Je, amani ina thamani kuliko haki?

andoza

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
1,610
2,000
Kesho tunaingia kwenye uchaguzi;

Katika tunayoomba yafanyike katika uchaguzi huu ni swala la HAKI kutendeka na AMANI kudumu. Kumekuwa na mjadala wa chini kuhusu AMANI yetu huku wengine wakitaka kuwaaminisha kwamba ni sawa kupoteza amani katika kudai HAKI.

Nianze kwa kusema kwamba HAKI pekee ambayo inaweza kudaiwa kwa kuvunja hali ya AMANI ni haki ya kuwa na AMANI haki nyingine zote haziwezi kuwa na thamani kuliko amani mfano swala la haki ya kuchagua viongozi tunaowataka

Kama wananchi tusikubali kupoteza amani yetu kwa sababu tu ya kudai eti viongozi fulani ndo wanapaswa kutangazwa ila tukubali kupoteza amani iwapo viongozi ambao tunapewa ni TISHIO kwa AMANI YETU.

Sasa nimeshachokoza mjadala. JE, AMANI yetu ina thamni gani? Inatishiwa na nani ili tuwe tayari kupoteza amani ili kupata haki ya kuwa na amani? Tukumbuke kwamba AMNI ikipotea haipatikani tena ispokuwa tu kwa ncha ya upanga tena.

Watumishi wa Serikali hasa majeshi yote waelewa hilo,Wanasiasa nao waelewe hilo.

JE, AMANI YETU INA THAMNI GANI?

Kwa masaa 24 yaliyopita mitandao yote ya kijamii imefungwa,simu na meseji zinakaguliwa,Mawasiliano ya watu yanafuatilia.Kule zanzibar kumekuwa kimya hakuna habari yoyote inayotoka kule.Maana yake ni kwamba kwa sasa nchi yetu imeingia katika GIZA kuu.Je hii ni gharama ya kutafuta hai au kutafuta amani?

Je nani talaumiwa iwapo mambo yataenda ndivyo sivyo?Je serikali inajua kwamba watu wanatazama kila kitu kinachotokea?

Naendelea kuuliza JE AMNI YETU INA THAMANI GANI?
 

Surya

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
5,779
2,000
Wanao piga kelele kua amani itapotea ni wale ambao wamejiandaa kushinda kwa kulazimisha, wanataka watakapokua wanalazimisha ushindi wao, sisi wananchi tukubali na kuinamisha vichwa yani tuwe wapoleeee
Kwa kupigwa kofi shavu la kulia na kugeuza shavu la kushoto.

: Nyie mafisi ccm tunawajua vizuri
 

MAMBOMPANGO

Senior Member
Sep 2, 2009
101
225
Kwa maisha ya kijamii, HAKI na AMANI vinafungamana, vinategemeana. Ni kama KUKU na YAI. Huwezi kupata kimoja kama huna cha pili.
Huwezi kudai HAKI kama huna AMANI; na huwezi kupata AMANI kama hutendi HAKI.

Kwa WATAWALA, kudai haki ni uanaharakati. Ni uchochezi. Ni uvunjifu wa amani. Kwao wao, AMANI lazima ilindwe hata kama wataua maelfu kwa maelfu ya watu, ili watakaobakia, wakiwamo wao, waishi kwa amani.
 

andoza

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
1,610
2,000
Je amani yetu ina thamani kuliko haki?Je HAKI NI NINI?na AMNI NI NINI?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom