Relevance ya hiyo diploma na diploma nyingine za kilimo kwa kozi ya Agricultural Economics haitokani sana na "How much of a knowledge of Economics is in those diploma courses". Bali inatokana na " hawa (wenye hizo diploma) ndio wenye kilimo chao, kwahiyo tuwaendeleze kimaarifa ili hicho kilimo chao kifanywe kibiashara na kiuchumi", na ndio maana ukiangalia hiyo kozi inatolewa kwenye Chuo cha kilimo (Bsc. AEA pale SUA) na hiyo ya UDSM (Bsc. ANEB) iko chini ya college ya kilimo, vinginevyo ingekuwa chini ya shule ya biashara (UDBS).
Lakini ukiangalia contents za hiyo kozi (Agricultural Economics) utagundua kwamba ni kozi ya uchumi zaidi kuliko ambavyo ni kozi ya kilimo. (It is much economic and less agricultural). Kwahiyo kimantiki, kuhoji hiyo Relevance ya mtu wa diploma ya mifugo (nadhani dhidi ya mtu wa diploma ya uchumi na biashara) unakua uko sahihi kwa namna fulani.
Lakini nikukumbushe tu kwamba kozi za shahada za uchumi kwa ujumla kwa hao wenye diploma za uchumi zimejaa tele huko Mzumbe, UDSM(UDBS), CBE, IFM, na kwingineko. Kuwadahili hawa kwenye Agricultural Economics dhidi ya wanakilimo wenyewe ni sawa lakini si sawa kwa maana ya kwamba "it is right but not fair". Itakuwa ni kama "unawaleta wataalam wa uchumi kwenye kilimo" badala ya "kuleta utaalam (kuwapa utaalam wa uchumi) watu wa kilimo".
Sasa nikujibu hili swali lako;
Je, kwenye Diploma in animal health and production kuna contents za uchumi na biashara ?
Kwa sababu shughuli ya ufugaji ni shughuli ya kiuchumi, na ni biashara pia, hao wenye hiyo diploma huwa wanafundishwa baadhi ya masomo yenye muelekeo wa uchumi na biashara. Nakumbuka kwa uchache wanasoma "Principles of Production Economics and Marketing" na "Livestock Enterprise Establishment and Management".
Suala la kumudu au kutokumudu litatokana na jitihada za mhusika, yote kwa yote Oktoba 2 itaamua.
Kwa lolote karibu.