Je hii ni kawaida au kuna tatizo?

Je hii ni kawaida au kuna tatizo?

BongeMwepesi

Senior Member
Joined
Aug 13, 2013
Posts
125
Reaction score
83
Habari wanajf,nimeoa yapata miezi 4 sasa na wife ni mjamzito wa miezi mitatu,sasa hali yake hii imemfanya awe anatapika sana na anatema mate sana,sasa siku za karibuni na mie nimejikuta kila nikiamka asubuhi lazima nitapike na najisikia kichefuchefu na nashikwa na usingizi muda wote hali hii imeanza kama wiki mbili zilizopita na inaendelea je kuna tatizo nimepata au hali hii utokea pia kwa watu wengine?naomba ushauri na uzoefu wako rafiki...asante
 
dah! Watu na vituko vyao,
Subiri waje na ushauri wao!!
 
Uuuuuupsi ivi hamfanyiwi jando nowdays
Kazi Ipo
 
Usihofu nilishawah kusikia kuna wanaume wake zao wakiw na mimba na wao wanapitia hali hizo mfano kaka yangu mimi mkewe alipokuw mjamzito yeye alikuwa anapata kichefuchefu na kula maembe
Mabichi lakn baada ya kujifungua hali hurudi kawaida
 
Nadhani hiyo ni hali ya kawaida kwa watuwaliozoeana na kuwa karibu sana, hivyo mmoja wao anapojisikia shida fulani kiafya na mwenzake pia anaweza kuathirika kisaikoloja na kujisikia hali kama ya mwenzake.kumbe na wewe huyo ni mke wako ni mwili mmoja, pengine mnashirikiana vitu vingi hivyo na wewe pia unapata baadhi ya anayojisikia yeye.lkn hiyo siyo homa ila ni mawazo yako tuu, punguza mawazo hali yako itarudi kuwa safi.
 
Nina rafiki yangu aliniambia mke akiwa mimba mwanaume anakuwa analala hovyo na kujisikia uchovu sana,labda na wewe ndio huko kwenye hali hiyo,inaweza kuwa hali ya kawaida tu itaisha.
 
Asante sana mkuu wasiwasi unapungua
 
Asante kwa kushare uzoefu wako na ushauri
 
Nina rafiki yangu aliniambia mke akiwa mimba mwanaume anakuwa analala hovyo na kujisikia uchovu sana,labda na wewe ndio huko kwenye hali hiyo,inaweza kuwa hali ya kawaida tu itaisha.

Asante umenipunguzia uoga
 
Hahahaha unamsaidia bi wifi lol

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Pole BONGEMWEPESI, kuna uwezekano hyo ikawa hali ya kawaida kutokana na ujauzito wa mkeo, ila ni vizuri ukaenda hosipitalini ukajipe uhakika unaeza ukawa na malaria...
 
Mkuu utakuwa mjamzito haki ya nani ha ha nakutania bana btw- hiyo hali huwa nasikia ni kawaida kwa waume usihofu yani hapo ndo unajua hicho kizygot chako kabisaaa! He he wanaume wasiosikia hiyo hali wakati wake zao ni wajawazito mujue mumechapiwa haha msinipige mawe we dare to talk openly loh!!
 
Huwatokea baadhi ya wanaume kipindi cha ujauzito wa wake zao,
Usihofu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom