Katika hiyo hiyo biblia tuwekee hapa walawi 11 kwenda mbele alafu utueleweshe tuielewe vp biblia huku ni ndio na kule ni hapana katika jambo hilohiloHAKUNA CHAKULA NAJISI.
Warumi 14:2,14,20
2 Mtu mmoja anayo imani, anakula vyote; lakini yeye aliye dhaifu hula mboga.
14 Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi.
20 Kwa ajili ya chakula usiiharibu kazi ya Mungu. Kweli, vyote ni safi; bali ni vibaya kwa mtu alaye na kujikwaza.
Marko 7:18-19
18 Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi;
19 kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote.
Wakolosai 2:16
16 Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;
Waebrania 13:9
9 Msipeperushwe huku na huku kwa mafundisho tofauti ya kigeni. Neema ya Mungu ndiyo inayoimarisha roho zetu na wala si masharti juu ya chakula; Masharti hayo kamwe hayakumsaidia mtu yeyote aliyeyafuata.
naona unajaribu kujenga hoja kwa kuangalia tu nyaraka za paulo, vipi kuhusu Yesu kwenye marko 7 : 18-22? hapo unasemaje. alivitakasa si tu vyakula bali na vinywaji. #si kimuingiacho mtu bali kimtokacho ndicho kinacompa mtu unajisi# biblia ipo wide mkuu usijaribu ukiitafsiri ukiwa closed minded but try to be opene minded.ACHA KUTAFSIRI BIBLIA KIHOLELA HIVO, TABIA HII IMEPELEKEA MADHEHEBU MENGI NA UTITIRI WA MANABII NA MITUME WASIOHESABIKA HAPA DAR ,ACHANA NA WALE WA MIKOANI,
Biblia haikurupukiwi hivo, HASA MAANDIKO YA MTUME PAULO
Ikumbukwe kuwa vitabu vya Paulo viliandikwa kama barua na wakati mwingine ilikuwa ni katika kujibu hoja ambazo zilileta mkanganyiko kwa waumini maana Paulo alikuwa akihubiri na kisha kuondoka mahali hapo asirudi tena. Hivyo kama kulikuwa na jambo lolote lililohitaji ufafanuzi basi walimwandikia Paulo naye aliwaandikia kuwajibu ambapo nyaraka zake zilikusanywa na kuwekwa pamoja na leo tunazisoma kama maandiko yaliyovuviwa. Kwa bahati mbaya nyaraka zile ambazo waumini walimtumia Paulo hatunazo hivyo wakati mwingine inakuwa vigumu kujua ni kitu gani kilipelekea mitume kujibu hivyo walivyojibu.
Wengi kati ya wakristo wa awali ambao Paulo alikuwa akiwaandikia barua walikuwa ni wapagani waongofu na hivyo waliishi katika jamii ya kipagani, na sehemu kubwa ya jamii iliyowazunguka walikuwa ni wapagani.
Katika kipindi hicho kulikuwa na utaratibu kwamba nyama yoyote kabla ya kuuzwa ilikuwa sharti itolewe sadaka kwa sanamu. Jambo hili liliwapa shida kidogo baadhi ya wakristo kwamba huenda Mungu akawahesabia dhambi kwa kula nyama iliyotolewa sadaka kwa sanamu.
Ndipo Paulo sasa anawajibu na kuwaambia kuwa sanamu haineni na wala siyo kitu na mwenye imani anajua kuwa sanamu si kitu chochote na hivyo hula nyama pasipo kujali kwamba imetolewa sadaka kwa sanamu au la. Lakini yule mwenye imani haba huwa na mashaka kwamba huenda ikawa ni dhambi na hivyo anaacha kula nyama na kuamua kula mboga.
Mahali pengine anaandika kwamba mkienda sokoni msiulize ulize na wala ndugu yenu akiwakaribisha kuleni bila kuuliza. Hakusema kwamba wasiulize ile nyama ni ya mnyama gani hasha! Alisema wasiulize kama hiyo nyama imetolewa sadaka kwa sanamu au la. Mwishoni anasema endapo kwa yeye kula nyama ( iliyotolewa sadaka kwa sanamu ) kutamkwaza nduguye basi hatakula nyama ili asije akamkwaza ndugu yake ambaye Yesu Kristo alimwaga damu pale mslabani kwa ajiliya wokvu wake.
Bado tunaona kwamba tatizo hapo halikuwa juu ya wanyama najisi bali lilikuwa juu ya nyama iliyotolewa sadaka kwa sanamu.
Jambo hili la vyakula safi na najisi lilikuwa linaeleweka vizuri miongoni mwa wakristo wa kipindi hicho, ndiyo maana huoni Biblia ikiliongelea. Katika mafungu yote hapo juu tumeona kuwa hakukuwa na shida yoyote juu ya wanyama najisi na wasio najisi.
Mbona hiyo ipo wazi, soma had mwisho, hakuzungumzia vyakula,bali matendo ya mwilinaona unajaribu kujenga hoja kwa kuangalia tu nyaraka za paulo, vipi kuhusu Yesu kwenye marko 7 : 18-22? hapo unasemaje. alivitakasa si tu vyakula bali na vinywaji. #si kimuingiacho mtu bali kimtokacho ndicho kinacompa mtu unajisi# biblia ipo wide mkuu usijaribu ukiitafsiri ukiwa closed minded but try to be opene minded.
Anachoelekeza Yesu hapa ni kukanusha imani iliyokuwa imeenea kuwa endapo Myahudi mtauwa (mcha-Mungu kwelikweli) angefuata tu sheria za usafi na taratibu za kidini angekuwa safi kimaadili/kiroho. Kwa upande mwingine, hakuna chakula ambacho kwa chenyewe kinaweza kuinajisi tabia ya mtu. Kinachonajisi ni mawazo maovu (ambayo hujitokeza kwa ndani na kujidhihirisha katika matendo ya nje). Ndiyo maana Biblia inatuambia, “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.” Mithali 4:23naona unajaribu kujenga hoja kwa kuangalia tu nyaraka za paulo, vipi kuhusu Yesu kwenye marko 7 : 18-22? hapo unasemaje. alivitakasa si tu vyakula bali na vinywaji. #si kimuingiacho mtu bali kimtokacho ndicho kinacompa mtu unajisi# biblia ipo wide mkuu usijaribu ukiitafsiri ukiwa closed minded but try to be opene minded.
AminAnachoelekeza Yesu hapa ni kukanusha imani iliyokuwa imeenea kuwa endapo Myahudi mtauwa (mcha-Mungu kwelikweli) angefuata tu sheria za usafi na taratibu za kidini angekuwa safi kimaadili/kiroho. Kwa upande mwingine, hakuna chakula ambacho kwa chenyewe kinaweza kuinajisi tabia ya mtu. Kinachonajisi ni mawazo maovu (ambayo hujitokeza kwa ndani na kujidhihirisha katika matendo ya nje). Ndiyo maana Biblia inatuambia, “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.” Mithali 4:23
Tunapaswa kuwa makini hapa kwa sababu Yesu hasemi kuwa vitu vyote vinaruhusiwa au vinafaa kuliwa. Hapa Yesu hazungumzii wanyama najisi na safi. Mada yake ni juu ya chanzo cha unajisi wa kimaadili/kiroho. Yesu anatumia kielelezo cha vitendo vya nje kama kuosha mikono na kula ili kuweza kutofautisha na hali ya moyoni. Yesu hugeuza mtazamo wa walimu wa sheria: walikuwa wamejikita katika mambo ya nje, wakati Yesu alisisitiza matendo ya ndani ya roho, hali ya kimaadili/kiroho. Kwa wengi, ni rahisi kudumisha hali ya nje ya kuwa Mkristo kwa kile tunachofanya au tusichofanya. Hata hivyo, wakati ambapo wanadamu huangalia nje, Mungu huangalia hadi ndani ya moyo—hupima nia na makusudi yanayosukuma matendo yetu. (Rejea Mwanzo 1:29-30; Matendo 10; 1 Wakorintho 10:31; Mathayo 5 :28, 29).
Watakula hadi ya kenge, ukiwauliza Baba askofu gwajima amesema tule kila kitu,Madhara ya kakaririshwa badala ya kuelewa maandiko ndo haya
Na kwa umelo huu watu mtajikuta mnakula hadi nyama za watu hakyanani...!!!
Tofauti yako wewe na wakristo wa zamani.waliowekewa mipaka ya vyakula ni nini??naona unajaribu kujenga hoja kwa kuangalia tu nyaraka za paulo, vipi kuhusu Yesu kwenye marko 7 : 18-22? hapo unasemaje. alivitakasa si tu vyakula bali na vinywaji. #si kimuingiacho mtu bali kimtokacho ndicho kinacompa mtu unajisi# biblia ipo wide mkuu usijaribu ukiitafsiri ukiwa closed minded but try to be opene minded.
Kwa hiyo Mungu akisema kuwa kuna vyakula najisi anaweza kusema tena kuwa hakuna Vyakula najisi mungu huyo wa hivyo anajichanganya sana.