SI KWELI Je, Barabara hii ipo nchini Nigeria?

SI KWELI Je, Barabara hii ipo nchini Nigeria?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
1774688442198.png

1774688469513.png
 
Tunachokijua
Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kumekuwa na picha inayoonesha barabra ikiwa na mikunjo mingi na kuelezwa kuwa ni kutoka nchini Nigeria, ikielezwa ni barabara ya Gembu jimbo la Taraba.

Wadau wa JamiiCheck kupitia Jukwaa la JamiiCheck.com na mitandao ya kijamii na kwa kutumia nyenzo za kidigitali ambapo wamekuwa na majibu mbalimbali huku wengi wakieleza kuwa barabra hiyo haipo nchini Nigeria na badala yake ipo Australia.

Dalton elijah alieleza kuwa:

Kwa kutumia nyenzo ya Google Reverse Image Search, imebainika kuwa picha hii ilipigwa katika eneo la barabara nchini Australia. Barabara hiyo inapatikana Cape du Couedic, ambapo inapita ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Flinders iliyopo kwenye Kisiwa cha Kangaroo. Hivyo, kwa mujibu wa uchunguzi huo, picha hii ya barabara haitokani na Nigeria bali imetoka Australia.

Aidha, kupitia ufuatiliaji uliofanywa kwenye tovuti ya picha ya Flickr, imebainika pia kuwa eneo hilo liko nchini Australia. Maelezo yaliyopo kwenye tovuti hiyo yanaonyesha kuwa picha hiyo ilichapishwa mtandaoni tarehe 1 Juni 2012, ikiwa na ujumbe ufuatao: “On the way to Karijini National Park in Western Australia.”

Mdau mwengine kutoka instagram aliandika:

Nimebaini hiyo barabara ipo Kangaroo Island, South Australia.

Uhalisia wa madai hayo ni upi?

JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa picha hiyo ama barabara hiyo si ya nchini Nigeria kama ilivyokuwa ikidaiwa katika mitandao ya kijamii.

Kwa kutumia google reverse image search imebainika kuwa picha hiyo imekuwepo mtandaoni kwa zaidi ya miaka 10.

1774851179134-png.3564420

Lakini uhalisia ni kuwa picha hiyo ilichapishwa mtandaoni katika vipindi tofauti mathali kupitia tovuti ya Flickr walichapisha picha hiyo mwaka 2012 na kueleza kuwa ni barabara inayopatikana katika kisiwa cha Kangaroo.
1774852047126-png.3564424

Back
Top Bottom