Je, engineering ina soko kwa Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, engineering ina soko kwa Tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Roland Bushumba, Feb 25, 2012.

 1. R

  Roland Bushumba Member

  #1
  Feb 25, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nimemaliza form 4 mwaka jana na nimefaulu mitihan yangu vizuri.Comb. Ambayo ningependa kuendelea nayo kwa A'level ni PCM coz napenda kuwa engineer ila habari nilizozisikia kwa watu mbalimbali huwa wanasema ukiwa engineer kwa Tanzania unaweza kuzunguka na vyeti vyako bila kupata kazi.Je, kuna ukweli wowote?Na kwa engineering ni coz zipi nzuri?Naomba mnisaidie.
   
 2. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2012
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,780
  Likes Received: 6,261
  Trophy Points: 280
  Si kweli dogo, we piga PCM na mwisho wa siku utakuwa Engineer. Ni mapema mno kwako kuanza kuulizia ati kozi ipi nzuri kwa ''Engineering''. However, zamani kidogo ''Electrical Engineering'' ilikuwa inakimbiliwa sana na watu wengi, na hivyo wakawa wanachukua waliofaulu vuzuri zaidi (I za tatu, nne mpaka 5). Ukikosa hapo ulikuwa unaambulia Civil Engineering, then Mechanical and Chemical & Process Engineering. Sijui siku hizi hali ipoje baada ya kuzipanua hizi course
   
 3. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Cku hz naona vipanga wengi wanakimbilia telecom,sa cjui ka inalipa au vp.
   
 4. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Form 4 bado sana kijana!! Ila kuna huu msemo, "An Engineer can be anybody, and not anybody can be an Engineer". Kwa hiyo kama PCM inapanda wewe piga shule uko penyewe. Kuhusu ajira, Engineers wanahitajika kila kona ya dunia hii! Tanzania hadi sasa hawatoshi, mi nilipomaliza undergraduate, nilikaa miezi 2 bila kazi, baada ya hapo nikawa nachagua niende wapi niache wapi!! Kifupi kazi ziko nyingi, na haziishi leo wala hivi karibuni kwani duniani kote, wahandisi wahatoshi.

  Utakapoona engineers wanakosa kazi, basi ujue tutaanza kupiga hatua mbele kubwa kwani watalazimika kuanza kuwa wabunifu zaidi na kujikuta nchi inatengeneza bidhaa nyingi za ndani badala ya kuimport kutoka china au nchi zingine.
   
 5. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Dogo kama namba unaziweza soma Engineering.
  Wakati ujao Tutaingia katika Duru mpya kabisa za Engineering.

  Kazi za kuajiriwa ni kweli zinaweza kukosekana lakini kazi za kujiajiri katika ubunifu zitakuwepo daima.

  Fikiria uwingi wa pikipiki pale Tanzania, Je wewe kama ni Engineer unweza fanya nini ili kugeuza pikipiki hizo kufanya kazi nyingine muhimu zaidi ile ya kubeba watu.

  Huko India
  Pikipiki zinatumika kama Mobile Mill machine, Mashine ya kusaga unga.
  Bangladesh wanatumia ku pump maji ya visima na Generata za umeme, power ya kukata na kulanda mbao .
  Wengine wanamodify,wanafunga Gia box na Exeli ya suzuki na kutengeneza pickup
  Tukiweza kufanya pikipiki zikatumika usiku na mchana kuisadia familia nadhni tutaweza kusukuma gurudumu la maendeleo bila msaad wa JMK naMafisadi wenzake. Mzee anasanya mchana kutwa jioni pikipiki inaunganishwa na generator kufua umeme watoto wanafanya HW.mara mojakwa wiki inavuta maji ya kisima na kujaza tanki la lita 20,000.

  Watu wanageuza Toaster kuwa Heater sehemu zile za baridi kama kwetu Makambako na kule Yakobi kwa shangazi yangu Anne Makinda

  Ukiwa Engineer unweza kuungana na mchomelea mageti na kuyadizaini upya ili yafunguke na kujifunga Automatically kwa kutumia ujanja mdogo sana wa kujenga remote receiver ya kubadili polarity katika motor,mnyororo na remote.

  Dunia ijayo hivi pundeni dunia ambayo itahitji watu kufikiri mar 3 hadi 4 ya watu wanavyofikiri sasa hivi.
  Engineer anaweza kuwa Meneja mzuri tu lakinisi rahisi sana kwa muhasibu kuwa Engineer mzuri

  Tanzania imejaa taka kutoka nchi zote duniani. Endapo wote tutaamua kuwa malawyer kuna siku tutashinda kesi zote lakini tutashindwa kuzuia watu wasifanye nchi yetu dampo kwani hata kesi ya mfanya biashara atakaye kuleta taka nchini mwetu nayo itashinda ahakamani.

  Hata hivyo dogo kama lengo lako ni michuzi basi somea mambo ya finance ili uwe karibu zaidi na michuzi.
   
 6. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,915
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  "Engineers always build the World"...ingawa sina kazi lakini am proud to be an engineer....mi nimefanya Civil Engineer na bado nahaso huku kitaa lakini sijakata tamaa coz I knw one day YES....na ni kweli mainjinia wengi wanasota huku kitaa hili halina ubishi.

  Lakini ni future nzuri sana kuwa engineer than doing BCom or accounts!!
   
 7. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Usiwe na shaka.
  Saidia tu kuiondoa CCM na wabunge wake vilaza kuna kazi ya kujenga upya jiji la Dar Mitaa yake, brabara zake na mifereji yake ya maji machafu.
  Kutakuwa na mradi wa nguvu wa kulifanya jiji la Dar liweze kubeba watu 25,000,000 bila matatizo yeyote.
  Fikiria sehemu ndogo ya eneo kama eneo la yale maghorofa ya Msajiri Ubungo itakuwa na uwezo wa kuhifadhi familia 3000 kw wastan wa vyumba vitatu kila familia bila matatizo.
  Usafiri wa Vipanya vinavyomiliiwa na Wawaziri, Wakuu wa polisi, Majenerari wa jeshi, Usalama wa Taifa na hata abalozi wa wetu itkuwa ni historia ya zama za giza na machafuko.
  Tutakuwa na mabasi makubwa kama yale ya Icarus enzi za UDA yaliyo madogo yatabeba abiria 75
  Umeme utawaka usiku na mchana uonavyo jua na utakuwa wa uhakika kama kuvuta hewa.

  Ulisha wahi kusikia mgao wa jua? Kwamba leo linawaka Msasani Manzese walietu?
  Mgao wa jua unawezekana tu kama CCM wataendelea kuund serikali ya JMT.

  Kutakuwa na barabara za kupita juu kwa juu za kwenda kai ya maili 120KM/saa zikiwa zimebebwa na miguzo ya nguvu ya cement kutoka picha ya ndege,pugu,Boko,Geza ulole mbagala hadi city center.
  Cement tunayo
  Nondo tunazo
  Mchanga Tunao
  Kokoto ziko kibao
  Mafundi mpo mmejaa tele.
  Hapa Mechanical engineers,Water engineers, soil chemistry engineers, civil engineers, electrical engineers, surveyors, Archetercture engineer na environmenta engineer watakutana na kuwek Bongo ao pamoja kutengeneza barabara za nguvu za juju kwa juu katika jiji la Bandari Salama Akina Kikwete Mkapa Mwinyi na wababaishaji wengine wote wa CCM watashuhudia mageuzi haya makuuwakiwa hai.

  Utakuwa mwisho wa kila nyumba kuchimba shimo la choo vinyesi harufu kuzagaa kila kona
  Utakuwa mwisho wa mafuriko kujitakia jijini Dar
  Mifereji ya chini kwa chini yenye uwezo wa kubeba maji yote machfu itajengwa bila kubomoa nyumba ya mtu yeyote. Utaalamu huo upo na umetumika mahali pengi duniani isipo kuwa Tanzania


  Dogo kila kitu kipo tatizo ni Uongozi wa serikali ya CCM tu.

   
 8. mtzedi

  mtzedi JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2012
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 372
  Trophy Points: 180
  soko kubwa la kujiajiri lipo. pia unaweza soma bsc education ndo soko lipo la kuajiriwa na gvt ila mshahara sasa mpaka mei mosi
   
 9. R

  Roland Bushumba Member

  #9
  Feb 25, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asanteni wote kwa kunitia moyo na kunifanya ni zidi kuipenda zaidi engineering kweli hii ndo JF.Ila jamii inayonizunguka hapa kwe2 inanishawish kusoma PCB Eti niwe daktar ila moyo wangu upo kwenye uhandic coz cna interest na M.D eti kisa wanataka nilipwe mshahara mkubwa na kwa haraka.Thaq u a lot guyz kwa kunitia moyo.Kip t up!
   
 10. R

  Roland Bushumba Member

  #10
  Feb 25, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole kijana kwa kuhaso ila 1day yes kama msemo wako unavyosema.Ila ningependa nikuulize ni kwa kipind gan umehaso kitaa?
   
 11. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #11
  Feb 25, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,118
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  Soma Computer Science au kitu kama hicho, uzuri wa Computer Science ni kuwa kujiajiri ni rahisi zaidi, unahitaji laptop tu unaweza kuanza kufyatua products, Mobile Apps, Websites, Desktop software etc na market yako ni global automatically hakuna haja ya kuangalia soko la TZ peke yake.

  Kufanya kitu kama hiko kwenye fani za traditional Engineering ni vigumu zaidi, plus nchi zengine wana resources ambazo sisi hatuna katika traditional engineering, lakini kama ni programmer wewe na Facebook mna access ya most software hizo hizo.

  Hakikisha unafanya project zako mwenyewe na kuangalia technology mpya maana University zinakuwa ziko slow kubadilika so unaweza ukasoma vitu vingi ambavyo havina market.
   
 12. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #12
  Feb 25, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145

  Dogo fanya kitu ambachoi unapenda, haya mambo ya kusema unasomea kitu fulani kwa sababu inalipa ndio yanasabibisha watu wanapasuliwa vichwa badala ya miguu. unajuaje kama by the time unamaliza masomo yako fani hiyo itakuwa inalipa bado. faida za kufanya fani unayoipenda ni pamoja na umakini kweny fani yenyewe na uvumilivu kama mambo yanachelewa ku tick, unataka kuniambia hamna madokta waliochoka, kila kitu ni wewe mwenyewe, wapo hata wahasibu waliochoka kwa taarifa yako.
   
 13. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #13
  Feb 25, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,630
  Likes Received: 1,990
  Trophy Points: 280
  wakipatikana watanzania asilimia 10 tu kama wewe mabadiliko ya kiuchumi yatakayopatikana lazima yawe makubwa. Ni watu wachache sana wenye fikra kama zako.
   
 14. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #14
  Feb 25, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,915
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180

  Tangu june last yr.....
   
 15. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #15
  Feb 25, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,915
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  Pamoja Madilu
   
 16. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #16
  Feb 25, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  mkuu nimemgongea ka like. kuna watz wengi sana wenye kuweza kuleta mabadiliko +ve tz tatizo ni swala la siasa kuingilia utaalamu. Wewe angalia sasa hivi swala la umeme, train, ATCL, mradi wa kigamboni, madini, matatizo ya maji etc haya yote ni mambo ya kutatuliwa na wanasayansi/engineers lakini hata siku humsikii engineer akiongela haya matatizo/solutions kwenye tv/radio... hehehe kila siku tunawaona wanasiasa tu mara leo january makamba, zitto, mnyika, mtoto wa mkulima, ngeleja, kilango na wote hawa wana degree za political science, human resources et al
   
 17. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #17
  Feb 25, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
  We dogo soma hiyo PCM ukimaliza ndyo utaamua usome nini kama si Engeneering, kwa sababu PCM inaweza kukupeleka kozi zingine nyingi nzuri kasoro Medicine.
   
 18. R

  Roland Bushumba Member

  #18
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asente mkuu.Pamoja sana!
   
 19. Fighter

  Fighter JF-Expert Member

  #19
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 611
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Mkuu kired una maana Engineering!

  Umegraduate lini? kwa nini huna kazi? ni PM please
   
 20. matungusha

  matungusha JF-Expert Member

  #20
  Feb 27, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Siku hizi telecom chaka mpango mzima civil & mechanical
   
Loading...