Je hii inawezekana TANZANIA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je hii inawezekana TANZANIA?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Game Theory, Nov 13, 2007.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2007
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa alizaliwa Aghanistan na ni mtaalam mzuri sana wa masuala ya Intel Relations...lakini America being America hawakujali kama ni Muislam wala kazaliwa wapi...sasa hivi anawakilisha United States kule UN...na alizaliwa MAZARI SHARIFF na ni PASHTHUN huyu!

  ANAITWA KHALIZAD ZALMAY  [​IMG]

  http://www.state.gov/r/pa/ei/biog/50305.htm
  huyu bibie anaitwa MADELINE ALBRIGHT naye hakuzaliwa United States, huyu alizaliwa na alikuwa ni Foreign secretary wa BILL CLINTON alizaliwa PRAGUE, Czechoslovakia (sasa hivi CZECH REPUBLIC)
  [​IMG]


  Je sisi tunaweza kuwakubalia wazaliwa nje ya Tanzania ambao wanamoyo wa kulitumikia Taifa letu bila kusimangwa?
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2007
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  GAMETHEORY,
  1. US is a mature democracy for over 200 years- and is made up of immigrants! It is unique even compared to other democracies in the world!

  2. Sisi bado- unakumbuka tu how Ulimwengu was humiliated? I don't think this happening in Africa-even Asia or even Europe! Remember what also happened to Kaunda and former PM of Ivory Coast!
   
 3. K

  Koba JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2007
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  tukiweza kupambana na mafisadi hili tutaweza tuu
   
 4. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #4
  Nov 13, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Nahisi tunaelekea huko huko, ingawa Wabongo ni wagumu kukabili hali hii. Ukiangalia bungeni tuna watu kadhaa ambao huenda baadhi yao hawakuzaliwa hapa. Hata katika ngazi za serikali za mitaa, tuna wageni walio 'enyejishwa' kibao sana ama kwa kuoa ama kuolewa na Wabongo, ambao ni viongozi wazuri tu. Sema tuache ubaguzi ili kufikia lengo hili, adhawaiz sio rahisi sana. Kwa sababu zilizo nje ya uwezo, nitataja majina siku nyingine.
   
 5. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #5
  Nov 14, 2007
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 3,589
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0
  Yule mama Joan Wicken hakuchukua uraia wa Tanzania?
   
 6. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #6
  Nov 14, 2007
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 687
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  kwani watu hamkuona issue ya Miss Tanzania Richa ilivyokuwa?
   
 7. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #7
  Nov 14, 2007
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Very well said. Kulinganisha Marekani na Tanzania ni sawa na kulinganisha mbingu na ardhi, au Ronaldino wa Brazil na Joseph Kaniki wa Taifa Stars. Vitu viwili tofauti kabisa

  Hiyo Marekani tunayoiona leo haikushushwa toka mbinguni, kila kitu kimejengwa na Wamarekani wenyewe kwa jasho lao. Kuanzia demokarasia, utawala wa sheria mpaka miundombinu. Imewachukua miaka 200 kufikia hapo walipo leo.
   
 8. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #8
  Nov 14, 2007
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  i) Ok, hatusemi tuwe kama wao leo hii. Lakini je, tupo safarini kuelekea huko? Je, tumepanda basi (CCM) inayoelekea huko?
  Nionavyo mimi ni kwamba tunataka kwenda Dodoma, lakini tumejikuta tupo katika basi linaelekea Mtwara. Hatutafika Dodoma kamwe!

  ii) Hivi mbona mambo ya kijinga tunaweza kuiga haraharaka kutoka kwa hawa wandugu, lakini ikija mambo ya maana tunaanza kuleta vizingizio vya hooo hao wamekaa miaka 200? Kwa mfano, kununua mabenzi mazuri kwa viongozi wetu na kufanya matanuzi mengi kama wanavyofanya hao waamerika hatusubiri tuwe na miaka 200 kama wao, lakini ikija kwenye mambo ya maana ya maendeleo hatuachi kutoa vizingizio inakuwaje? Hii haijakaa sawa!
   
 9. M

  Mwakilishi JF-Expert Member

  #9
  Nov 14, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 484
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu Kitila,
  hapo umesema, ikifikia kuiga mambo ya maana utasikia vilio vya "ohhh sisi taifa changa" lakini kuiga upumbavu wa wamagharibi tuko mstari wa mbele,(ushahidi: mikataba na manunuzi yetu mabovu tunayofanya kila leo) in short ni kwamba hatutaki wala hatupendi mabadiliko ya maana hilo hatutaki kabisa kusikia. Tuko comfortable kwenye uduniduni wetu tuliojigubika mradi we are armed with visingizio lukuki.
   
 10. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #10
  Nov 14, 2007
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,763
  Trophy Points: 280
  Muungwana Kitila, ungekuwa karibu leo ningekupa hata bia mbili pale Kibadamo!!! yaani ni ukweli tupu, hapa hakuna cha maendeleo wala nini ni ubinafsi wetu tuu! Jiulize leo Obama angerudi Kenya hata udiwani asingeruhusiwa kugombea!

  All in all, Africans tuna visingizio vingi sana zinapokuja substantive issues! na tatizo ukifuatilia sio swala la patriotism ni swala la kulinda parochial interests za wachache ambao always wanaogopa mawazo mbadala!
   
 11. Mwanamalundi

  Mwanamalundi JF-Expert Member

  #11
  Nov 14, 2007
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 3,034
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180
  Inawezekana kwa kiasi fulani. Kuna watusi waliokimbia rwanda miaka ya nyuma ambao wanafanya kazi katika sekta muhimu tanzania. Kwa mfano, wengi wapo usalama wa taifa, etc. Wengine walikuwa wanafundisha chuo kikuu cha dar es salaam. Kwa mfano, Professor Rutayisire aliwahi kufundisha miaka ya 80 pale chuo kikuu cha dar es salaam. Baada ya kagame kuchukua nchi, huyu bwana alirudi rwanda. Vilevile, professor wamba dia wamba aliwahi kuwa muhadhiri pale chuo kikuu cha Dar es salaam. Hawa walilitumikia taifa la tanzania bila kusimangwa na watanzania.


  Ukija katika nyanja ya siasa, waziri mungai inasemekana kuwa ana asili ya kenya. Abulrahman kinana inasemakana ni msomali. Arcado ntagazwa, aliyewahi kuwa waziri katika kipindi cha awamu ya 1, 2, na 3 inasemekana alizaliwa burundi. The list is endless.

   
 12. Mwanamalundi

  Mwanamalundi JF-Expert Member

  #12
  Nov 14, 2007
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 3,034
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180
  Ni kweli unayoyasema. Labda nikuulize maswali mawili. moja, hiyo miaka 200 unayozungumzia ina maana sisi hatukuwepo katika huu ulimwengu??? Mbili, les us forget democracy, rule of law and infrastructure. Swali analouliza Gametheory ni je, tunaweza kuwatumia watu waliozaliwa nje ya tanzania bila kuwasimanga??? Jibu swali.
   
 13. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #13
  Nov 14, 2007
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160

  Kitila,
  Sidhani kama ni swala tu la kuiga. Most African leaders and the ruling elites are an extension of Western elites Ndo maana JK, na mawaziri ukiwauliza leo kama wao wanawakilisha na kutetea watu maskini-hata ni ngumu kujibu- kwani maisha yao ni mazuri kuliko elites wa Magh!

  Hayo mabenzi sii yananunuliwa Magharibi? Fat Accounts of African elites sii zipo Magh? Stolen Wealth- converted into nyumba, n.k sii zipo Magh? Je unadhani haya mambo ni siri na Magh yawaoni? Siyo visingizio- Africans we have our own portion of blames- but we are also victims of foreign interests! We need to fight in all fronts!

  We need a new Political, Social and Economic order. Ila pia life style of our elites lazima ibadilike! Remember kuna wakati Chenge aliulizwa msimamo wa serikali over mashangingi akasema shangingi la 100 M sii ghali! Eti tunataka waziri atembelee Bitto? Yet hawa hawa wabunge huchaguliwa every 5 years tena kila mwisho wa ubunge kila mbunge hupewa 30M kumsaidia campaign!

  Nafikiri mstakabali wetu- ni juhudi za kundoa injustice Tanzania, ila pia globally!
   
 14. Mkereketwa

  Mkereketwa JF-Expert Member

  #14
  Nov 14, 2007
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hiyo kwa USA inawezekana kabisa na ndiyo maana walianzisha utaratibu wa GREEN VISA, kwa ajili ya ku-drain talented people toka nchi masikini na kuwaruhusu waishi na kuiendeleza USA. Na kwa kuona watu wa Europe wanapigwa bao na Marekani kwa utaratibu huo nao wameanzisha BLUE VISA ambayo lengo lake ni sawa na la Wamarekani.
   
 15. B

  BROWN Member

  #15
  Nov 14, 2007
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nchini India kuna mwanamama anaitwa Sonia Gandhi,ni President wa Indian National Congress,huyu ni mzaliwa wa Italy.
  Kama mtu anafanya kazi vizuri na anajali maslahi ya wazawa,hakuna haja ya kumbagua wala kumtenga,ubaguzi usiokuwa na maana hautakiwi,unasababisha ukiritimba kwenye vichwa vya watu.Inawezekana na ilishawezekana siku nyingi tu.
   
 16. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #16
  Nov 14, 2007
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Sii India huyu mama alishtuka na kukataa kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu- kwa vile sii mzawa! Aliogopa atauliwa!
  Hii democrasia tunayoiona US- ni vigumu kulinganisha na India!
   
 17. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #17
  Nov 14, 2007
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..hit the bull! sema unayemlenga au walenga then tutachambua!

  ..lakini kama alivyosema mtu huko juu,we need a matured democracy to do just that!
   
 18. K

  Koba JF-Expert Member

  #18
  Nov 15, 2007
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  to me ubaguzi wa aina yeyote ni ignorance tuu,na ile issue ya yule MISS Tanzania ilinishtua sana na imeonyesha jinsi watanzania walivyo intorelant & ignorant,watanzania wengi bado ni wajinga inabidi waelimishwe ubaguzi wa aina yeyote hauna maana na haukubaliki katika jamii yenye usawa na haki,sio kwa makelele jukwaani tuu hata kisheria itasaidia.
   
 19. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #19
  Nov 15, 2007
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,969
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  Haaitawezekana.Kwanza kufikiria tuu ni kuonyesha kutokuwa mkomavu katika habari mbalimbali.Lakini ni ktokuwa mchambuzi sahihi wa mambo.Huyo Mpashtuun lazima awe raia wa marekanikiakili na kimwili.Pili uislamu wake ni wa kiimani au kwa jina lake.Jee nchi gani zingine kama uingereza,ufaransa.urusi zimefanya hivyo.kabla ya kulinganisha marekani na Tanzania ambayo bado iko nyuma kimaendeleo kwa miaka kadhaa.isitoshe marekani inaweza kumpa madaraka mtu yeyote.akileta rongorongo inaweza kumuadhibu hata akikimbilia popote duniani.Ndugu yangu mawazo ya kusadikika umeyapata wapi.ningeweza kuendelea kuchambua hoja moja baada ya moja lakini gharama za internate za bongo zimepaa
   
 20. Nungunungu

  Nungunungu JF-Expert Member

  #20
  Nov 15, 2007
  Joined: Feb 13, 2007
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunahitaji muda kidogo tu kuweza kutoa mshindi wa BBA na Miss World Africa ila tunahitaji miaka 200 kuweza kung'amua na kuvutia vipaji vya kuiendeleza nchi!! Kazi ipo.
   
Loading...