Je? Chadema mko tayari kurudi CCM kama haya yatafanyika?

Mr.Mak

JF-Expert Member
Feb 23, 2011
2,841
1,102
Nimekuwa nikifuatilia sana malalamiko yanayotolewa na ima viongozi au wanachama hai na mfu kuhusu malalamiko mengi juu ya CCM. Sasa napenda kuuliza, iwapo kama CCM ikiwatimua mafisadi wote na ikafanya yale yote ambayo cdm mnalalamikia, je mtakuwa tayari wote kurudi CCM?
 
Nimekuwa nikifuatilia sana malalamiko yanayotolewa na ima viongozi au wanachama hai na mfu kuhusu malalamiko mengi juu ya CCM. Sasa napenda kuuliza, iwapo kama CCM ikiwatimua mafisadi wote na ikafanya yale yote ambayo cdm mnalalamikia, je mtakuwa tayari wote kurudi CCM?

Sina shika ndugu kama Mwembeyanga & Tabora list itapelekwa Keko basi wengi wanaweza kurudi CCM. Lakini umeshasoma list hizi mbili? ngumu sana!
 
Nimekuwa nikifuatilia sana malalamiko yanayotolewa na ima viongozi au wanachama hai na mfu kuhusu malalamiko mengi juu ya CCM. Sasa napenda kuuliza, iwapo kama CCM ikiwatimua mafisadi wote na ikafanya yale yote ambayo cdm mnalalamikia, je mtakuwa tayari wote kurudi CCM?

Ubavu huo CCM hawana, hivyo tusipoteze muda bure kujadili vitu visivyowezekana. Tazama hata maamuzi ya NEC hapo chini wapi walitaja siki 90? Ni usanii mtupu.

5. KUHUSU TATHMINI YA UCHAGUZI MKUU 2010

(d) Chama Cha Mapinduzi na Serikali zake kiongeze kasi ya mapambano dhidi ya viongozi na wanachama wanaojihusisha na rushwa. Aidha viongozi na wanachama wanaotuhumiwa kwa vitendo vya rushwa wajenge tabia ya kuwajibika wenyewe kwa maslahi ya Chama wasipofanya hivyo Chama kiwawajibishe kwa maslahi ya Chama na nchi
 
CCM na ‘gamba' la ufisadi
ban.blank.jpg


Bakari M. Mohamed

amka2.gif

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kinadai kimejivua gamba! Inawezekana kwa mtazamo wa propaganda ikadhaniwa ni kujivua gamba la nje na kubakisha gamba la ndani lenye ukale na ukuukuu uleule.
Ni kawaida ya vyama vya siasa vinavyokaa madarakani na kushika dola kwa muda mrefu kama CCM kupoteza mwelekeo wake wa asili kwa kumezwa na viongozi wenye uchu, tamaa na uroho wa kutumia siasa katika kujinufaisha kifisadi.
Hivi ndivyo CCM ilivyofanya tangu pale ilipopoteza mwelekeo wa kujenga jamii ya watu waliyo sawa na huru. CCM, kama chama kilichofisidika, kilianza kupotea njia yake ya ‘ujamaa na kujitegemea' baada ya kuacha mapendekezo ya chama yaliyotolewa wakati chama hicho kilipokuwa kinatimiza miaka kumi, yaani mwaka 1987.
Tathmini ya chama ilionyesha wazi juu ya kupoteza mwelekeo katika kusimamia ujenzi wa jamii isiyokuwa na dhuluma, vitisho, uonevu na aina zote za ufisadi.
Kwa ujumla, viongozi waandamizi wa CCM walimezwa na au kuwekwa ‘mtu-kati' na mafisadi waliojipenyeza ndani ya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) na hata kuathiri maamuzi na utendaji wa chama. CCM, badala ya kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi kama ilivyodhaniwa kwenye falsafa ya chama, kiligeuzwa chama cha wafanyabiashara matajiri na mafisadi! Huu umekuwa mwendo wa siasa za ndani ya CCM tangu pale chama hicho kilipoliua Azimio la Arusha na kutupilia mbali maadili ya uongozi wa siasa.
Siasa imekuwa ikitumiwa na baadhi ya mafisadi kwenye mduara wa ndani wa CCM (CC na NEC) katika kufanikisha mipango ya kimafia na kushadidi kwa vitendo vya ujambazi wa kiserikali. Miongoni mwa mambo anuai yanayoanishwa kwenye gamba la ufisadi lililovishwa kwenye utendaji wa CCM ni: ufisadi wa kimfumo; ufisadi wa ndani ya mfumo; ujambazi wa kiserikali; kunyonga haki ya kukosoa na kukosolewa; na kuwaacha wafanyabiashara waendeshe chama kama kampuni. CCM imefanywa kama "shamba la bibi" kwa wafanyabiashara mafisadi kuwekeza mitaji yao inayotokana na fedha haramu na au fedha chafu!
Ufisadi wa kimfumo umeifanya CCM inuke ufisadi kuanzia kada za chini (kwenye mashina, matawi na kata), wilaya, mikoa hadi taifa. Uongozi wa CCM, baada ya kuvurugwa kwa maadili ya siasa, umekuwa ukitolewa kwa ununuzi wa kura na wapiga kura na hata wakati mwingine kwa matumizi ya hila, ghiliba, uonevu na vitisho! Mafisadi wenye satwa (uwezo na nguvu) ya fedha wamekuwa wakipanga nani awe kiongozi na awatumikie mafisadi kwenye mfumo na ndani ya mfumo.
Mfumo wa chama wa ndani (CC), katikati (NEC) na nje (wanachama wa kawaida) umefanywa kuwatumikia watu wachache wenye nguvu ya kuathiri maamuzi vile watakavyo kwa kuwa sehemu kubwa ya viongozi wamerogwa na kurogeka kwa fedha chafu inayotumika katika kuendesha siasa za kifisadi kwa manufaa ya ufisadi na mtandao wa ufisadi wa kimfumo. Hata hivyo, ufisadi wa ndani ya mfumo umeenea kwenye mifumo inayounda mfumo mzima wa CCM – uongozi wa kifisadi unaofanyakazi kwa maslahi ya viongozi mafisadi wa ndani ya mfumo – pamoja na msonge wa utawala wa chama.
Ndani ya CCM kumevamiwa na watu wenye tamaa ya kushika uongozi na au madaraka ya kuongoza hata kwa kuvuruga mfumo wa kuongoza! Ni rahisi sana ndani ya CCM kuona watu wakifanya urafiki wa moja kwa moja na wafanyabiashara wenye mafungamano ya kifisadi ili chama kishinde! CCM imekuwa ikitumia fedha nyingi na chafu kwenye chaguzi zake katika kuhakikisha kwamba viongozi wenye dhamira ya kuwatumikia mafisadi wanapata nafasi ya kushika nafasi hizo kwa manufaa ya kifisadi na mfumo wa ndani wa kifisadi.
Chama kimefanywa kama ‘genge' la watu wachache wenye maamuzi ya kuendesha nchi kwa kutumia nguvu ya uwezo inayotokana na mafungamano ya kifisadi baina ya viongozi waandamizi wa CCM na wafanyabiashara matajiri na mafisadi papa wenye nia ya kuwatumia kwa faida ya mtandao.
Hapa ndipo unapoweza kuona jinsi wafanyabiashara wenye kumiliki siasa za kifisadi walivyoweza kupata nafasi hata za kutumikia CCM kama viongozi waandamizi, kama vile kuwa mweka hazina wa CCM taifa na au meneja wa kampeni wa mgombea wa urais wa CCM (2005).
CCM isifanye mzaha na hali ya ufisadi wa kimfumo na wa ndani ya mfumo uliopo ndani yake. Kwa kuwa mtandao wake umeenea kwenye ngazi zote na waliyefanyakazi ya kuubuni, kuutengeneza, kuusimamia na kuuendeleza mtandao wa kifisadi ndani ya CCM wana nguvu nyingi na mbinu za mikakati; lazima CCM ijichunguze kutokea nje na ifanyekazi ya ziada kuanzia ndani!
Mwenyekiti wa CCM taifa lazima ajivue au avuliwe ‘gamba' la uswahiba alionalo baina yake na mafisadi ambao wengi wao ndio waliomuunga mkono na kumpatia usaidizi wa hali na mali kwenye harakati zake za kugombea uongozi wa nchi na chama.
Uswahiba uliopo kwenye mzingo wa ndani wa CCM (japokuwa CC imepanguliwa) unaweza kuchukua sura mpya ya kuwatumia wajumbe na viongozi wapya kwa utumizi wa mbinu zile zile zilizotumika kuingiza biashara na hatimaye kukifanya chama kuwa kampuni la wenye hisa mafisadi wanaotumia ufisadi kama mtaji wa kuendeleza maslahi ya kifisadi.
Wengi wa viongozi wa iliyokuwa CC walikuwa na uswahiba wa moja kwa moja na baadhi ya mafisadi ‘papa' na hata wakati mwingine mafisadi hao waliweza kuathiri maamuzi ya kushindwa kutenganisha bishara na siasa!
Haikuanza jana kusemwa majukwaani na kuandikwa na waandishi, wapembuzi na wachokonozi kwamba CCM ni chama cha mafisadi kwa vile maamuzi yake yanaathiriwa na mafisadi na au mtandao wa kifisadi uliyojikita kindakindaki kwenye CCM na NEC ya CCM.
Viongozi wa CCM waliziba masikio kwa nta na kuendelea na mwendo mdundo hadi pale walipozidiwa na kuona chama chao kinapoteza ushawishi wake kwa wananchi na hata wananchi kupoteza matumaini na kutafuta vyama mbadala.
Kutokana na kukomaa kwa ufisadi wa kimfumo na wa ndani ya mfumo, CCM ilikuwa inafanya ujambazi wa kiserikali kwa kuwaruhusu mafisadi kuwaibia wananchi kwa mgongo wa kiserikali kwa serikali kuridhia na au kusimamia kuvunjwa kwa sheria na kanuni mbalimbali kwa maslahi ya mafisadi na mitandano ya kifisadi.
Mafisadi wamekuwa wakitumia nafasi ya serikali dhaifu kufanikisha mipango yao nyeti katika kujinufaisha na kuunufaisha mtandao wa kifisadi unaounganisha nguvu za mafisadi waliyo ndani ya CCM na wale wa nje (wanaowatumia mafisadi waliyo ndani).
Kwa jinsi hii, wananchi (wakulima na wafanyakazi) walalahoi wamekuwa wakiminywa na kukamuliwa na mafisadi kwenye nyanja zote za uchumi-jamii na jamii-siasa huku CCM ikibariki dhuluma na hata wakati mwingine kutumia vyombo vya dola kusimamia dhuluma inayofanywa na mafisadi!
CCM imefikia hatua mbaya sana ya ufisadi hata kusahau dhima yake ya kuwatetea walalahoi wanaodhulumiwa haki na stahili zao za kazi (ujira na mishahara) zenye kuzingatia hali-halisi; na wakulima kupunjwa bei na au kulanguliwa na walanguzi ikiwemo serikali!
Gamba la ufisadi kwa CCM ni kule kujivisha uwakala wa utawandawazi na ukoloni mamboleo huku chama hicho kikiwachuuza wananchi kwa kunadi kuwaletea maisha bora ilhali maisha yanazidi kuwa magumu na yenye kukatisha tamaa!
Hivi ndivyo CCM ilivyojivika gamba na hata kwa ngozi hiyo ngumu kukomaa na kuwa kama gamba la kobe au kasa ambalo kuvuka kwake ni kifo cha kobe au kasa! Hakika, CCM ina gamba linalochukiza na kunyong'onyesha.
Hata kama baadhi ya wana CCM wameanza kusherehekea na au kushangilia kujivua gamba kwa chama hicho, bado kuna safari ndefu ya kukamilisha mchakato wa kujaribu kurudisha imani ya wananchi iliyoyeyuka kama theluji.
Kama kweli gamba lililovuliwa na CCM ni ufisadi tuna kila sababu ya kudhani kwamba chama hicho kimejengwa kwenye mihimili ya ufisadi wa kimfumo na wa ndani ya mfumo kwa vile wale wanaopewa nafasi ya kujiondoa wenyewe kwenye nafasi za uongozi wa CCM wanapatikana kwenye iliyokuwa CC na wale waliyomo ndani ya NEC.
Nani asiyefahamu kwamba sehemu kubwa ya viongozi na au wajumbe wa CC na NEC (ya sasa na ya zamani) kwa nanma moja na au nyingine wanahusika kwa njia moja au nyingine na mitandano ya ufisadi? Kama jibu ni ndiyo; je, kuwataka wajiondoe wenyewe ilhali chama kinawafahamu si mzaha?
Inawezekana kabisa kauli ya viongozi wa CCM, mwenyekiti, makamu mwenyekiti, katibu mkuu na viongozi wengine juu ya kuwataka mafisadi wajiondoe wenyewe ni mchezo wa kuigiza na au kujaribu kumtaka paka ajifunge kengele!
Huu ni utani wa kisiasa na inaonyesha kwamba uongozi wa CCM hauna dhamira ya kweli na ya makusudi kushughulikia suala la ufisadi ndani ya chama hicho.
Ilitegemewa chama kingechukua hatua madhubuti na kuwang'oa mafisadi ili kitoe fundisho la kihistoria!
Haikuwa na haitokuwa kwa vile CCM ina mtandao wa ndani na ule wa nje unaofungamana moja kwa moja na mafisadi wenye nguvu zinazojionyesha kwenye taathira ya maamuzi yote mazito na au magumu ya chama kuhusiana na suala la ufisadi.
Kigugumizi cha mwenyekiti wa CCM taifa kinatokana na ukweli kwamba miongoni mwa wanaodhaniwa ni mafisadi wamo watu waliomsaidia katika kupata nafasi ya kuongoza.
Vilevile wapo wale yeye (kama mwenyekiti wa CCM taifa) aliyewanandi mbele ya wapiga kura kwamba ni watu ‘safi' na hata yaliyowakuta ni ‘ajali ya kisiasa'!
Ajali ya kisiasa imefanywa mtaji kwa vile kwa sehemu kubwa hakuna mtu anayeweza kusimama na kuwataja mafisadi wakubwa waliyemo ndani ya CCM hata kama dalili na ushahidi wa moja kwa moja unatoa nafasi ya watu hao kutajwa na hatimaye kufukuzwa na CCM.
Kama CCM ingeliona hili ingelibidi kuchukua hatua za kuwafukuza mmoja baada ya mwingine na au hata kuwachukulia hatua za kisheria kwa vile wamekifanya chama kupoteza haiba ya kisiasa mbele ya wananchi.
CCM imebakisha gamba lake kwa vile ina nafasi ya ufisadi unaochukua sura ya gamba jipya kwenye mfumo wa zamani!
Kwa kutumia falsafa, tunaweza kuuliza swali hili; Nani awezaje kumfunga paka kengele? Ikiwa kiongozi wa serikali ya CCM amewahi kutamka hadharani kwamba, "wala rushwa anawafahamu; isipokuwa anawapa muda wajirekebishe." Na vilevile, ushahidi wa wazi unaonesha kwamba wale majambazi wa fedha za akaunti ya madeni ya nje (EPA) walipewa nafasi warudishe fedha walizoiba na au kukwapua Benki Kuu! Gamba la ufisadi linaweza kuvuliwa na chama sampuli hii ya CCM?
Uongozi wa CCM uliojibakisha na kudai wamejivua gamba wana jambo gani la kujivunia juu ya uvuaji wa gamba wa kisanii walioufanya Dodoma? Au tuseme kwamba wamefunika kawa ili mwanaharamu apite?
Hawajui kwamba hawatahukumiwa kwa maneno yao bali watapimwa kwa matendo yao juu ya dhamira ya kupambana na mafisadi.
Na kwa kuwa ufisadi umeshachukua msamiati wa siasa katika Tanzania kuna kila sababu ya CCM kuwa chama cha mafisadi hadi pale uongozi wa chama hicho utakapochukua hatua kali dhidi ya mafisadi wanaotamba kukisambaratisha chama hicho.
Kama wamechukua uamuzi baada ya utafiti wa wataalamu (wasomi) makini na bobezi kwenye kutafiti matatizo ya kudumaa na kukosa mvuto kwa vyama vya siasa; basi kuna kila sababu ya kudhani kwamba ushauri wa kitaalamu uliotolewa hauna mashiko kwa wakati huu.
Nadhani ushauri muhimu kwa CCM ulikuwa ni kuifumua CCM kuanzia kada za kati ambazo nyingi (wilaya na mikoa) zimeundwa kwa utashi wa mafisadi katika kufanikisha malengo ya ufisadi wa kimfumo katika kujenga mtandao kuanzia wilayani na mikoani. Viongozi wengi wa kada za wilaya na mikoa ni wale waliopewa fedha za kampeni na kufanyiwa kampeni na mafisadi katika kupata uungwaji mkono kwenye kupitisha maamuzi yanayohitaji maamuzi ya wengi.
Kama kujivua gamba ni kuivuruga CC na NEC ya CCM ilhali mtandao wa wilaya na mikoa na wajumbe wake wanaotokana na mfumo wa kifisadi utabaki kama ulivyotengenezwa na kusimamiwa mwaka 2007 na kama ulivyopangwa mwaka 2002 kuna kila sababu ya kudhani kwamba CCM inachimba kaburi lake na kutamani kujizika yenyewe.
Hakuna awezaye kuinusuru CCM kama inatamani kujimaliza yenyewe isipokuwa utashi wa kweli wa viongozi wake katika kurudi kwenye asili ya chama (political roots). CCM itambue kwamba ni chama cha wakulima na wafanyakazi walalahoi wenye kutamani ujamaa na kujitegemea kama njia ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru.
Wananchi wa Tanzania wanahitaji uhuru! Uhuru wa kweli wa kujitawala kiuchumi, kijamii na kisiasa kwa haki, usawa na uadilifu. Wananchi wa Tanzania wanatamani kufaidi matunda ya uhuru wa nchi yao; na kwa jinsi hiyo, CCM ilidhaniwa kuwa ni chama cha kuleta manufaa kwa maisha ya wananchi wengi maskini wa Tanzania. CCM haikudhaniwa kingekuwa chama kinachokumbatia mafisadi wanaonyonya rasilimali za nchi na au kupora na kukwapua bila huruma na insafu.
Mwisho wa makala ni rai kwa wananchi na wanachama wa CCM; kujivua gamba kwa CCM kusiwafanye msahau na au mjisahau katika harakati zenu za kudai Katiba Mpya itakayoondoa aina zote za dhuluma, vitisho, uonevu na ufisadi unaofanywa na mtu, kundi la watu na au chama cha siasa kinachosimamia maslahi ya mafisadi. Ni wakati muafaka wa kutumia nafasi iliyotolewa ya kujenga ujamaa wa nchi yetu. Kila mwananchi wa Tanzania ana wajibu wake; na tutimize wajibu huo bila ya ajizi. Mungu ibariki Tanzania!
 
CCM inajiandalia anguko jingine!
ban.tuendako.jpg


Absalom Kibanda

amka2.gif

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kwa mara nyingine tena kimechafua hali ya hewa kisiasa nchini, safari hii kikija na kaulimbiu tata ya kujivua gamba iliyoasisiwa, ikaratibiwa (Waswahili wanasema – kimkandamkanda) na kuendeshwa kimafia na Mwenyekiti wake wa taifa, Rais Jakaya Kikwete.
Sina shaka hata kidogo kwamba, wasomaji wazuri wa gazeti hili, watakuwa wamepata picha halisi ya kile kilichotokea mjini Dodoma hivi karibuni, kikianzia katika kikao cha Kamati Kuu (CC) na baadaye Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC).
Mchezo. Nauita mchezo kwa kuwa hauna tija wala matokeo yoyote ya mabadiliko ya kimfumo au kifalsafa, ulianza katika Kamati Kuu iliyoketi kwa siku mbili na kuhitimishwa na hatua ya Kikwete kumtumia mmoja wa wanasiasa wanaoheshimika, Abdulrahman Kinana kubeba ajenda yake.
Ajenda katika mchezo huo wa kuigiza na uliokuwa umepangwa mapema kabisa, ilikuwa ni pendekezo la kuwalazimisha wajumbe wote wa sekretarieti na kamati kuu ya chama hicho kujiuzulu nafasi zao.
Maelezo yasiyo ya kisayansi yaliyotolewa na ambayo tayari yalikuwa mitaani wiki mbili kabla ya kikao chenyewe yalikuwa na maelezo dhaifu: Kwamba wajumbe wa vikao hivyo viwili walikuwa wameshindwa kumsaidia Mwenyekiti wao, Rais Kikwete.
Watu wenye akili zao ndani ya kikao hicho na nje, walijua fika kwamba, walengwa wakuu katika ajenda hiyo walikuwa ni aliyekuwa Katibu Mkuu, Yusufu Makamba, Rostam Aziz na Andrew Chenge.
Kwa muda mrefu hoja dhidi ya Makamba kwamba alikuwa ameshindwa kazi, ilikuwa mtaani na yeye mwenyewe mara kadhaa alishapata kujaribu bila mafanikio kuitolea ufafanuzi.
Kwa upande wao, Chenge na Rostam walitakiwa kutemwa, lengo la kwanza likiwa ni kuifanya ile kauli aliyoitoa Rais Kikwete, Februari 5, mwaka huu wakati chama hicho kikisherehekea miaka 34 ya kuzaliwa kwake, alipotumia kaulimbiu ya kujivua gamba ionekane ilikuwa halisi na yenye mwelekeo madhubuti.
Panga lililowalenga wanasiasa hao watatu, kwa bahati mbaya au kwa kupangwa lilijikuta likimkumba pia Bernard Membe, mmoja wa wanasiasa waliokuwa wakiunda sekretarieti, akiwa Mkuu wa Idara ya Siasa na Mambo ya Nje na mjumbe pia wa Kamati Kuu.
Hatua ya Rais Kikwete kutolirudisha jina lake ili lipigiwe kura tena wakati alipokuwa akipendekeza majina mapya ya wajumbe wa CC baada ya ile ya kwanza kujiuzulu, bado imeacha maswali mengi.
Wako wanaoamini kwamba, msingi wa hatua hiyo ya Rais Kikwete ilikuwa ni kuwaweka kando wanasiasa wote ambao tayari walikuwa wameshaanza kukigawa chama katika misingi ya makundi ya urais wa mwaka 2015.
Jina la Membe kama yalivyo majina ya wanasiasa wengine kama Profesa Mark Mwandosya, Emmanuel Nchimbi, Edward Lowassa, Samuel Sitta, Frederick Sumaye na Mathias Chikawe, yanahusishwa na urais na hakuna hata mmoja miongoni mwao ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu.
Ukiliacha hilo na kurejea katika hoja ya ufisadi, ni wazi kwamba tuhuma dhidi ya Chenge na Rostam zilikuwa ni moja ya majibu rahisi yaliyokuwa yakificha maelezo halisi yanayokihusisha chama hicho na swali gumu linaloitaka CCM ieleze kwa kina ni kwa namna gani dhana hiyo nzima ya kujivua gamba itamaliza wingu hilo linalokitafuna chama hicho na serikali yake kwa miaka mingi sasa.
Ni jambo la kutia shaka sana kwamba wakati kina Kikwete, Kinana na wenzao wakikuna vichwa kutafuta majibu ya haraka haraka ya kukinusuru chama chao na hatima iliyo wazi ya anguko lake linalokuja kwa kujongea kadiri muda unavyozidi kusonga mbele, walisahau kabisa kuzigeuza fikra ili zimuelekee mwenyekiti binafsi na kumchambua ni kwa kiwango gani, yeye mwenyewe alikuwa ameshindwa kufanya kazi na sekretarieti na kamati kuu yake.
Kwa namna ninavyomfahamu Kinana, ninao uhakika wa asilimia 100 kwamba wakati wote walipokuwa wakijadiliana na wenzake ndani ya chama chake kuhusu hatua wanazopaswa kuzichukua, ukweli kwamba moja ya matatizo makubwa yanayokikwamisha chama hicho ni Kikwete mwenyewe aliliona.
Tunapaswa kuomba Mungu katika siku isiyo na jina huko tuendako, tuje kumsikia Kinana kwa maneno yake mwenyewe akikiri kwamba tatizo la kwanza na la msingi ambalo limekikwamisha chama chao na hususan serikali ya CCM katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ni mwenyekiti wake, Rais Kikwete.
Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba, leo hii unapoandika maneno ya namna hii, yenye mwelekeo wa kumsema vibaya Kikwete, marafiki zake na wale wataalamu wa masuala ya intelijensia, wanaofanya mambo yao wakitumia kanuni moja tu ya hesabu za kujumlisha na mbinu ya kuoteshwa majibu ya matatizo ya taifa hili huwa wepesi kuzusha na kutunga uongo kwamba fulani ametumwa na fulani ili amchafue fulani.
Wazushi hawa ambao baadhi yao ni makachero wanaopaswa kujua mapana na marefu ya kufanya upembuzi yakinifu kabla ya kuwahadaa viongozi wetu wakuu ndio ambao walikuwa nyuma ya ajenda nzima ya CCM kujivua gamba.
Ni jambo la kusikitisha sana kwamba wazushi hao ambao leo hii wamefikia hatua ya kuwa ndiyo ‘think tanks' ndani ya CCM na serikali yake wakiongozwa na kachero mmoja mwandamizi aliyeingia katika siasa, ndio waliokuwa pia nyuma ya hoja ya kuwapa siku 90 baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi walio wajumbe wa NEC ambao kwa muda mrefu majina yao yamechafuka.
Ni wazushi hao ambao kwa kujua au kutokujua baada ya hoja yao hiyo ya kuwaandama watuhumiwa wachache wa ufisadi kuonekana ikipwaya na hata kufikia hatua ya kushambuliwa katika vyombo vya habari na ndani ya vyama vya siasa, wameanza kupindua maneno.
Sasa wazushi hao wanayatuhumu baadhi ya magazeti, likiwamo hili kwamba eti yanatumiwa na mafisadi ili kumchafua Rais Kikwete.
Kwa kauli hiyo hiyo, wazushi hao wamemlisha ujinga wao, Katibu wa Idara ya Uenezi na Itikadi wa CCM, Nape Nnauye, ambaye naye hata kabla ya kufikiri na kuchanganua mambo ameanza kupita akikishambulia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Katibu Mkuu wake, Dk. Willibrod Slaa kwa kutumiwa na mafisadi eti kumchafua Rais Kikwete.
Nape na wazushi wenzake hao wanasahau kwamba, msimamo wa magazeti wanayoyashambulia kama ‘Tanzania Daima' kuhusu Kikwete na ufisadi wanaojaribu kuufanyia usanii hata kabla hawajabuni nadharia yao ya kujivua gamba haujapata kubadilika na utaendelea kubakia na kuwa ule ule siku zote.
Hivi Nape na makachero wengine wanaoasisi michezo ya kisiasa ndani ya CCM wanapojaribu kuitumia dhana ya kujivua gamba kama mkakati wa kuzima kishindo cha mabadiliko kinacholikumba taifa leo wanadhani Watanzania hawajui kwa mapana na marefu ukweli wote kuhusu ufisadi hapa nchini?
Hivi CCM hii inayojaribu leo hii kujiokoa kwa gharama ya kusalitiana, kulana wenyewe kwa wenyewe kisiasa (political cannibalism) na kutoana kafara hata katika kashfa kama za Kagoda na Richmond haijui kuwa tuko wengi tunaojua kuwa ushiriki wake ni mpana zaidi na unawagusa wakubwa wengi zaidi ndani ya chama hicho tawala na serikali yake?
Itakuwa ni dharau mbaya dhidi ya Dk. Slaa, CHADEMA na Tanzania Daima iwapo wanasiasa wa aina ya Nape na wenzao watafikiri kwamba wanaweza kutujumuisha katika kundi la watu wanaoyashangilia mageuzi hewa yanayoendelea kufanywa ndani ya CCM leo kwa lengo la kuwahadaa wananchi.
Litakuwa ni jambo la kututia aibu iwapo sisi wa Tanzania Daima pia tutaingizwa kichwa kichwa katika sanaa mpya ya CCM ya ‘kujivua gamba' hata tukaisahau na kuipuuza orodha ya Mwembe Yanga ya watuhumiwa 11 wa ufisadi iliyosomwa na Dk. Slaa, Septemba 15, mwaka 2007.
Yatakuwa ni matusi dhidi ya uwezo wetu wa kufikiri iwapo CCM itafikiri kwamba hiki kiinimacho chao kipya wanachokifanya sasa kinaweza kikatufanya tuweke kando madai yenye harufu ya ukweli yatakaoendelea kuitafuna Serikali ya Awamu ya Nne kwamba iliingia madarakani kwa ushawishi wa nguvu ya fedha, ilipatikana kutoka katika Akauti ya EPA na kupitia katika akaunti ya Kagoda.
Itakuwa ni fedheha kwetu iwapo tutaupuuza ukweli ulio dhahiri kwamba tatizo la ufisadi ndani ya CCM na serikali yake haliwezi kumalizwa kwa kuwaruhusu viongozi na makada wa chama hicho wahujumiane kisiasa kwa malengo ya kusaka madaraka, tena kwa gharama za kufifisha upepo wa mabadiliko ya kisiasa ambao kwa sasa unaongozwa na CHADEMA.
Rais Kikwete na timu yake mpya ya uongozi ya CCM wanapaswa kutambua kuwa kama walivyokwama wakati walipojaribu kuinunua ajenda ya ufisadi kwa njia mbalimbali kupitia bungeni, mahakamani, TAKUKURU na kwingineko ndivyo watakavyokwama pia safari hii wanapojaribu kupanda farasi mpya waliyempachika jina la kujivua gamba. Kwa sababu hiyo, wanapaswa kuanza kutambua mapema kabisa kwamba, maamuzi waliyofanya Dodoma hivi karibuni, japokuwa leo hii yanashangiliwa na wengi ndani na nje ya chama hicho ni kaburi walilojichimbia wenyewe. Nyuma ya mabadiliko hayo ya CCM Dodoma, naona kuzaliwa Maalim Seif mpya. Naona kuibuka kwa Jacob Zuma mwingine na kwa hakika tunaweza tukampata Raila Odinga wetu. Tusubiri tuone. Huko ndiko TUENDAKO.
 
Nnauye anavaa gamba lililovuliwa na wazee!
ban.blank.jpg


Barnabas Maro

amka2.gif

"WALA watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuuu; na kama wakitia, vile viriba hupasuka , divai ikamwagika, na viriba vikaharibika. Bali hutia divai mpya katika viriba vipya, vikahifadhika vyote" (Mt. 9:17).
Kijana wangu aitwaye Nape Nnauye ambaye sasa amepewa wadhifa wa kuwa Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, anasema orodha mpya ya mafisadi iliyotangazwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa mjini Tabora majuzi ni ‘sawa na mchezo wa kuigiza'. Nimtahadharishe Nnauye kuwa akiingilia lisilomhusu atapata lisilomridhi; tena maji asiyoyafika hajui kina chake.
Mwaka 2007 wakati Dk. Willibrod Slaa alipotangaza orodha ya mafisadi 11 pale Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam, CCM wakiongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wao, Yusuf Makamba, waliibeza orodha ile wakimwambia Slaa aende polisi kama ana ushahidi.
Ngoma ileile aliyocheza Makamba ndiyo anayocheza sasa Nnauye; ila anajikanganya kwa kukataa na wakati huohuo anakubali asemayo Slaa.
Nnauye anasema tangazo la Slaa halina lolote katika mchakato wa kuwang'oa mafisadi ndani ya CCM na kwamba wanachofanya (CHADEMA) ni sawa na kuwasha moto juu ya petroli. Akaendelea: "Tunajua mipango yao ya kujaribu kufanya kampeni za kuchafua watu wasafi ndani ya CCM akiwamo rais na familia yake".
Kwa kuwa Nnauye amevishwa ‘gamba' la wazee, naye ghafla amezeeka hata kumbukumbu zimemtoka kwa kudai eti CHADEMA wamepanga kutumia baadhi ya vyama vya upinzani, viongozi wa dini na baadhi ya vyombo vya habari na waandishi ili kuwachafua makada wa CCM, Rais Kikwete na familia yake.
Eti mkakati huo hautaweza kuidhuru CCM wala kuifanya iachane na mchakato wa kuwashughulikia mafisadi ndani ya CCM. Anakataa nini na anakubali nini?
Kuhusu madai yake kwamba CHADEMA inavitumia vyama vingine vya upinzani, viongozi wa dini, baadhi ya vyombo vya habari na waandishi, Nnauye amesahau ndoa ya CCM na CUF? Barazani CUF ni serikali na uani ni ‘wapinzani'. Yawezekana kuchanganya sukari na magadi katika chai na ikafaa kunywewa? Ni siri gani itakayozungumzwa na wapinzani isiifikie CCM?
Mara ngapi Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, ameshirikiana na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia kuishambulia CHADEMA na viongozi wake? Mara ngapi viongozi wa dini nao wameingizwa kwenye mkumbo wa kuishambulia CHADEMA wakidai kuwa eti maandamano na mikutano yake inahatarisha amani ya nchi?
Nnauye anasahau kuwa hivi karibuni vikao vya NEC na Kamati Kuu ya CCM vilifanya mageuzi ya uongozi na kupitisha maazimio yenye lengo la kuwaondoa wenye tuhuma nzito za ufisadi na ukosefu wa maadili ili kujivua ‘gamba'.
Katika orodha mpya ya viongozi, Nnauye ni Katibu wa Uenezi na Itikadi, hivyo kavishwa ‘gamba' lililoachwa na wazee wake!
Tangu mwaka 2007 viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakiilaumu CCM kwa kuwakumbatia mafisadi. Ingawa watuhumiwa walikanusha kwa mapana na marefu, sasa ndio walio mahakamani, wamejiuzulu na wengine (wanaofahamika lakini hawatajwi), wamepewa miezi mitatu wajiondoe wenyewe katika chama. Isijekuwa kisu kibutu hakichinji kuku!
Kwa upande wake, Dk. Slaa amemwambia Rais Kikwete kwamba kama watuhumiwa hao watatajwa na kuchukuliwa hatua ikiwamo kuondolewa kwenye nafasi zao za uongozi, katika chama na ubunge, ndipo dhana ya kujivua ‘gamba' itakapokuwa na mantiki, vinginevyo ni usanii mwingine.
Dk. Slaa anasema Watanzania wanataka kuona fedha zilizoibwa na mafisadi zinarejeshwa na wahusika wafikishwe mahakamani badala ya kushikilia maneno matupu ya chama kujivua ‘gamba'.
Zi'wapi fedha za EPA, Kagoda, Benki Kuu ya Tanzania, Meremeta na Tangold?
Mbona mpaka sasa serikali inashindwa kuchukua uamuzi dhidi ya wahusika? Je, waliorejesha fedha za EPA ni kina nani na kwa nini inakuwa ‘haramu' kuwataja; tena hawajafikishwa mbele ya sheria?
Si kweli kwamba miongoni mwao ni viongozi wakuu wa serikali? Kama ni hivyo, basi CCM kujivua ‘gamba' hakutoshi kwani kinachotakiwa ni kufyonzwa damu yote na kuwekewa nyingine isiyokuwa na virusi vya ufisadi na kiwewe cha kutotaka kuwaachia wengine (wapinzani) madaraka.
Usanii uliofanywa na NEC na Kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma ni sawa na "kutia kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu, maana kile kilichotiwa huondoa kipande cha lile vazi, na pale palipotatuka huzidi." (Mt. 9:16).
Nape Nnauye ni kiraka cha nguo mpya katika nguo mbovu; tena ni divai mpya katika kiriba kilichochoka. Amesahau alivyosakamwa na baadhi ya viongozi alipozungumzia ufisadi wa ujenzi wa jengo la Umoja wa Vijana wa CCM? Hakumbuki jinsi mmoja wa watuhumiwa alivyokataa kuupokea mkono wake na kumtamkia wazi kuwa "kijana wewe nakuchukia!" Kama Nnauye anadhani amesimama, aangalie asianguke!


h.sep3.gif
 
Safisha safisha haitaishia

Monday, 18 April 2011 11:35 newsroom


chiligati.jpg
"Safisha safisha haitaishia Kamati Kuu na Sekretarieti..uchaguzi ujao mafisadi hawatapata nafasi ya kupitishwa : Chiligati

Kupeng'e, hivi CCM wameshatoa definition ya neno 'ufisadi'? Hii itasaidia kujua ni watu wa aina gani ambao "hawatapata nafasi ya kupitishwa".
 
Hili swali linafanana na hili: Shetani akiokoka, mtafanya nini na makanisa? polisi watafnya kazi gani?, magereza mtayageuza kuwa kumbi za disco? watu wangapi watakosa kazi? je, mnataka shetani aokoke aache kudanganya watu?
 
Hili swali linafanana na hili: Shetani akiokoka, mtafanya nini na makanisa? polisi watafnya kazi gani?, magereza mtayageuza kuwa kumbi za disco? watu wangapi watakosa kazi? je, mnataka shetani aokoke aache kudanganya watu?
Uuuuuwi mzee umeuaaaaa!!!
 
Nimekuwa nikifuatilia sana malalamiko yanayotolewa na ima viongozi au wanachama hai na mfu kuhusu malalamiko mengi juu ya CCM. Sasa napenda kuuliza, iwapo kama CCM ikiwatimua mafisadi wote na ikafanya yale yote ambayo cdm mnalalamikia, je mtakuwa tayari wote kurudi CCM?

Baada ya hapo ndugu utarajie maendeleo kurudi nyuma kuliko tulipo sasa, unajua lazima kuwe na mawazo chanya na hasi (Hegel theory, thesis-antithesis = synthesis) yani kwakifupi lazima kuwe na mkosoaji wa mambo, hata CDM itakapoingia madarakani itegemee kupata upinzani mkubwa toka kwa vyama vya upinzani kikiwemo ccm, tena upinzani huo utazidi huu wa sasa.
 
CCM inakufa polepole itachukuwa muda lakini kwa nini watu waende kwenye chama ambacho kinakufa na kinaenda chini!!!. Ni lazima watu waangalie mbele
 
Muda mliokaa madarakani inatosha, hata kama ccm wote mtakua walokole, hatuwahitaji tena!hamna upeo wa kuongoza nchi!
 
Nimekuwa nikifuatilia sana malalamiko yanayotolewa na ima viongozi au wanachama hai na mfu kuhusu malalamiko mengi juu ya CCM. Sasa napenda kuuliza, iwapo kama CCM ikiwatimua mafisadi wote na ikafanya yale yote ambayo cdm mnalalamikia, je mtakuwa tayari wote kurudi CCM?

Waulize akina mama wa pika maandazi wakufaamishe kazi ya amira ccm&cdm vyote vinatakiwa kuwepo unga+amira+unayvo faham=maandazi
 
Warudi?
kwani wote walikua ccm?
zitto hajawahi kuwa ccm,maybe wengine wanaweza kukujibu na kwa msingi huo chadema bado itakuwepo
 
Nimekuwa nikifuatilia sana malalamiko yanayotolewa na ima viongozi au wanachama hai na mfu kuhusu malalamiko mengi juu ya CCM. Sasa napenda kuuliza, iwapo kama CCM ikiwatimua mafisadi wote na ikafanya yale yote ambayo cdm mnalalamikia, je mtakuwa tayari wote kurudi CCM?

Mods,nadhani kuna umuhimu wa kuWAFAHAMISHA BAADHI YA WANA-jf WENZETU matumizi ya NEWS ALERT.

Back to your question,kama ulimtaliki mkeo kwa kuzaa na mwanaume mwingine.Wakiachana utarejeana nae?

Labda kukusaidia kupanua upeo wako,do you genuinely think the only problem with CCM ni existance ya mafisadi in it?And do you think kuwafukuza pekee inatosha kuifanya CCM kuwa safi?Vipi kuhusu madhara yaliyokwishasababishwa na mafisadi hao?

Nahisi unataka kuturejesha kwenye kasumba ya CCM kwamba mtu akiboronga anaombwa (tena hii ni extremely rarely) ajiuzulu,anapewa mamilioni ya kumfariji na taifa linaendelea kubeba gharama ya kumhudumia.Would that be enough for you?

Na kibaya zaidi ni ukweli kuwa swali lako ni too ullusional to be practical.CCM inaweza kutimua mafisadi wote lakini ni vigumu kwa chama hicho kutosa ufisadi kwa sababu ufisadi na CCM ni sawa na ukimwi na virusi vya ukimwi.Kumtimua kila fisadi would mean kuanzia na Kikwete mwenyewe....na mlolongo utakwenda hadi kwa wenyeviti wa serikali za mitaa.Do you think kitu kama hicho ni practically possible?Na hata kikiwa possible,what would you then be left up with kama sio chama kipya kabisa cha siasa?
 
Swali zuri... ha ha ha ila watakuja na sababu nyingine. ohh sijui chama kizee. Kazi yao ni kuponda tu.
 
Nimekuwa nikifuatilia sana malalamiko yanayotolewa na ima viongozi au wanachama hai na mfu kuhusu malalamiko mengi juu ya CCM. Sasa napenda kuuliza, iwapo kama CCM ikiwatimua mafisadi wote na ikafanya yale yote ambayo cdm mnalalamikia, je mtakuwa tayari wote kurudi CCM?
Pole sana Mr. Mark, inaelekea hujui maana ya demokrasia ya vyama vingi. Swali lisilo na mashiko kama hili linatakiwa wapelekewa watu wenye uwezo mwembamba wa kuchambua mambo.
 
Back
Top Bottom