Je, aina fulani ya ulinzi inaweza kukujulisha kuwa kuna aina fulani ya adui?

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
30,265
69,511
Bila kwenda mbali jambo hili nalipeleka moja kwa moja kwenye mifumo ya ulinzi ya dunia hasa angahewa(atmosphere).

Angahewa ni kama blanket ambalo limeizunguka dunia huku likiwa na hewa mbalimbali.. Angahewa jinsi lilivyo lina ulinzi kutokana na adui jinsi alivyo!

Kuna aina mbalimbali za mionzi ambayo hutoka nje ya dunia lkn angahewa huizuia mionzi hio moja wapo ni;

Cosmic rays
Hii mionzi huweza kuharibu DNA, pia huleta cancer lkn inapopita kwenye angahewa hukutana na oksijen na nitrojen ambazo huzuia upitaji wake.

Ultraviolet rays
Hii pia huzalishwa na jua lkn kupitia ozon layer huchujwa na kufika hafifu..aina hii ya mionzi husababisha matatizo ya macho na cancer ya ngozi.

Mbali na mionzi angahewa pia hupambana na adui (maada) hapa nasemea vitu kama vimondo n.k kwa kuunguzwa kutokana na msuguano kati ya hewa na kitu hicho pindi kinapotaka kuingia duniani.

Hayo ni machache kati ya mengi sasa tukimuangalia kiumbe binadamu ndio kama mlinzi wa humu duniani iwe gonjwa majanga sisi ndo huwa tunapambana nayo.

Namaanisha kuwa kama kitu chochote kikifanikiwa kupita na kuingia duniani ambacho kitaleta madhara basi directly mpambanaji ni binadamu!

Mpaka hapo tumeshakuwa na sifa ya kuitwa walinzi maana hata magonjwa yakiwapata wanyama(sio yote)binadamu huwatibisha ama kuwasaidia..

Sasa kiumbe huyu akiwa kama mlinzi na kama kichwa kinavyosema (je,aina fulani ya ulinzi inaweza kukujulisha aina fulani ya adui..?)

Kwa jinsi tulivyo na utashi, ubunifu, uyakinifu, ujuzi na maarifa; Je, kuna aina ya adui mwenye sifa kama zetu?
 
Sio aina fulani ya adui pekee,hata thamani ya
Kinacholindwa.

Sio rahisi kukuta askari
wa KK au SGA analinda
Genge la kuuzia michicha na vitunguu
 
Hapana mkuu!Aina ya ulinzi hua inategemea na kitu gani kinalindwa.Mfano kama unataka kumuwekea ulinzi mke wako watu wasimle huwezi kumpa mwanaume ambaye ni kito....mbi akulindie but utampa hiyo kazi PUNGA
 
Sio aina fulani ya adui pekee,hata thamani ya
Kinacholindwa.

Sio rahisi kukuta askari
wa KK au SGA analinda
Genge la kuuzia michicha na vitunguu
Mkuu hapa unatakiwa uangalie aina ya ulinzi sio adui.
hlf unaposema thamani sisi binadamu tunajilinda lkn nani anafaidika au anaona thamani ya uhai wetu pamoja na viumbe wengine..?
 
Hapana mkuu!Aina ya ulinzi hua inategemea na kitu gani kinalindwa.Mfano kama unataka kumuwekea ulinzi mke wako watu wasimle huwezi kumpa mwanaume ambaye ni kito....mbi akulindie but utampa hiyo kazi PUNGA
sasa ukimpa hiyo kazi punga si watamla hao wajanja kwa kumshinda punga!
 
Mkuu hapa unatakiwa uangalie aina ya ulinzi sio adui.
hlf unaposema thamani sisi binadamu tunajilinda lkn nani anafaidika au anaona thamani ya uhai wetu pamoja na viumbe wengine..?
Kila kitu kina sababu
 
Tunalindwa na Mungu tu.
Ambae amewaletea shetani anaewatesa na kuhangaika hovyo,kisha anateuwa viongozi maana yeye ndio mpangaji wa kila kitu leo na kesho mnaanza kuwagomea hao viongozi mnapigwa virungu na mabomu loh!,kuna watu wanaliwa na fisi wengine wanapigwa pembe na ng'ombe wanakufa na hao viumbe wameumbwa na Mungu! hii aina ya ulinzi ndo kwanza naiona kwako!

Mungu alieachia magonjwa,vita na majanga ndo huyo anatulinda au unaota mkuu..?
 
Back
Top Bottom