Mambo mengine mwacheni Pascal Mayalla awe Paskali Mayalla a.k.a Njaa. Au mnataka arudi kwenye lile chaka lake la Pasco wa JF?Aliahidi atatoa story yote ya mahojiano nashangaa mpaka leo hii hajatuwekea uzi wa kilichomtokea, nadhani alitishwa
Nahisi walimbinya korodani maana analiogopa bunge kuliko al-shababMambo mengine mwacheni Pascal Mayalla awe Paskali Mayalla a.k.a Njaa. Au mnataka arudi kwenye lile chaka lake la Pasco wa JF?
Paskali kuna kitu umeruka,nacho ni inferiority complex.Wanabodi,
Naomba kuanza na angalizo, hii ni thread ya swali na sio statement.
Jee Bunge Letu Ni Bunge Butu?. Angalia Bunge la Uingereza Lenye Meno Linavyong'ata Serikali. Jee Kuna Ubaya Wowote na sisi Bunge Letu Tukiiga Mazuri ya Mabunge Mengine Katika Kuisimamia Serikali Zao?.
Kumewahi kutolewa tuhuma kadhaa kuhudu udhaifu wa mhimili wetu wa Bunge, hadi kuitwa "Bunge Dhaifu" au "Bunge Butu" kwa hoja kuwa halina meno makali ya kuweza kung'ata Mhimili mmoja wa The Executive, wakati mhimili huo unapokwenda kinyume cha sheria, taratibu na kanuni nikitolea mfano mmoja tuu wa matumizi ya fedha za umma.
Hoja za watoa hoja ni hatua mbali mbali zinazochukuliwa na Bunge, kunyamazia makosa ya the executive.
Kwa vile Bunge letu tunafuata mfumo wa Westiminster wa Uingereza ambao pia ndio unaofutwa na mabunge mengi ya nchi za Jumuiya ya Madola, jee kuna ubaya Bunge letu na Wabunge wetu, wakanoa meno na kuwa makali kama Bunge la Uingereza ambalo ni Bunge lenye meno kweli, ukilinganisha na Bunge letu, mtu unaweza kuliita Bunge letu ni Bunge...(sitaki kuitwa tena Dodoma).
Ripoti ya CAG ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali, itashuka Bungeni Dodoma hivi karibuni, tuifuatilie kuona ripoti hiyo itabaini nini na kulifuatilia Bunge letu litafanya nini.
Natoa wito kwa Wabunge wetu, kufuatilia kwa karibu kinachoendelea kwenye Bunge la Uingereza kwa sasa, ambapo Bunge la nchi ,linaonyesha perliamentary supremacy kwa kuiathibu The Executive, na kura zikitosha, Waziri Mkuu Bi Theresa May ndio safari.
Soma hii
Our cover in Britain dissects a week in which Theresa May, the prime minister, has offered to resign and Parliament has seized control of Brexit—sidelining the executive for the first time in over a century. Sadly, Mrs May’s sacrifice does nothing to solve Britain’s Brexit mess. Her resignation depends on Parliament voting through her deal after two crushing defeats. Even if she succeeds (a very big if), Parliament remains hopelessly divided about Britain’s future relationship with Europe. If her deal fails and Parliament forces its own alternative on her, she could resist. If she goes, the next prime minister’s Brexit plan will have no popular mandate. Brexit remains as radically uncertain as it has ever been.
Source ni The Economist.
Nawatakia Furahi Dei Njema.
Paskali
...Jee Kuna Ubaya Wowote na sisi Bunge Letu Tukiiga Mazuri ya Mabunge Mengine Katika Kuisimamia Serikali Zao?.
Hatuna bunge sisi zaidi ya wapiga vigelegele wa CCM, ni kama toy la mbwaUwe makini, hivyo viulizo wenzio huwa hawavioni.
Utasikia umelikashifu bunge kwa kuliita butu.!
Na huku kwetu tatizo sio bunge kuwa na meno, tatizo ni katiba ya nchi ndio inalea Madudu yote haya..
Kwetu chama ndio kinamvua ubunge mbunge.
Katiba haijampa mwananchi haki yake kumlinda mwakilishi wake.
Siku bunge likiwa huru labda ndio tutaona mijadala moto na yenye nguvu dhidi ya serikali.