chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 21,569
- 28,486
Habari wanaJukwaa pendwa MMU,
Nipo mbele yenu siyo kuhukumiwa bali kuomba ushauri kwa hili jambo ninaloliteta mbele yenu.Nina mpenzi wangu ambaye nimedumu naye katika mahusiano yapata miaka mitatu sasa, katika harakati za kutafuta maisha imetokea tukawa tunaishi mikoa miwili tofauti ila ninapopata likizo ya majukumu huwa tunakutana.
Mimi kuna wakati maisha yananipiga nakuwa sina hela kabisa na wakati mwingine madeni kuniandama sana, kuna wakati huwa namshirikisha huyu mpenzi wangu hali halisi ya mimi kuishiwa hela na bila hiyana huniuliza " Unadaiwa Kiasi gani au nikusaidie kiasi gani mpenzi" ? Kiukweli aibu hunijaa ghafla na kuanza kujiuliza nimuambie kiasi gani? Lakini huwa namtajia kiasi halisi ninachokuwa nakihitaji na bila hiyana huniambia " basi usijali nitakutumia" Punde nashangaa Tigo Pesa inasoma salio. Dah!!
Wakuu siyo mara ya kwanza kumuomba anisaidie hela huyu mpenzi wangu na mimi hata siku moja hajawahi kuniomba hata shilingi mia ingawa nafahamu yeye anaishi maisha ya kawaida tu na hajawahi kuniambia nimrejeshee hela anazonisaidia hata siku moja na wakati nikijaribu kufanya hivyo hunikatalia. Mungu akipenda tuna mipango ya kuanzisha familia lakini wakuu naombeni mnipe ushauri.
Hivi suala la mpenzi wangu kunisaidia fedha mara kadhaa ninapokuwa na uhitaji linaweza kuvuruga mahusiano yetu?
Nawasilisha