Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,129
- 35,148
Siku chache kutoka sasa Bunge la Katiba litaanza rasmi mkoani Dodoma. Watanzania wengi sana tungependa kusikia au kuona moja kwa moja mijadala yote ya Katiba katika Bunge hilo kupitia wajumbe mbalimbali wanaotuwakilisha.
Mpaka sasa bado sijasikia utaratibu wowote wa kurushwa kwa matangazo hayo, yaani kuna ukimya fulani kutoka mamlaka husika!!
Binafsi nitapinga ukiritimba na urasimu wowote katika kurusha matangazo hayo, ambao mara zote umekuwa ukifanywa na serikali katika matukio muhimu ya kisiasa kama Matangazo ya vikao vya bunge.
Wadau wote tunapenda kupaza sauti zetu kutaka kusikia sasa ni utaratibu upi utatumika katika kutangaza ama kuonyesha matangazo hayo moja kwa moja.