Je, hawa tu ndio CCM vyuo vikuu?

Vyuo vikuu maana yake ni chuo zaidi ya kimoja kama hiyo ndio maana yake basi ni wachache sana.......#mtazamo.

hao ukiwaangalia wote wana sura ya chadema ukitaka kujua ccm haipendwi vyuoni angalia jimbo la ubungo huwa haliongozwi na ccm toka vyama vingi vilipoanza
 
"Mbona kama vile mwandiko wa mabango yote ni kama unafanana!??
Ama kweli, "ndio maana Kenya wanatudharau"

Si kenya tu Kamanda Dunia nzima wanaidharau siasa ya Tanzania kwasababu ya CCM. Usanii mwingi sana, Kumbukeni Nepi sijui Nape ni msanii na alishatangaza kuwa ni msanii, yawezekana kuna Movie anaanda ya namna hiyo. Tusimdharau sana maana yeye kuwa CCM ni kwa maslahi zaidi na sio kwa uchungu wa nchi. Mwisho ni Kwamba msajili wa vyama vya siasa angalie umuhimu wa kupitia Katiba za vyama vyote ili aone kwanini Viongozi wa Serikali hawatii Katiba ya nchi waliyoapia na badala yake kila kitu tunasubiri majadiliano ya vyama vyetu vinasema nini, huu ni upuuzi.
 
Once upon a time PWD meant public works department. Not any more, baada ya maandamano haya PWD is officially punda wengi duniani.
 
Kweli nimeamini ukiwa ccm na uwezo wa kufikiri huwa unapungua. Sasa wanampelekea ujumbe nape kwani yeye ndo raisi wa nchi?? Sikua najua kama kuna vijana bado wamepotea kihivyo ila nawapa pole sana
 
Mbona mwandiko ni wa mtu mmoja? Mabango yote ameyaandika Nape, kisha akakodi kikundi cha kulipwa cha kulia na kuimba misibani cha huko Bonyokwa. Kuna vijana wawili wa kikundi hicho nimewaona kwenye picha. Kuna vijana kama kumi hivi ndio wanachuo ambao wameahidiwa ukatibu tarafa wakihitimu masomo yao. Yule mmanga anayedai ni mwenyekiti inasemekana amekwisha "disco", hivyo kisheria si mwanafunzi.
 
Ngoja na chadema waandamane kumpongeza zitto,utasikia maandamano hayana vibari,sisa hairuhusiwi vyuoni
alaf mbona wanatia huruma sana yani wako wachache kama wanafunzi wa shule ya secondary magamba
 
Jamani mimi labda sikuelewa vizuri.
Nakumbuka kuwa serikali ilipiga marufuku siasa katika vyuo vikuu na kwamba ikionekana mwanafunzi anajuhusisha na siasa atafukuzwa shule. Sasa hii sielewi imekaaje ? au kwa ccm Ruksa
 
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipokea Vijana wa Shirikisho la CCM la vijana wa CCM wlioko vyuo vya Elimu ya Juu, walipofika leo kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Dar es Salaam, kumfikishia ujumbe wao kuhusu mawaziri na watumishi wa serikali wanaotuhumiwa kuhusika na upotefu wa fedha za umma.

Nape akisoma ujumbe kwenye moja ya mabango waliyofika nayo wanafuvyo hao.

Wanavyuo wakionyesha bango la kuwataka wasaidizi wa Rais kuwajibika inapobidi.

. Nape akisoma ujumbe uliloonyesha kumvutia zaidi kwenye moja ya mabango ya wanavyuo hao.

Vijana hao wakionyesha bango lenye ujumbe mahsusi kuhusu maana ya Mapinduzi.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na vijana wa Shirikisho la CCM la vijana wa CCM wlioko vyuo vya Elimu ya Juu, walipofika leo kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Dar es Salaam, kumfikishia ujumbe wao kuhusu mawaziri na watumishi wa serikali wanaotuhumiwa kuhusika na upotefu wa fedha za umma

Kweli naona propaganda za CCM zinaanza kuishiwa nguvu. Hata hao wanafunzi wameshindwa kuandika kitu cha maana kwenye hizo poster zao. Pia inaelekea hao ni watoto na ndugu wa vigogo. Haiwezekanai Univeristy student akawa utando kichwani kiasi hicho!! Inaelekea walikurupushwa tu ndiyo maana hata kuandika wamekoseakosea!!
 
Wanafunzi wa chuo kikuu hawawezi kuandika bango lenye maneno kumi tu ya Kiswahili bila ya kukosea?! #Aibu

*Kujiuzuru iwe kujiuzulu
 
Siasa vyuoni vipi tena? mbona hapa ni eneo la car parking udsm? Nape alijuaje wataandamana akaenda kuwapokea? kwa nini wasingeandamana kuelekea LUMUMBA? CHEAP POLITICS.
 
Duu!! Hii nimeipenda sana. Ni vizuri kwamba wamejionea wenyewe kuwa walichofanya ni kichekesho ambacho badala ya watu kucheka wamesktika sana, lakini jambo moja nimeliona kutoka katika maandamano yao haya ni kwamba baada ya hapa, vijana wote hawa watakimbilia kwa M4C ili kujisafisha na hii aibu.

Kusema kweli hii tamu hasa kama kweli hawa vijana sijui kumi au Ishirini wametoka vyuo vikuu, inawezekana ndo wale wa-admission za mgongo wa shangazi, mwenyekiti wa CCM, katibu kata n.k. lakini wakae wakijua "KIMBUNGA KINAKUJA NA KAMA HAKITANG'OA NYUMBA BASI KITANG'OA WALAU BATI AMBAYE NI WAZIRI MKUU-MIZENGO PINDA" Bagambila balinsi baliiguru kuulila

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipokea Vijana wa Shirikisho la CCM la vijana wa CCM wlioko vyuo vya Elimu ya Juu, walipofika leo kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Dar es Salaam, kumfikishia ujumbe wao kuhusu mawaziri na watumishi wa serikali wanaotuhumiwa kuhusika na upotefu wa fedha za umma.

Nape akisoma ujumbe kwenye moja ya mabango waliyofika nayo wanafuvyo hao.

Wanavyuo wakionyesha bango la kuwataka wasaidizi wa Rais kuwajibika inapobidi.

. Nape akisoma ujumbe uliloonyesha kumvutia zaidi kwenye moja ya mabango ya wanavyuo hao.

Vijana hao wakionyesha bango lenye ujumbe mahsusi kuhusu maana ya Mapinduzi.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na vijana wa Shirikisho la CCM la vijana wa CCM wlioko vyuo vya Elimu ya Juu, walipofika leo kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Dar es Salaam, kumfikishia ujumbe wao kuhusu mawaziri na watumishi wa serikali wanaotuhumiwa kuhusika na upotefu wa fedha za umma
 
ilikuwa kwenda kwenye maandamano ni elfu 10000 ukiwa na shati la kijana unapata 15,000 ila pamoja na njaa wengine hawakwenda.na wengine walipewa mshiko wakaishia bar hata kwenye maandamano hawakufika.kwa stail hii lazima ninunue shati la kijani la kupigia mahela ya bure na mabia ya bure kwani walivyotoka kwenye mkutano walifunga bar.
 
hawa ndio wasomi wakuleta mabadiliko..wanamwomba Nappe awape amri ya kuwatoa wafanyakazi wasaliti serikalini kama nani.?
 
katibu wa halmashauri kuu ya taifa ya ccm, itikadi na uenezi nape nnauye akipokea vijana wa shirikisho la ccm la vijana wa ccm wlioko vyuo vya elimu ya juu, walipofika leo kwenye ofisi ndogo ya makao makuu ya ccm, dar es salaam, kumfikishia ujumbe wao kuhusu mawaziri na watumishi wa serikali wanaotuhumiwa kuhusika na upotefu wa fedha za umma.

nape akisoma ujumbe kwenye moja ya mabango waliyofika nayo wanafuvyo hao.

wanavyuo wakionyesha bango la kuwataka wasaidizi wa rais kuwajibika inapobidi.

. Nape akisoma ujumbe uliloonyesha kumvutia zaidi kwenye moja ya mabango ya wanavyuo hao.

vijana hao wakionyesha bango lenye ujumbe mahsusi kuhusu maana ya mapinduzi.

katibu wa nec, itikadi na uenezi, nape nnauye akizungumza na vijana wa shirikisho la ccm la vijana wa ccm wlioko vyuo vya elimu ya juu, walipofika leo kwenye ofisi ndogo ya makao makuu ya ccm, dar es salaam, kumfikishia ujumbe wao kuhusu mawaziri na watumishi wa serikali wanaotuhumiwa kuhusika na upotefu wa fedha za umma

mimi ni mwanafunzi wa elimu ya juu, mwanachama wa chadema ma muumini wa movement for critical change.

Inasikitisha kuona msomi yupo ccm.
 
Back
Top Bottom