Je, hapa kuna ujirani mwema?

Je, hapa kuna ujirani mwema?

farujohni

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2017
Posts
212
Reaction score
285
Ilikuwa tarehe moja mwezi wa 6 ambapo nilipokea simu muda wa saa 1 jioni nikitaarifiwa kuwa mke wangu amedondoshewa kipigo na kijana wa jirani na mama yake mpaka kupoteza fahamu.

Ndipo nilimpigia simu shemeji yangu aende eneo husika ili aweze kutoa msaada. Baada ya majirani kuendelea kummwagia maji na kupepea bila kurudisha fahamu ikabidi wampeleke polisi ili wapate kibali cha kumpeleka hosptali.

Baadae polisi wakaja kufanya upelelezi usiku huo huo wakawakamata. Sasa ilikuwa Ijumaa wakakaa sero mpaka Jumatatu ndo wakadhaminiwa.

Kipindi chote nilikuwa sipo kesi imeenda mimi nikaonesha kuwanyima ushirikiano polisi ili kesi ifutwe na kulinda heshima ya ujirani na kweli wakaenda mahakamani mara 3 kesi ikafutwa.

Sasa jirani kanitengenezea kesi polisi eti mimi na mke wangu tumemtukana siku ya Jumamosi ambayo mimi nilikuwa mpirani naangalia mechi ya Simba.

Je, nifufue kesi yangu? Maana kwenye ile kesi sikutia saini ya kufuta na kuna karatasi sikupeka polisi au nisamehe na kuangalia dhamira ya kunitengezea kesi?
 
kama ni mimi ningeama tu...si uwoga bali kujiepusha na matatizo
 
Kwa maelezo yako, ninamuonea huruma sana mkeo aliyepata madhila makubwa bila kupata utetezi wowote.
Jukumu ambalo lilikuwa lako la msingi wewe mmewe, badala yake ukathamini na kutetea ubaya wa majirani zako mabazazi, sasa unavuna malipo.

Hao si jirani, bali ni maadui zako wa karibu.
Si kila anayeishi karibu yako ni jirani, no!

Wangelikuwa ni majirani wema na kwa kumtambua kuwa mkeo ni mwanandoa, kama aliwakosea, basi wangelileta kwanza mashitaka kwako na mkakaa pamoja kumaliza tofauti zilizopo, huo ndiyo ujirani.

Lakini hili la kuchukua sheria mikononi mwao, hapana.

Wamekudharau sana kukupigia mkeo na wewe kushindwa kuchukua hatua yoyote ya maana dhidi yao, ndiyo maana wanaendelea kukuchimba mpaka leo.

Sina taaluma ya kisheria kujua kama kesi iliyofutwa kwa kukosa ushahidi kama inaweza kufufuliwa.
Lakini busara ni kwamba, kwanza hangaika nao kumaliza kesi hii ya kizushi iliyopo mezani.

Ninatumaini kesi ya kubambikiwa ikipata wanasheria wazuri, lazima tu itagonga mwamba baada ya ukweli kujulikana.

Kwa sasa usilifufue jambo ulilokwishalisamehe, maana ukweli ukijulikana, basi utaonekana wewe ni mbabaishaji na haya mashitaka ya sasa yakaonekana yana ukweli.

Epukana na mambo ya uzushi na kudanganya mahakama, isije ikakugharimu.

Likiishamalizika hili, kaanao kimahakama, ninamaanisha kuwa, uwe nao makini juu ya matendo yao na kukusanya ushahidi wa kila jambo na watakapoingia kwenye 18 zako, usije tena kuchezea shilingi chooni.
Hao si majirani bali ni maadui zako waliojipambanua ubaya wao mapema, hawasitahili msamaha. Pole sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha Roho ya utu kwa mashetani mkuu. Fufua kesi na kama una watoto wadogo fungia ndani

asante sana kwaushauri namimi nimewaza hivyo nisifufuwe kesi.kwanza nimalizane nao nakesi.yao ya kizushii maana nilipo enda polis ndio walio.nieambia kuwa.kutokana nahujuma.za jirani.yangu kwamba ile kesi kunamtuhumiwa mmoja ambae nikijana wake hawakufanikiwa kutia nguvuni sasa wamkate wana kumpeleka mahakani kwakosa baada,ya kukimbia siku ya,tukio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom