Je, DOWANS wameshalipwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, DOWANS wameshalipwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaHaki, Oct 20, 2011.

 1. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1
  Oct 20, 2011
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Wajumbe

  Naombeni ufafanuzi wenu.

  Kuna uvumi/uzushi/tetesi kwamba, kwa mujibu wa Sheria, baada ya Mahakama Kuu kusajili hukumu (tozo) ya uamuzi wa ICC dhidi ya TANESCO, ulioipa ushindi DOWANS, kwamba, kitendo cha Mahakama Kuu kuridhia tozo hiyo na kuisajili, ni sawa na kuamuru DOWANS ilipwe.

  Je, kuna ukweli wowote ndani ya hili?

  Pia, ninakumbuka, kuna mdau mmoja ndani ya JF alitoa ufafanuzi ambao unaashiria kwamba hakukuwa na hukumu kama hiyo iliyotolewa, na/au waliotoa hukumu hiyo hawakuwa na nguvu ya kisheria ya kutoa hukumu hiyo kutokana na wao wenyewe kutokuwa waajiriwa wa ICC. Nawaombeni ufafanuzi juu ya hili pia.

  Asanteni.

  ./Mwana wa Haki
   
 2. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Tanesco wanakata rufaa.
   
 3. Architect E.M

  Architect E.M JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 813
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 60
  mi nahisi itakua imeshalipwa, ndo maana hata makali ya mgao yamepungua (kwa tulioko arusha nadhani wengi mtakua mmejionea hili suala la kupungua kwa makali ya mgao wa umeme),,,kwasababu wangelipa bila kupunguza mgao, wananchi wangecharuka sana, soo wamefanya kupunguza mgao, wadanganyika tudanganyikem kumbe kwa chini dowans waleeeeee,,,, washalipwa,,,, ni mawazo yangu tu lakini wakuu, msije mkanishambulia hapa
   
 4. T

  Tujisenti JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2011
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Waliisha lipwa siku nyingiiiiiiiiiiiiiiiiii kupita usalama
   
 5. jebs2002

  jebs2002 JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 4,298
  Likes Received: 2,370
  Trophy Points: 280
  Watalipwa hela ya Rada inayokuja!!!!

  Hii nchi ina matatizo makubwa mno!
   
 6. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Yaani kwako wewe kigezo cha kulipwa ni kutokuwepo na mgao huko arusha kwenu. What a juvenile thinking!
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Nov 1, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,276
  Likes Received: 19,423
  Trophy Points: 280
  Ndio maana serikali haina pesa? wameshaanza mchakato wa kulipa? pesa zimeenda wapi na wakati kodi kila siku zinakatwa?
   
 8. ikizu

  ikizu JF-Expert Member

  #8
  Nov 1, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inabidi wanyongwe waliohusika na hiyo kashifa au tuwapeleke kwa kagame atajua nini cha kuwafanya
   
 9. ikizu

  ikizu JF-Expert Member

  #9
  Nov 1, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pesa zote zimeenda kwenye safari ya kikwete ya 318 tangu awe rais australia
   
 10. ikizu

  ikizu JF-Expert Member

  #10
  Nov 1, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Muulize mh Nkulo auNdio maana serikali haina pesa? wameshaanza mchakato wa kulipa? pesa zimeenda wapi na wakati kodi kila siku zinakatwa?
   
 11. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #11
  Nov 1, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Pesa nyingi imeenda India kuhudumia mawaziri na wabunge wanaoumwa.
   
 12. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #12
  Nov 1, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Sherehe za miaka 50 ya uhuru zimemaliza pesa.........sijui zile bili kule Apollo zitalipwa?
   
 13. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #13
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,276
  Likes Received: 19,423
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Wakati serikali ya Tanzania imekuwa katika hali ya ukata wa kifedha nchini na kusababisha baadhi ya miradi na malipo mbalimbali kushindwa kufanyika serikali hiyo hiyo imekamilisha ununuzi mwingine mkubwa wa tatu wa majengo nchini Marekani ndani ya miaka miwili. Serikali ya Tanzania imekamilisha ununuzi wa jengo kubwa huko New York ambalo limegharimu dola za Kimarekani milioni 24.5 karibu sawa na shilingi bilioni 41.6 za Tanzania.

  Jengo hilo jipya liitwalo Timekeeper Building (pichani) ni la ghorofa sita na lenye ukubwa wa futi 40,000 za mraba lipo jijini New York karibu na Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Jengo hilo limenunuliwa toka kampuni ya madalali wa majengo ya Amerimar ya huko Philadelphia jimbo la Pennsylvania. Kampuni ya Amerimar ilinunua jengo hilo mwaka 2005 kwa gharama ya dola milioni 15.45 kutoka kwa kampuni nyingine ya Mittman Associates.

  Jengo hilo ambalo tayari linawapangaji linatarajiwa kuwa makao makuu mapya ya Ubalozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa. Baadhi ya wapangaji wengine wa jengo hilo ni pamoja na Bombo Sports and Entertainment, Frederick Wildman & Sons na Ofisi za Caudalie Vinotherapy Spa.

  Kununuliwa kwa jengo hilo kumeifanya serikali ya Tanzania kununua majengo matatu ndani ya miaka miwili na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa ajira na uchumi wa Marekani. Mwaka 2009 serikali ya Tanzana ilinunua jengo jingine la Ubalozi wa Tanzania huko Washington DC ambalo lilifunguliwa na Rais Kikwete. Jengo hilo la Ubalozi huko DC nalo ni la ghorofa sita na liligharimu dola za Kimarekani milioni 10.415 sawa na shilingi bilioni 13.5

  Ununuzi mwingine wa majengo uliofanywa na Serikali ya Tanzania uliripotiwa mwezi Augusti mwaka huu ambapo huko huko New York serikali ya Tanzania ilinunua nyumba kwa ajili ya mwanadiplomasia wake na familia yake kwa gharama ya dola milioni 1.3 sawa na shilingi bilioni 2.2 hivi za Kitanzania. Dili la ununuzi huo lilikamilika mwezi Juni na kuridhiwa na serikali ya Marekani. Nyumba hiyo ina vyumba vitano, mabavu manne na vikolombwezo vingine kadhaa vya kufanya liwe maridadi kwa makazi ya mwanadiplomasia.

  Kwa miaka hiyo miwili Serikali ya Tanzania hivyo imetumia fedha za wananchi wa Tanzania zipatazo dola 36.215 karibu sawa na shilingi za Kitanzania bilioni 61. Pamoja na gharama hizo za awali serikali itatakiwa itumie kiasi kikubwa cha fedha kuyaendesha majengo hayo katika kiwango kinachokubalika ikiwa ni gharama ya maangalizi, usafi, na huduma mbalimbali kama maji na umeme. Jengo la Washington DC kwa mfano linakadiriwa kugharimu dola 367,593.54 kwa mwaka kuliendesha huku nyumba ya Balozi New York itatakiwa kulipiwa kodi ya jengo ya dola 22,000 hivi kwa mwaka. Gharama za kuendesha Jengo la New York kwa mwaka haijawa wazi.

  Ununuzi huu ambao unapita ununuzi wa rada ya kijeshi ambayo ilileta mgogoro na Uingereza unaweza kusababisha kashfa nyingine baadaye hasa endapo taarifa za kina nani walihusika katika ununuzi huo katika kuufanikisha na walipata nini zitajulikana na wananchi wa Tanzania. Toka mwanzo wa ununuzi wa jengo kubwa la NY tetesi za baadhi ya watu wazito katika serikali yetu (Ubalozi na nyumbani) kunufaika zilikuwa zinasikika kutoka vyanzo vya kuaminika.

  Jambo ambalo hata hivyo linaweza kuweka mgogoro mkubwa wa vipaumbele ni taarifa za wiki za karibuni kuwa serikali ya Tanzania iko katika hali mbaya ya kifedha hata kushindwa kufanya malipo mbalimbali yakiwemo yale ya mishahara ya watumishi wa umma.

  Mwezi Juni mwaka huu serikali ilifanya mabadiliko ya baadhi ya viwango vya mishahara na kupunguza baadhi ya mastahili ambayo iliyapandisha kuelekea uchaguzi mkuu mwaka jana. Taarifa zilizotolewa na Magazeti ya Serikali baadhi ya posho mbalimbali na mishahara ya watumishi ilibadilishwa kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma.

  Siku chache tu zilizopita Serikali imedai kuwa haina fedha za kutosha kuweza kuwapatia wanafunzi wa elimu ya juu mikopo ambayo walikuwa wamekubaliwa na hivyo kusababisha aidha baadhi ya wanafunzi kushindwa kuendelea na masomo au kuwa mzigo mkubwa kwa familia zao.

  Watu wengine ambao wamejikuta wakichelewesha mishahara yao au ikija pungufu ni pamoja na askari, walimu na watumishi wengine wa Halmashauri. Huko Geita Halmashauri ilitoa tangazo wiki iliyopita ambapo iliwataka watumishi kutambua kuwa baadhi yao mishahara yao itakuwa pungufu.

  Wakati huo huo serikali inaonekana kukosa fedha za kutimiza miradi mbalimbali. Akizungumza kwenye Kamati ya Kudumu ya Miundombinu ya Bunge Mwenyeketi wa Kamati hiyo Bw. Peter Serukamba alielezea kwa kirefu kushangazwa kwake na hali mbaya ya kifedha ambayo imesababisha baadhi ya miradi mbalimbali ya ujenzi kukwama huku wakandarasi wengine wakiacha kabisa kufanya kazi na wengine hata kutishia kuondoka.

  Bw. Serukamba alidai kuwa kutokana na hali ilivyo mbaya Kamati yake itajitahidi kutafuta ufumbuzi kwa kujaribu kuonana na Waziri wa Miundombinu na hata ikibidi kumuona Waziri Mkuu.

  Hata hivyo inaonekana viongozi na wananchi wengi bado hawajaona uhusiano wowote wa fedha zinazotumiwa kama hizo za bilioni zaidi ya 60 ambazo nchi maskini kama Tanzania inaingiza katika uchumi wa Marekani wakati wananchi wake wakihaha hata kupata mshahara wa ajira walizonazo.

  Hata hivyo serikali kwa upande wake imekuwa ikitetea manunuzi hayo ya majengo huko Marekani ikidai kuwa ni "uwekezaji" mzuri ambao baada ya muda utalipa na kurudisha faida. Baadhi ya wachunguzi wa mambo wameendelea kushangazwa na imani hiyo hasa kwa sababu baadhi ya kashfa za ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi zinahusu manunuzi mbalimbali katika balozi zetu huko nje.

  Katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kwa mwaka uliopita umeonesha kuwa Wizara ya Mambo ya Nje bado inakabiliwa na changamoto katika manunuzi ya umma. Kwa mujibu wa taarifa ya CAG kwa mwaka uliopita unaonesha kuwa Ubalozi wa Abu Dhabi kwa mfano ulitumia zaidi ya shilingi milioni 865 bila ya idhini ya Wizara (ushahidi haukutolewa kwa CAG kama ilikuwepo idhini hiyo). Kiasi kama hicho kilitumika pia kwenye Ubalozi wa Tanzania London, Uingereza huku Ubalozi wa Tanzania huko Moscow, Urusi nao ukitumia zaidi ya shilingi milioni 500 ya bajeti na bila idhini ya Wizara.

  Huko Kinshasa ukaguzi wa CAG ulionesha kuwa nyumba Na. 772 iliyoko mtaa wa Kacyiru ilikuwa inalipiwa na ubalozi kwa muda wa miezi saba wakati hakuna mtu anaishi. Ubalozi ulikuwa unalipia na walinzi vile vile. Hii yote ni pamoja na kashfa ya ununuzi wa jengo la Ubalozi huko Italia ambayo kesi yake inamhusu aliyekuwa Balozi wa Tanzania Prof. Mahalu.
  Ni kwa kiasi gani manunuzi ya majengo haya huko New York yatawasaidia wananchi wa Tanzania haijajulikana na kama fedha hizo kweli zinaweza kurudi kulinganishwa na kiasi cha uwekezaji unaotoka Marekani kuja Tanzania. Vyovyote vile ilivyo baadhi ya watu wanaweza kuhoji hekima ya serikali maskini kama ya kwetu tena katika wakati wa hali mbaya ya uchumi kuamua kuwekeza fedha nyingi namna hiyo huko Marekani wakati kiasi kama hicho kingeweza kusaidia sana katika kutatua tatizo la nishati, barabara, na hata elimu nchini.

  Mwandishi Wetu, New York, NY
   
 14. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #14
  Nov 2, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,992
  Likes Received: 2,650
  Trophy Points: 280
  Punda afe mzigo ufike.
   
 15. Pelekaroho

  Pelekaroho JF-Expert Member

  #15
  Nov 2, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,502
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  Kumbe tunapinga Dowans wakati kuna malipo mengine yanayofanyika ambayo huenda ni makubwa kuliko ya dowans, CCM bila ufisadi haiwezekani!
   
 16. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #16
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Jana niliagizwa kwenda Hazina kufuatilia jambo fulani la Kampuni yetu ya Uwakili. Nilipofika Ofisi ya Kamishna wa Bajeti pale Hazina na kujitambulisha, Katibu Muktasi ambaye labda hakusikia vizuri mahali nilipotoka, aliniambia:

  'Ndugu, malipo yenu ya Tunzo ya Jaji Mushi yataanza mwezi huu. Yatafanywa kupitia akaunti ya Caspian(Kampuni ya Rostam Aziz). Au kama mnabadilisha akaunti mseme kabisa ili tuyafanye kwenu Mawakili.'

  Nilikosa la kusema, nikajiondokea zangu nikiisikitikia Tanzania yangu. Naahidi kufuatilia suala hili kwa kina na kuliweka hapa jamvini.

  Picha ndio inakaribia kuanza.....
   
 17. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #17
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Nilijua tu.Tanzania ya Kikwete hiyo.Tunasubiri habari zaidi.Wanaharakati mpo?
   
 18. P

  Paul J Senior Member

  #18
  Dec 2, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani tuwaache walipe dowans wakati upatikanaji wa mishahara ya watumishi wa umma siku hizi ni sawa na makampuni ya huku uswazi ya magabachori na walimu tayari wameitangaza mgomo hapo january, kikubwa ni kufikisha ujumbe kama huu kwa wananchi ili waweze kuona nini vipaumbele vya serikali ya CCM, kwa wazee wa dar na makada wa ccm hili kwao si tatizo maana wengine waliishapata buku tano na pesa ikitoka mgawo kama kawaida.
   
 19. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #19
  Dec 2, 2011
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Mlikuwa mnacheza ngoma ya gamba, kwani imekwisha?
   
 20. k

  kajembe JF-Expert Member

  #20
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 755
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Katibu Muktasi anaonekana ni Mjuzi sana na alisema Mengi sana!
   
Loading...