Je hapa naweza kuishtaki serikali? Na je ni hatua gani za kufuata?

eity 4

Senior Member
Dec 7, 2014
147
206
Niliingia mkataba na Kamati ya ujenzi kwa niaba ya halimashauri wa kujenga wodi ya wazazi kwenye kituo cha afya. Mkataba ulikuwa nijenge jengo kwa miezi mitatu.

Mimi kazi yangu ilikuwa kujenga na wao Kamati walete vifaa na kunilipa labour charge.

Sasa kazi imesimama ni mwezi wa tisa sasa, sababu hawaleti vifaa site, na kunilipa malipo yaliyobakia hawataki wanasema mpaka nimalize kazi, huku vifaa hawaleti.

Hapa unatakiwa kufanya nini?
 
Alafu subiri wanasiasa siku wakija kwenye mradi na makamera wanakutoa sadaka na matamko kibao! NA kashfa kibao kuonesha kuwa wewe ndio chanzo cha mradi kukwama
 
Niliingia mkataba na Kamati ya ujenzi kwa niaba ya halimashauri wa kujenga wodi ya wazazi kwenye kituo cha afya. Mkataba ulikuwa nijenge jengo kwa miezi mitatu.

Mimi kazi yangu ilikuwa kujenga na wao Kamati walete vifaa na kunilipa labour charge.

Sasa kazi imesimama ni mwezi wa tisa sasa, sababu hawaleti vifaa site, na kunilipa malipo yaliyobakia hawataki wanasema mpaka nimalize kazi, huku vifaa hawaleti.

Hapa unatakiwa kufanya nini?
Mkataba unasemaje kwenye vifungu vinavyohusu utekelezaji wa mkataba yaani performance clause?

Rejea kwanza mkataba.
 
Mkataba unasemaje kwenye vifungu vinavyohusu utekelezaji wa mkataba yaani performance clause?

Rejea kwanza mkataba.
Jukumu langu lilikuwa kujenga kama local fundi na wao walete vifaa.Mkataba wa utekelezaji miezi mitatu.
 
Jukumu langu lilikuwa kujenga kama local fundi na wao walete vifaa.Mkataba wa utekelezaji miezi mitatu.
Kama wamekiuka unaweza kwenda kushitaki kwa kukiuka mkataba, ukiomba watekeleze mkataba ama wakulipe kwa kadri ulivyofanya n.k
 
fuatilia kwa Mkurugenzi au hata DC na ikibidi cheki na RC...Nenda na vielelezo

wakati mwingine wanaweza wakawa wamekula pesa na hata mabosi wao hawajui.

kuwapeleka mahakamani ifanye iwe option ya mwisho baada ya kufanya hizo hatuaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom