Je hii ndio imekuwa Dar Es Salaam mpya?

Je hii ndio imekuwa Dar Es Salaam mpya?

Teknocrat

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2018
Posts
7,970
Reaction score
15,802
Mji umekuwa mweupe, hakuna hata watu
Wale watu wote waliokuwa wamejaa mitaani wameenda wapi?

Natabiri uhamisho wa wakaazi wengi wa Darisalama kurudi mikoani walikotoka katika kipindi hiki, na wakiwa huko watajikuta na kuona fursa nyingi sana mikoani kwao kwa kuwa maisha walioshi Darisalama yamewafumbua macho na kujua kila shida za watu unazigeuza fursa.

Na wengi watajipata huko na hawatataka tena kurudi kwenye mateso ya kuishi Darisalama...

Uzi tayari.....
 
Dar ni patamu sana
Mikoani napo ni patamu sana
Tanzania ni mbingu ndogo, nchi nzuri mno ukiwa na kazi ya kufanya na kipato cha kuridhisha. Ni siasa tu ndio zinaturudisha nyuma
Always kutakuwa na watu wanaopenda mikoani na wanaopenda Dar au Zanzibar, hao walioenda mikoani wanakaa siku chache, ni kama likizo tu. Ngumu kupoteza mapenzi yao kwa Dar kisa kujificha mikoani siku mbili tatu
Subiri utajionea mwenyewe, Dar itarudi kuwa vilevile
 
Hii inaweza kuwa ni big RESET..
Ni kweli ukiishi Darisalama unaona sehemu nyingine zote bado sana...
Lakini kadri unavyozidi kuishi na kupajua ndio unaanza kuona unababana na umati mkubwa sana kugombania fursa.....
Kuna wengine hasa vijana watakuwa na shinikizo kubwa kutoka kwa wazazi wao kutokana na maafa waliyoyaona ya vijana.
Unakuta hao vijana masikini walikuwa wanategemewa kwao, lakini wazazi mara nyingi kwao uhai kwanza hata kama huna kitu bora akuone karibu yake....
 
Watu wana majonzi, baada ya mwezi hili litathibitika wapo au wamerudi mikoani
 
Dar ni patamu sana
Mikoani napo ni patamu sana
Tanzania ni mbingu ndogo, nchi nzuri mno ukiwa na kazi ya kufanya na kipato cha kuridhisha. Ni siasa tu ndio zinaturudisha nyuma
Always kutakuwa na watu wanaopenda mikoani na wanaopenda Dar au Zanzibar, hao walioenda mikoani wanakaa siku chache, ni kama likizo tu. Ngumu kupoteza mapenzi yao kwa Dar kisa kujificha mikoani siku mbili tatu
Subiri utajionea mwenyewe, Dar itarudi kuwa vilevile
Umesema kweli. Mi Mafya sihami hata kwa mikwaju. Samaki bwerere, wali kg moja nazi 5. Dar ni ya kuwekeza na kufanya shopping tu
 
Back
Top Bottom