Mcqueenen
JF-Expert Member
- Nov 2, 2019
- 6,818
- 11,542
Nasilsiniz JF üye?
Naomba unisamehe maana kwa haraka haraka hata mimi najishangaa kuuliza hili swali, kwasababu it's a No-brainer right?, Namaanisha ofcourse binadamu sisi sio kama wanyama wanaotawaliwa kwa instincts, sisi tuna free will right?, Maana tokea nianze kujitambua mpaka sasa kila nachofanya nimefanya kwa hiari yangu. nikitaka kunyanyua mkono nanyanyua nikitaka kucheka nacheka. Mimi ndiyo nauendesha huu mwili si ndio?
Sadly, sikuizi mwenzenu nimeanza ku'second guess hayo mawazo baada ya ku'consider hizi factors.
1. Uwepo wa Mungu anayetaka ufuate masharti yake: Uwe mkristo au Muislam, Mungu anataka ufuate masharti yake, kuna mambo unatakiwa kuyafanya na kuna mambo hutakiwi kuyafanya. Kuna zawadi na adhabu kwa watakomfuata au kumpinga. Kitendo cha kuwepo tu adhabu nisipomfuata Mungu kinamaanisha sina hiari/free will katika maisha yangu hapa duniani, maana ningekuwa nayo ningekuwa na uhuru wa kufanya jambo lolote liwe jema au baya bila kuwa na consequences. Ni sawa na mtu akuwekee bunduki kichwani akuambie una uhuru wa kutaja au kutotaja password yako ya benki, ila usipotaja nakuua. Sasa hapo unao huo uhuru?
2. Mazingira: Hapa nazungumzia mazingira yanayonizunguka tangu nizaliwe, ikihusisha vitu kama utamaduni wa jamii inayonizunguka(mfano jinsi ninavyovaa, ninavyoongea, ninayolia msibani, ninavyokula nk. Siwezi kwenda kinyume na utamaduni wa jamii niliyopo. Siwezi kwenda msibani na boxa tu huku nacheka, sina huo uhuru),Sheria inayonitawala (Siwezi kuendesha gari upande wa kulia), Malezi niliyokulia(Kwetu mwanaume Siwezi kusuka nywele nitakataliwa na ukoo), Elimu niliyoijaza kichwani (Elimu naweka mwenyewe kichwani ila ikishakaa yenyewe ndiyo inanitawala na kuniongoza, nilishasoma bailojia kwahyo siwezi kula vyakula vilivyochacha.), Status niliyo nayo katika jamii (Hakimu siwezi kushinda kwenye vijiwe vya kubeti na kulewa gongo),teknolojia, nk. Hivi vyote ni vitu ambavyo vinanipokonya uhuru wangu wa machaguzi. Ndiyo maana ukichukua binadamu waliokulia katika mazingira tofauti lazima watakuwa na tabia tofauti, ina maana hawana uhuru wa hizo tabia bali mazingira ndiyo huwaamulia. Vilevile binadamu waliokulia mazingira yanayofanana huwa na tabia inazofanana (Mf. Kuna tabia zinajulikana za wazaramo,wahaya,wazungu,wachina nk.)
3. Vizingiti vya kibaiolojia: Ninaweza kuwa na uhuru wote ila siwezi kuipinga baiolojia yangu, Siwezi kuacha kula, kulala, kupumua, kujisaidia nk. Pia siwezi kupaa,kubeba gari, kujifupisha, kujirefusha, kula viwembe, kupiga bao 10 nk.
Hivyo kwasababu lazima nile kuna vitu lazima nifanye ili nile (mf. kuomba, kufanya kazi, kubeti, kuiba nk.) na sina hiari katika hilo.
4. Brain Chemistry: Neuroscientists bado wanaendelea kugundua mchango mkubwa wa kemikali mbalimbali katika ubongo ambazo zinaweza kutengeneza,kubadili au kuondoa tabia kwa mnyama. Ubongo wa binadamu umeundwa kurespond to chemicals mbalimbal ndani yake. Mfano wa hizi chemicals ni Dopamine, Adrenaline, Oxytocin, Serotonin, Testosterone, Oestrogen na zingine nyingi. Viwango vya hizi chemicals vinaathiri tabia ya mtu. Mfano Dopamine inatoka pale unapopata raha, kwahyo Dopamine husababisha mtu kufanya vitu ambavyo vinampa raha (kama Chaputa, kubeti, ngono, Kutumia mihadarati, kucheza mpira nk. nk.) Ukiondolewa dopamine unaweza ukafa maana unaweza ukaacha hata kula kwasababu huoni raha yake. Vilevile ikizidishwa dopamine kwenye ubongo unaweza ukafanya kile kitu kinachokuletea dopamine mpaka ukafa (mfano unaweza ukaacha kula ili utumie cocaine)
Kuna panya aliwekewa cocaine na chakula, ila akaacha chakula ili ale cocaine mpaka akafa kwa njaa.
Mfano mwingine ni hizi kemikali za kijinsia kama Oestrogen na Testosterone ndio hufanya mwanaume au mwanamke kuwa na tabia za kiume au kike anapobarehe. Oestrogen inapozalishwa mda wa hedhi/mimbA hubadili tabia ya mwanamke. Ukiachana na hizi kemikali natural kwenye ubongo, hata hizi artificial tunazokula binadamu kama bangi, pombe, Cocaine Nk. zinaonyesha jinsi ambavyo kemikali kwenye ubongo huathiri tabia ya mtu. Sasa kama tabia zetu zinaathiriwa na viwango vya kemikali kwenye ubongo wetu, utasemaje kuwa tuna free will?