Je, Biblia inasema nini kuhusu chakula?

Uko sahihi mkuu,ni ruksa kula cho chote kwa mwenye imani, ila uhuru huo usiwakwaze wenye imani dhaifu.Kwa hiyo kama kwa mfano unaona ukila Nguruwe ndugu yako atakwazika ni bora kuacha.Biblia imeweka wazi kwamba ni dhambi kula kitu kama unajua kwamba kwa kufanya hivyo ndugu yako atakwazika(1Wak.8:9-13.).Biblia pia inakataza kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa idols(miungu ya uongo),mashetani na damu(Mat.15:29).Swala la kula damu linawahusu sana ndugu zetu Wachaga na Wamasai.
 
Me Nahic We Unaongelea Kisabato Huongelei Kibiblia Hayo Maelezo Ya Paulo Kujibu Hoja Za Watu Waliokuwa Wana Muuliza Umeyatoa Wapi ,pili Kama Zilikua Zinajibu Hoja Za Wengine Kwa Nn Ziliwekwa Kwenye Biblia Tukapewa Cc Wakati Hazituhusu Na Kama Hazituhusu Ni Nyalaka Zote Za Paulo Au Baadhi Ya Mistari Ndo Haituhusu?
 
WEWE BIBLIA HAISOMWI KWA KUDOKOA VIFUNGU, NGOJA NIKUULIZE, JE MUNGU HUJIPINGA AU NYINYI KWA ULAFI WENU HUPOTOSHA VIFUNGU?

INAKUWAJE HAPA MUNGU HUYO HUYO YESU, AAPE KUWAPOTEZA WOTE WALA NGURUWE NA PANYA ,HALAFU NAADAE ATUHUSU TENA MLE PANYA?


ISAYA 66

15 Maana Bwana atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto.

16 Kwa maana Bwana atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga wake; nao watakaouawa na Bwana watakuwa wengi.

17 Watu wale wajitakasao, na kujisafisha katika bustani, nyuma yake aliye katikati; wakila nyama ya nguruwe, na machukizo, na panya; watakoma pamoja, asema Bwana.

18 Nami nayajua matendo yao na mawazo yao; wakati unakuja nitakapokusanya mataifa yote na lugha zote; nao watakuja, nao watauona utukufu wangu

HAPO UTAGUNDUA SHIDA IPO KWENU SABABU YA ULAFI HIVO HUPELEKEA MPOTOSHE VIFUNGU VYA BIBLIA
 

hapo kwenye red kuna uhusiano gani na maandiko uliyoyaandika hapa?
 
Uwiii umenikumbusha lile rojo la ndani ya mfupa wa kuchoma wa kitimoto, linanyonywa na ulimi atiiiii.....au unalivuta na kidole?
Yaani natamani kama Jumamosi hii...sema nene, badae naenda kontena.
Ka vepe...ntakustua
Jipange niko kwenye Xmas mode tayari
 
Matayo 15:10
. Akawaita makutano akawaambia
Matayo 15:11
. Sikilizeni, mfahamu; Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho mtu unajisi; bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho mtu unajisi.
Matayo 15:12
. Ndipo wanafunzi wake walipomwendea, wakamwambia, Wajua ya kuwa Mafarisayo walipolisikia neno lile walichukizwa?
Matayo 15:13
. Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang'olewa.
Matayo 15:14
. Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.
Matayo 15:15
. Basi Petro akajibu, akamwambia, Tueleze mfano huo.
Matayo 15:16
. Yesu akasema, Hata sasa ninyi nanyi mngali hamna akili?
Matayo 15:17
. Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni?
Matayo 15:18
. Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.
Matayo 15:19
. Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;
 
Kwa hiyo Mungu akisema kuwa kuna vyakula najisi anaweza kusema tena kuwa hakuna Vyakula najisi mungu huyo wa hivyo anajichanganya sana.
Matayo 15:10
. Akawaita makutano akawaambia
Matayo 15:11
. Sikilizeni, mfahamu; Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho mtu unajisi; bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho mtu unajisi.
Matayo 15:12
. Ndipo wanafunzi wake walipomwendea, wakamwambia, Wajua ya kuwa Mafarisayo walipolisikia neno lile walichukizwa?
Matayo 15:13
. Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang'olewa.
Matayo 15:14
. Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.
Matayo 15:15
. Basi Petro akajibu, akamwambia, Tueleze mfano huo.
Matayo 15:16
. Yesu akasema, Hata sasa ninyi nanyi mngali hamna akili?
Matayo 15:17
. Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni?
Matayo 15:18
. Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.
Matayo 15:19
. Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;
 
Kilichotakaswa na Mungu usikiite najisi
 
Katika kitabu hicho ni vitu vingapi vimeorotheshwa ni nàjisi; je unavifata au kitimoto tu

Kwa upande wangu na imani yangu kitimoto yenyewe nakula sababu vitu vilivyoorezeshwa naviona mtaani vinaliwa mbaya ila kwa vile ss tulishaambiwa kinachomtia mtu najisi n kile kinachomtoka kinywani mwake na wala si kiingiacho hiyo ni kwa upande wa imani yangu
 
Kwa hiyo Mungu akisema kuwa kuna vyakula najisi anaweza kusema tena kuwa hakuna Vyakula najisi mungu huyo wa hivyo anajichanganya sana.
MUNGU hajichanganyi, bila wewe ndo unajichanganya. Lazima ujue Amri juu ya Vyakula ilitolewa kipindi gani na kwanini ???. Hakuna chakula najisi, wewe ukiona mjusi anapanda mbanike na mkamue taratiiibu.
 
Wewe unatudanganya kwa kujifanya Unajua Biblia kumbe hakuna lolote, WASABATO bhana !!!, Kwa kujifanya ujuaji. Hamna kitu hapo. Kitimoto ni mboga km mboga zingine.
 
Basi tuendelee kugonga kitimoto
 
Hapa tutabishana sana kwa vifungu vya biblia, wengine km kawaida wanapenda sana kuponda au kutaka kuonyesha kuwa biblia ina makosa flani yaani inajichanganya ilhali aonyeshe yeye dini yake ni sahihi na haina mapungufu.

Tofauti za maandiko ya kibiblia ambayo wengi hawajajua ni kuhusu MUDA NA TAFSIRI YAKE.
kwa mfano kuhusu petro, kipindi chake kulikuwa na udhaifu wa jamii kubwa kuweza kuamini katika midoli na hivyo maisha ya jamii yalizungukwa na imani hyo.
Ukiangalia majibu yake yanaendana na jamii hiyo na hata maswali ya jamii hiyo yalijikita katika tafsiri yenye muonekano wa ulaji wa vyakula either kwa kula nyama iliyotolewa kafara zao kwanza na je kuna madhara gani mtu akila nyama isiyopitia kwa makafara yao hayo na watu wakataka kujua position ya neno la mungu.

Biblia haisomwi kama vitabu vya abunuwasi.
Hao wengine pia watujuze kuwa mbona kiongozi wao alioa wake 11 lakini kitabu chao kunazungumzia waoe 4 pekee? Tumsikilize nani hapo? Au huyo kiongozi aliteleza kidogo? Maana kitabu chao chaeleza hivyo, usizidi 4.

Tusome vitabu vya dini huku tukiomba pia kuongozwa na roho mtakatifu
 
Linda sana moyo kuliko vyote ulindavyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…