi kwa sababu nina hakika hata kama Ngeleja angekuwa fisadi, sidhani kama angeweza kutumia fedha yake ya mfukoni kupeleka umeme huko alikosema.

Ninasita kujikita zaidi katika kumjadili Ngeleja na kauli zake kwa sababu nadhani ninaweza kufika mbali ambako hakutamfurahisha. Nadhani inatosha tu nikieleza kuwa kiongozi huyu kijana amejivua nguo, ameonyesha ni jinsi gani asivyoweza kuchagua maneno ya kuzungumza kulingana na eneo alilopo na tukio husika.

Na hata kama alitumwa na mkubwa wake yoyote kueleza hivyo, bado hawezi kujisafisha na doa hili kwa sababu kwa kiongozi kama yeye, anapaswa kupima uzito wa amri anazopewa kuzitekeleza na hata kutoa ushauri kwa bosi wake na ikibidi kukataa kwa ile staili yetu ya kiungwana kutekeleza amri ambazo anadhani hazistahili kufanywa na mtu mwenye hadhi kama ya kwake kwa maslahi ya wale anaowaongoza.

Vyovyote iwavyo, alichokifanya kiongozi huyu kijana ni kitu cha ovyo kinachomuonyesha kuwa mtu mwenye urafiki na kifo. Yaani anapenda kutumia vifo vya wenzake kujinufaisha yeye na wenzake fulani kisiasa. Nafikiri, fikra zangu ni sahihi na hata Ngeleja mwenyewe atakubaliana na mimi.

Mwingine tena huyu hapa Mh Ngeleja na aliyoyasema kwenye msiba wa Mh Nyaulawa

Source: Tanzania daima ya 16 Nov 08; William Ngeleja, rafiki wa kifo by Charles Mulinda
 
Tatizo ni mfumo mzima wa kuwa eti ili mtu awe Waziri lazima awe Mbunge! Wasomi wengi na wenye uwezo wa kuendesha hizo Wizara hawawezi kwenda kupambana kwenye majukwaa ya siasa, kulikojaaa ubabe, wizi wa kura, rushwa, takrima, ushirikina na majungu na kujipendekeza!

Matokeo yake hao watu ambao wanayaweza hayo mambo ndio wanaojitokeza kugombea. Sasa Rais anajikuta analazimika kuteua hao hao! Ni kama kwenye mashindano ya Miss Tanzania, wanaojitokeza hata kama wote ni wabaya, lazima jopo la majaji limpitishe mmoja mwenye afadhali kuliko wengine; kwa kuwa wale wazuri hawakujitokeza kugombea kutokana na sababu zao tofatui tofauti.
 
Well said mkuu, tuko pamoja. Nafikiri pia tatizo lingine lipo kwenye kuchagua ccm members pekee kushika uongozi wa nchi baada ya ushindi wao wa tsunami, EPA?. Mimi huwa najiuliza sana, ina maana kuwa ccm ndo kuwa na "akili"? Naamini kuna watu wenye uwezo mkubwa sana wa kuongoza vizuri ambao hawapo ccm, sijui tutafika lini huko ila ilitakiwa kuchagua viongozi regardless of their chama provided wana uwezo na waadilifu. Ndo maana nikasema we need a change otherwise...
 
Kuna thread kama hii tayari.

Yes mama, you are right. Lakini angalia ni ipi ilikuwa ya kwanza kkubandikwa hapa. Ingawa to me its ok either ways kama hii ikiunganishwa kule au ile iunganishwe huku... Mods pls...
 
Yes mama, you are right. Lakini angalia ni ipi ilikuwa ya kwanza kkubandikwa hapa. Ingawa to me its ok either ways kama hii ikiunganishwa kule au ile iunganishwe huku... Mods pls...

Nadhani hii, labda kwa vile uliweka kwa kifupi watu hawakuelewa. Itakuwa vizuri zikiunganishwa.
 
Back
Top Bottom