Je, CCM ni chama cha ukombozi Afrika? Naomba kuwajua makada wa CCM walipoteza maisha ktk vita ya ukombozi, na maeneo walipozikwa

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,441
55,018
..kwa muda mrefu sasa waTz tumekuwa tukiambiwa ccm ndiyo Baba wa vyama vya ukombozi kusini mwa Afrika.

..kama hoja hiyo ina ukweli basi bila shaka watakuwepo makada wa ccm wanaotambulika kuwa walipigana bega kwa bega na wapiganaji wa vyama kama FRELIMO, MPLA, ZANU, ZAPU, SWAPO, ANC na PAC.

..na inawezekana bahati mbaya wapo makada wa ccm waliofariki ktk vita ya ukombozi. Je, makada hao ni kina nani? Wamezikwa wapi?

..na kama hakuna taarifa zao, Je, nitakuwa nimekosea nikisema kwamba madai kuwa ccm imeshiriki ktk vita vya ukombozi kusini mwa Afrika ni uzushi?

cc Mzee Mwanakijiji, Nguruvi3, KARLO MWILAPWA , Magonjwa Mtambuka , tindo, Salary Slip
 
Mimi naona hujakosea kabisa.

kama kuna makada/kada aliefia huko,basi mpaka muda huu vijana wa Lumumba wangeshakuja na orodha yao.

..Seth Benjamin ndiye kada pekee anayejulikana kuwa shahidi wa Azimio la Arusha.

..zaidi ya huyo sijasikia mwana tanu au ccm aliyekifia chama chake.

..sina uhakika kama wazalendo uchwara wa uv-ccm na mataga hata wanajua Seth Benjamin ni nani.

.
 
Hoja nzito sana hii. CCM wanajinasibu ni chama cha mapinduzi kwa sababu ya mapinduzi ya Zanzibar ila Karume wanataka tumsahau kama mmoja wa waasisi wa taifa.

CCM waliwafundisha wasauzi kulipua miundombinu yao. Nadhani zile operation bado ni classified.
 
..ccm ilikuwa na wataalamu / instructors wa milipuko waliokuwa wakifundisha wapigania uhuru?
 
JokaKuu, swali lako lina walakini. Linadhania kuwa ili mtu kuwa shujaa ni lazima "afe". Kwamba, kama hakuna mtu aliyekufa basi hakuwa shujaa. Ni kweli wapo Watanzania wengi (sidhani kama unataka kusema ni wana CCM) ambao walitoa michango mbalimbali katika harakati za ukombozi. Kuna wale walioitwa "walikuwa mstari wa mbele" na wale wa "mstari wa nyuma". Waliokuwa mstari wa mbele ni wale wote walioshirikiana bega kwa bega katika mapambano; wapo walioshiriki Msumbiji, Zimbabwe na sehemu nyingine. Hawa walikuwa ni wanajeshi wetu. Wengi walirudi na kuendelea kutumikia nchi katika nyadhifa mbalimbali. Michango yao haijatajwa. Lakini wapo pia ambao walitoa mafunzo ya aina mbalimbali na walifanikisha kwa mfano kupitishwa kwa silaha kupitia "underground railroad" kwenda kwa wapigania Uhuru wa ANC, Frelimo, ZANU-PF, PAC, n.k Hawa pia majina yao hayajatwa.

Kwa hiyo, labda ubadilishe swali lako maana kama unataka kupima ushiriki wa Watanzania kwa kuangalia a. kama walikuwa ni wanachama wa CCM na b. walikufa na kusahaulika; unaweza kupata watu wachache, au usipate watu kabisa. Reframe your question.
 
..kwa muda mrefu sasa waTz tumekuwa tukiambiwa ccm ndiyo Baba wa vyama vya ukombozi kusini mwa Afrika.

..kama hoja hiyo ina ukweli basi bila shaka watakuwepo makada wa ccm wanaotambulika kuwa walipigana bega kwa bega na wapiganaji wa vyama kama FRELIMO, MPLA, ZANU, ZAPU, SWAPO, ANC na PAC.

..na inawezekana bahati mbaya wapo makada wa ccm waliofariki ktk vita ya ukombozi. Je, makada hao ni kina nani? Wamezikwa wapi?

..na kama hakuna taarifa zao, Je, nitakuwa nimekosea nikisema kwamba madai kuwa ccm imeshiriki ktk vita vya ukombozi kusini mwa Afrika ni uzushi?

cc Mzee Mwanakijiji, Nguruvi3, KARLO MWILAPWA , Magonjwa Mtambuka , tindo, Salary Slip
Pamoja na kwamba sikuitwa, lakini imenilazimu nichangie machache ninavyoyajua.

Sidhani kuwa ni kweli waliopoteza maisha katika vita vya ukombozi vilivyopiganwa na "FRELIMO, MPLA, ZANU, ZAPU, SWAPO, ANC na PAC" walikuwa ni wanachama/makada wa vyama hivyo. Ila vyama hivyo vilikuwa na wapiganaji ambao wengi wao ndio waliopoteza maisha.
Sisemi hapa kuwa baadhi ya hao wapiganaji (inawezekana hata wakiwa wote) hawakuwa wanachama wa vyama hivyo kwa maana ya kuwa na kadi. Vile vile, sidhani kuwa viongozi wa ngazi zote wa vyama hivyo walikuwa wapiganaji, kwa maana ya kuwa kwenye uwanja wa mapambano kivita. Wegine walikuwa katika nafasi mbalimbali za uendeshaji wa shughuli za vyama hivyo.

Ukija kwa CCM, nafasi yake katika ukombozi utahusisha zaidi kushirikiana na pengine kuelekeza baadhi ya shughuli za vyama hivyo rafiki.
Na kwa kuwa CCM ndio walikuwa na serikali yao hapa kwetu, na serikali hiyo ilikuwa na chombo chake cha shughuli za kivita, bila shaka chama hicho hakikusita kutumia nyenzo hizo kuwasaidia vyama rafiki.

Sasa hapa ndipo swali lako linapokuwa linajibika, kwamba hata kama CCM haikuwa na 'wapiganaji makada wa chama' kuwepo kwa jeshi (ambalo kiukweli halikuwa la CCM), chama hicho kiliweza kutumia kifaa hicho katika ukombozi.

Wapo wanajeshi wetu wengi waliopoteza maisha yao katika mapambano ya ukombozi na hawakuwa wanachama wa CCM, kwa maana ya uanachama tunaouelewa wote hapa.

Nina hakika watu kama 'Colonel' Mbita unaweza kumpa nafasi yake katika mapambano hayo. Na wapo wengi wa aina yake.

Tahadhari: usiihusishe CCM iliyopo sasa katika swali lako. Hii ni CCM nyingine, tofauti kabisa na hiyo ya wakati huo.
 
Kwa umri wako unatia huruma kuuliza maswali kama haya.
 
Jibu la haraka ni "ndiyo".

..lakini ukipitia makala mbalimbali za wapigania uhuru hazionyeshi kama kulikuwa na waalimu / instructors wa ccm ktk makambi kijeshi ya wakimbizi.

..makala nyingi zinaelezea kwamba makambi hayo yalikuwa yanaendeshwa na kusimamiwa na wapigania uhuru wenyewe na hayakuwa na wasimamizi wa Kitanzania.
 
..Hashim Mbita alikuwa Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya OAU ambayo ilikuwa na makao yake makuu hapa D'Salaam. Kamati ya ukombozi ilikuwa na kazi ya ku-mobilize misaada kwa ajili ya vyama vya ukombozi, na misaada hiyo ilitoka ktk nchi mbalimbali ndani na nje ya Afrika.
 
Sawa kabisa; na bila shaka hata humo OAU utaiona nafasi ya CCM katika upigania uhuru wa Africa.
Kupigana ni kwa aina nyingi, si kwa silaha peke yake.
 
JokaKuu, swali lako lina walakini. Linadhania kuwa ili mtu kuwa shujaa ni lazima "afe". Kwamba, kama hakuna mtu aliyekufa basi hakuwa shujaa. Ni kweli wapo Watanzania wengi (sidhani kama unataka kusema ni wana CCM) ambao walitoa michango mbalimbali katika harakati za ukombozi. Kuna wale walioitwa "walikuwa mstari wa mbele" na wale wa "mstari wa nyuma". Waliokuwa mstari wa mbele ni wale wote walioshirikiana bega kwa bega katika mapambano; wapo walioshiriki Msumbiji, Zimbabwe na sehemu nyingine. Hawa walikuwa ni wanajeshi wetu. Wengi walirudi na kuendelea kutumikia nchi katika nyadhifa mbalimbali. Michango yao haijatajwa. Lakini wapo pia ambao walitoa mafunzo ya aina mbalimbali na walifanikisha kwa mfano kupitishwa kwa silaha kupitia "underground railroad" kwenda kwa wapigania Uhuru wa ANC, Frelimo, ZANU-PF, PAC, n.k Hawa pia majina yao hayajatwa.

Kwa hiyo, labda ubadilishe swali lako maana kama unataka kupima ushiriki wa Watanzania kwa kuangalia a. kama walikuwa ni wanachama wa CCM na b. walikufa na kusahaulika; unaweza kupata watu wachache, au usipate watu kabisa. Reframe your question.

..kwa leo tuanze na mchango wa wana-CCM, ukiratibiwa toka makao makuu ya CCM.

..baada ya hapo tunaweza ku-expand na kutafuta mchango wa Tanzania wote.

..but so far sijaona mchango wa wana-ccm ktk mafunzo au operation za kijeshi zilizofanywa na wapigania uhuru.
 
Sawa kabisa; na bila shaka hata humo OAU utaiona nafasi ya CCM katika upigania uhuru wa Africa.
Kupigana ni kwa aina nyingi, si kwa silaha peke yake.

..hebu tuonyeshe basi kama umeuona mchango wa ccm. tupe mfano walau mmoja.

..
 
..lakini ukipitia makala mbalimbali za wapigania uhuru hazionyeshi kama kulikuwa na waalimu / instructors wa ccm ktk makambi kijeshi ya wakimbizi.

..makala nyingi zinaelezea kwamba makambi hayo yalikuwa yanaendeshwa na kusimamiwa na wapigania uhuru wenyewe na hayakuwa na wasimamizi wa Kitanzania.
JokaaKuu, huo mstari wa pili hapo juu ufanyie tafakuri zaidi. Sina hakika kama ulitegemea kwamba makambi hayo yaendeshwe na CCM au Tanzania. Mbona hilo lisingewezekana kabisa?
Au unayo maana nyingine?
 
..nataka kujua role ya ccm ilikuwa ni nini ktk makambi hayo mpaka wajiite chama cha ukombozi.
 
Sawa!
Tungekuwa na uwezo wa kumwita Pius Msekwa hapa labda angeweza kutusaidia na swali lako gumu.
Sisi wengine tunapapasa tu na kukisia.
Kwa mfano. Kama unakubali kuwa Tanzania ilishiriki/saidia katika ukombozi wa Afrika, na kujiruhusu kudadisi ni nani alikuwa anafanya maamuzi ya Tanzania kushiriki, huenda ingesaidia kidogo kuona mchango iliokuwa nao CCM katika maamzi hayo.

CCM ndio ilikuwa na serikali na hapakuwa na chama kingine chochote cha kuhoji maamzi yake.

Kama nilivyoeleza hapo juu, mimi nakisia tu. Natumia 'instinct' kujaribu kujibu swali.
 
..Seth Benjamin ndiye kada pekee anayejulikana kuwa shahidi wa Azimio la Arusha.

..zaidi ya huyo sijasikia mwana tanu au ccm aliyekifia chama chake.

..sina uhakika kama wazalendo uchwara wa uv-ccm na mataga hata wanajua Seth Benjamin ni nani.

.
Huyu kada sijui kama kizazi hiki wanamsoma tena historia yake ya ushujaa!
 
Back
Top Bottom