Je, Bashiru ni Bepari au Ni Mjamaa Uchwara?

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
2,030
3,908
Aliyekuwa katibu mkuu kiongozi,katibu mkuu wa CCM na balozi asiyekuwa na Portfolia Mh Mbunge kwa sasa Dr.Bashiru Ali na ambaye alikuwa mhadhiri katika chuo kikuu cha Dar es salaama kabla ya kutwaliwa na mwendazake pamoja na wengine waliotwaliwa kutoka Jalalani na kupewa nafasi ya kuwa watumishi wa kisiasa ndani ya chama na Serikali.

Binafsi namfahamu Bashiru kama Mwalimu pale UDSM lakini pia nimefahamu katika majukwaa mbalimbali kama makongamano ya UDASA ambayo naona sasa yamepigwa marufuku.Katika kumfahamu Bashiru sikuwahi kumuona kama Mjamaa kwa namna yoyote ile.Hakuwa na mtazamo wa kijamaa na wala hakujipambanua kwa uwazi kwa maneno na matendo kama mjamaa.

Kwangu mimi Dr.Bashiru ni Mjamaa Uchwara,ni bepari ambaye hana ujasiri/mwenye aibu na woga ambaye anajificha nyuma ya kivuli cha Ujamaa ili apatapo ujasiri wa kujipambanua basi atuoneshe Ubepari wake halisi.

Katika zama za Bashiru kama katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi sikuona uelekeo wa chama kuwa cha kijamii kwani bado kilikumbatia ubeberu na uzandiki huku yeye na mpiga pambio mwenzake Polepole wakiwa vinara wa kuwalisha watanzania Upepo wa ujamaa huku wakiwananga kwamba hawaifahamu V8.

Binafsi nashangaa sana hata hatua ya Mh.Rais kumpeleka Bashiru Bungeni.Ameenda Bungen kufanya nini?Maana hata katika kufanya maamuzi hatakuwa na msimamo wa kijamaa wala wa kibepari bali atatafuta namna ya kujificha nyuma ya wengi au nyuma ya wenye mamlaka .

labda kwa wale wanaoamini kwamba Bashiru ni Mjamaa watueleze Ujamaa wa Bashiru ukoje hasa.Ni Ujamaa tunaoufahamu au ni ujamaa ambao anaufahamu yeye tu?
 
Bashiru amekariri ma- theory ya kijinga ya akina Max na Lenin kisha akatoa ka- theory kake ka kijinga eti " UNYERERE" !

Hayo mapumba ndo walimjaza Hayati Magufuli yeye na Prof. Palamagamba Kabudi ,Magufuli akawa neno Mabeberu halikauki mdomoni mwake!
Ona sasa kwa uoga wa Mabeberu wa kufikirika Rais Magufuli amekufa kwa kukosa huduma bora za matibabu alizokuwa anastahili na badala yake Rais Magufuli kwa huzuni ninaweza kusema amefia mikononi mwa "waganga wa kienyeji" akiwemo huyu Professor Mabula Michembe!
 
Back
Top Bottom