Je hii ni kweli?

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,502
19,341
Siku ya fainali za kombe la dunia nilikuwa na rafiki yangu mmoja ambaye huko nyuma alikuwa ni mmoja wa maofisa katika serikali ya Bush. Kwa sasa hivi anahanja tu kama mimi na wewe akijitahidi kujipatia vijisenti hapa na pale katika biashara zake ndogo ndogo za uanasheria. Wakati Rais Zuma anakabidhi kombe la ushindi kwa kapteni wa Spain, jamaa yule akaniuliza swali dogo sana kuwa kwa nini viongozi wengi wa kiafrika hupenda kujitambulisha kwa symbols fulani kama ambavyo wafalme hujitambulisha kwa yale ma-crown yao? Nikapinga, lakini akasisitiza kuwa hilo scarf alilovaa Zuma ni identification kuwa huyo ni president!!!

zuma_gettyimages_1652581c.jpg

Kusistiza hivyo, akasema hata Haiti wanafanya hivyo. Nikamwambia, well, sijui taratibu za nchi mbalimbali, kila nchi wana utaratibu wao. Akasisistiza kuwa hata Tanzania tuna utaratibu huo ambapo First Lady wetu ana scarf anazotumia. Nikacheka kweli kweli, lakini akasisitiza kuwa wakati yuko Tanzania na President Bush mwaka juzi, kila alipokuwa akimwona first Lady wa Tanzania, alikuwa amevaa scarf hiyo. Mwishoni akasema labda nimekaa mimi nje muda mrefu kwa hiyo sijui yanayoendela huko nyumbani. Tulipoachana, nikasema ngoja nipitie kwa michuzi nione picha za First Lady wa Tanzania wakati wa ugeni wa bush nione alikuwa amevaa scarf ipi. Nilikutana na picha nyingi sana kama zionekanavyo hapa. Inawezekana kweli yule rafiki yangu alidhani kuwa hiyo ni scarf ya mama ni alama yake kulingana na position yake kwa vile huwa haachani nayo. Nadhani huo ndio mtindo wake mama yake ajitofautishe na wanawake wengine, lakini sina uhakika. je mnaojua protocol za Tanzania, je ni kweli kuwa first lady wa Tanzania lazima awe na scraf ya aina hiyo?

Nimeangalia pia marasi wa haiti, wanavaa scarf za aina yake kama ionekanavyo hapa chini
aristide-again.jpg Rene-Preval-2.jpg
 
Je, Maria Nyerere, Siti Mwinyi, Anna Makapa nao walikuwa wanavaa hiyo mitandio?
 
Nafikiri anavaa kama pambo tu. Kama ingekuwa ni alama ya ukuu, au ufalme basi angevaa Rais wa nchi kama ambavyo Zuma au marais wa Haiti wamevaa. Sasa yeye first lady ni mkuu wa nani/ni kiongozi wa nani? Hatukuwahi kumchagua yeye kuwa kiongozi wetu. Hata hivyo sikuwahi kumwona mama Mkapa amevaa. Kama kweli inamaanisha hivyo basi huyu naye ni limbukeni. Maana ukuu wa mtu hautambulishwi kwa mavazi bali kwa kazi nzuri anayoifanya.
 
Kaaaaaaaaazi kwelikweli. Hilo ndo tatizo la kufikiri kupita kiasi yaani mtu unaanza kutengeneza vitu kichwani badala kuishi katika uhalisia. Huyo jamaa ana-overthink.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom