Je, Bunge letu ni Bunge Butu?. Angalia Bunge la Uingereza lenye meno linavyong'ata Serikali. Je, Kuna ubaya tukiiga?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,475
2,000
Wanabodi,
Naomba kuanza na angalizo, hii ni thread ya swali na sio statement.

Jee Bunge Letu Ni Bunge Butu?. Angalia Bunge la Uingereza Lenye Meno Linavyong'ata Serikali. Jee Kuna Ubaya Wowote na sisi Bunge Letu Tukiiga Mazuri ya Mabunge Mengine Katika Kuisimamia Serikali Zao?.

Kumewahi kutolewa tuhuma kadhaa kuhusu udhaifu wa mhimili wetu wa Bunge, hadi kuitwa "Bunge Dhaifu" au "Bunge Butu" kwa hoja kuwa halina meno makali ya kuweza kung'ata Mhimili mmoja wa The Executive, wakati mhimili huo unapokwenda kinyume cha sheria, taratibu na kanuni nikitolea mfano mmoja tuu wa matumizi ya fedha za umma.

Hoja za watoa hoja ni hatua mbali mbali zinazochukuliwa na Bunge, kunyamazia makosa ya the executive.

Kwa vile Bunge letu tunafuata mfumo wa Westiminster wa Uingereza ambao pia ndio unaofutwa na mabunge mengi ya nchi za Jumuiya ya Madola, jee kuna ubaya Bunge letu na Wabunge wetu, wakanoa meno na kuwa makali kama Bunge la Uingereza ambalo ni Bunge lenye meno kweli, ukilinganisha na Bunge letu, mtu unaweza kuliita Bunge letu ni Bunge...(sitaki kuitwa tena Dodoma).

Ripoti ya CAG ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali, imeishakabidhiwa kwa rais, hivyo sasa itashuka Bungeni Dodoma wiki ya kwanza ya kikao cha mwezi April, hivyo kuwa a public document, tuifuatilie ripoti hiyo itabaini nini na kulifuatilia Bunge letu litafanya nini this time.

Ripoti ya CAG kwa miaka mitatu mfululizo, 2016, 2017 na 2018, zote zimeonyesha serikali imekuwa ikitumia fedha za umma kutoka mfuko mkuu wa hazina bila kufuata sheria, taratibu na kanuni, ikiwemo kuidhinishwa na Bunge, tabia hii imekuwa ikijirudia mwaka hadi mwaka, na Bunge limekuwa halifanyi kitu, hali iliyopelekea Bunge kuitwa dhaifu kutokana na kuonyesha udhaifu huu katika kuisimamia serikali ifuate sheria, taratibu na kanuni za matumizi ya fedha za umma, ikiwamo matumizi yote ya fedha za umma, lazima yaidhinishwe na Bunge, isipokuwa matumizi ya dharura pekee.

Jee tabia hii itajirudia katika Ripoti ya CAG ya safari hii?, likijirudia, Jee Bunge letu litafanya chochote tofauti na nyuma kuonyesha Bunge letu sio dhaifu katika kuisimamia serikali?.

Natoa wito kwa Waheshimiwa Wabunge wetu, kufuatilia kwa karibu kinachoendelea kwenye Bunge la Uingereza kwa sasa, ambapo Bunge la nchi ,linaonyesha perliamentary supremacy kwa kuiadhibu The Executive, na kura zikitosha, Waziri Mkuu Bi Theresa May ndio safari.

Soma hii
Our cover in Britain dissects a week in which Theresa May, the prime minister, has offered to resign and Parliament has seized control of Brexit—sidelining the executive for the first time in over a century. Sadly, Mrs May’s sacrifice does nothing to solve Britain’s Brexit mess. Her resignation depends on Parliament voting through her deal after two crushing defeats. Even if she succeeds (a very big if), Parliament remains hopelessly divided about Britain’s future relationship with Europe. If her deal fails and Parliament forces its own alternative on her, she could resist. If she goes, the next prime minister’s Brexit plan will have no popular mandate. Brexit remains as radically uncertain as it has ever been.
Source ni The Economist.

Nawatakia Furahi Dei Njema.

Paskali
 

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
23,765
2,000
Uwe makini, hivyo viulizo wenzio huwa hawavioni.

Utasikia umelikashifu bunge kwa kuliita butu.!

Na huku kwetu tatizo sio bunge kuwa na meno, tatizo ni katiba ya nchi ndio inalea Madudu yote haya..

Kwetu chama ndio kinamvua ubunge mbunge.

Katiba haijampa mwananchi haki yake kumlinda mwakilishi wake.

Siku bunge likiwa huru labda ndio tutaona mijadala moto na yenye nguvu dhidi ya serikali.
 

mkafrend

JF-Expert Member
May 12, 2014
3,053
2,000
Natoa wito kwa Wabunge wetu, kufuatilia kwa karibu kinachoendelea kwenye Bunge la Uingereza kwa sasa, ambapo Bunge la nchi ,linaonyesha perliamentary supremacy kwa kuiathibu The Executive, na kura zikitosha, Waziri Mkuu Bi Theresa May ndio safari.
Paskali
Comrade nchi zilizoendelea mbunge huzungumza yatokayo kichwani mwake - nchi zinazoendelea wabunge huzungumza maneno waliyolishwa kwenye vikao vya chama chao

Tuna safari kama ya wana wa Israel (Miaka 40)
 

KIDUNDULIMA

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
965
500
Bunge huwa kali pale kunapokuwa na uwakilishi wa vyama unaoshabihiana, kosa letu ni kuruhusu chama tawala kuwa na two third ya kufanya maamuzi bungeni. Serikali ya chama tawala hutumia mwanya huo kuwadhiti wabunge wake wasiende tofauti na matakwa ya serikali ya chama chao.
 

Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,469
2,000
Bunge la Uingereza linaisimamia serikali yenye mfumo tofauti na wa serikali ya kwetu. Kule uingereza Waziri Mkuu ni Mkuu wa Serikali wakati Mkuu wa nchi ni Malkia.

Hapa kwetu tuna Rais ambaye ni Mkuu wa Serikali na pia ni Mkuu wa Nchi. Waziri Mkuu wa Uingereza si Waziri Mkuu Mtendaji bali ni kiongozi tu wa Serikali ya Uingereza. Hapa kwetu Rais ni Rais Mtendaji.

Uingereza chama cha siasa hakina nguvu ya kufukuza Mbunge uanachama wake na mbunge huyo kupoteza sifa ya kuwa Mbunge. Hapa kwetu Mbunge akihama chama ama kufukuzwa uanachama wa chama chake ubunge wake unapotea.

Hapa kwetu Rais wa Nchi kwa sasa ndiye Mwenyekiti wa CCM ambaye anaongoza kikao kinachoweza kumfukuza uanachama mbunge yeyote bila ya kuwa na sababu ya msingi. Kwa maana hiyo unapotaka wabunge wa CCM (Ndiyo walio wengi bungeni) wapingane na serikali inayoongozwa na Rais ambaye ni mwenyekiti wa chama chao, UNAJIDANGANYA.
 

CHLOVEK

JF-Expert Member
Mar 8, 2017
537
1,000
Pasikali, usitubadilishie mada bwana, acha kwanza tuongelee "Air hostage wetu, rangi ya ndege yetu, balozi wa Zambia anayeaga kila siku" haya tuna uwezo nayo. Bunge la uingereza lina miaka zaidi 200 tangu uwepo wake, hatuwezi kujadili mambo kwa weledi kama wao.
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,784
2,000

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom