Bei Rahisi Electronics
Senior Member
- Apr 4, 2025
- 197
- 583
Mimi ni kijana wa miaka kadhaa sijaoa lakini nilikua na mpenzi ambaye sasa tumetengana kwakua kaolewa na mwanaume mwingine. Iko hivi mwaka juzi mpenzi wangu alipata nafasi ya kwenda chuo, mimi naishi Arusha nayeye alienda kusoma Dar, tulikua tunawasiliana vizuri lakini baada ya muda niliona mambo yanabadilika, aliacha kupokea simu zangu, hajibu meseji zangu, nilikua nimempangia chumba nnje ya chuo lakini alihama akisema anataka kuishi chuoni ili kusoma vizuri.
Mimi nilimkubalia na kumuelewa lakini baada ya muda nilikuja kugundua kuwa hakua amerudi chuoni bali kuna mwanaume aliyekua akiishi naye ambaye ni mwanafunzi mwenzake. Iliniuma sana lakini nilipomuambia alibisha mpaka nilipokuja kumfumania, akaniambia hanitaki niendelee na maisha yangu. Kumbuka mimi ndiyo nilikua namlipia chuo, mwaka jana alikua anaingia mwaka wa pili, alikosa ada na kuja kuniomba msamaha, aliniambia ulikua utoto nikamsamehe.
Nilimlipia ada ya mwaka wa pili lakini nilikuja kugundua kuwa alikua na mimba ya yule kijana, alitaka kuitoa ikashindikana ndiyo akaja kuniambia, nilimuambia basi kwakua nampenda nitamsaidia kulea, nikaanza kulea mpaka alipojifungua. Sikutaka kumchukua mtoto kama wangu, alichukua jina la Baba yake ingawa aliniambia kuwa hawapo pamoja, nimeendelea kumsomesha na kumsaidia, mwaka huu anaingia mwaka wa tatu chuoni na anahitaji ada, aliniomba nikamtumia kama kawaida yangu.
Lakini cha ajabu nikua nimemuona rafiki yake kapost picha za yeye na mchumba wangu wapo nyumbani kwa yule mwanaume mwingine. Nilipomuuliza aliniambia nikweli, wazazi wa yule kijana walitaka kumuona mtoto na walipomuona waliwalazimisha waoane huvyo wamefunga ndoa na huyo Kaka kwa madai eti wazazi wake wamamuambia kama hawezi kuoa basi hawamsomeshi tena huyo Baba wa mtoto wake. Ananiambia bado ananipenda lakini wamelazimika kufunga ndoa na mzazi mwenzake akishalipiwa ada basi atampa talaka. Lakini cha ahabi nimefuatilia nimekuja kujua kuwa kumbe wanaishi pamoja na nikimuuliza anasema ni ili kuwazuga wazazi wa huyo mwanaume lakini bado ananipenda na nisubiri wakimaliza chuo wataachana, niko njia panda je ananipenda kweli au ananipotezea muda wangu?