Je, AC ya gari inatumia mafuta?

Naongelea kitu kama hiki yan unaweka Gar On then unawasha AC je hapa mafuta yanatumika?

Uki start gari najua yanatumika je ukiweka tu on bila kustart gar mafuta yanatumika?View attachment 1541269View attachment 1541268

kwani gari ikiwa silence haitumii mafuta?!

inatumia mafuta japo kidogo sababu haiko kwenye gia so haina mzigo

inapokua silence ukawasha AC unaongeza mzigo wa kusukuma compressor na mfumo mzima wa AC unatumia nguvu ya engine,ndio maana consumption ya mafuta pia inaongezeka

so ukiwasha AC unaongeza matumizi ya mafuta hataa gari ikiwa kwenye silence
 

siyo kwa kiasi kidogo mkuu

AC inachapa wese kinoma noma
 
siyo kwa kiasi kidogo mkuu

AC inachapa wese kinoma noma
Ni kwa kiasi kidogo sana mkuu. Ila sasa kama utakua upo kwenye foleni au kwa namna yoyote ile gari haitembei na umewasha AC hapo lazima matumizi ya mafuta yataongezeka.
Labda tuchukulie mfano unatoka dar unaelekea moro ukiwasha AC au usipowacha matumizi ya mafuta ni almost yale yale. Ila kama unatoka mbezi unaenda mbagala utaona utofauti mkubwa wa matumizi ya mafuta ukiwasha au usipowacha AC kwasababu ya foleni.
 
Kama Hujawasha engine AC haiwezi kuwaka. pale unachokipata ni upepo toka kwenye feni.
 
siyo kwa kiasi kidogo mkuu

AC inachapa wese kinoma noma
Labda ili kutoa elimu kwa njia rahisi, mngetoa mfano kwamba kama gari yako ina average ya kilometre 10 kwa lita moja kwa mizunguuko ya kawaida ya mjini, kama ukiweka AC mafuta yatatumika kwa kiwango hiki kwa kilometre hizo unazotembea au vyovyote vile lakin average ya consumption ya mafuta tuone.

Tukisema inakula sana au inakula kidogo, je ni kwa kiwango gani? Japokuwa kama mtumiaji wa gari nisiekuwa mtaalam shida ya AC ina pale unapokuwa mtu wa "weka mafuta ya buku 5" ila kama ukiweka mzigo hata nusu tank wakati mwingine effect za AC kuhusu kula mafuta hazionekani sana
 
Kama hujui kitu ni vema kunyamaza , maelezo yako yanapotosha
 

Umeongea ukweli, atakayebisha akapimwe mkojo!!!
 
Naombeni kueleweshwa ni kwanamna gan AC ya gar inatumia mafuta

Mfano nikiwa nimeweka gar on bila kuliwasha kabisa alafu nikawasha AC mafuta yanatumika?
Compresser ya AC inategemea mzunguko wa engine kufanya kazi. Iko connected to the engine, ndio inayoizungusha compressor
 
Well, hawa wanasema si kweli....

Wanasema hvyo sabab mafuta yanayolika ni kidogo sana ukilinganisha na full tank. Wenzetu nje magari yao wanaweka full tank or half tank. Ssa sisi tunaoweka mafuta ya buku 20 (aprox. Ltr 10 - 20) lazima hyo tofaut utaniona sabab mafuta yako ni kdg tu.

Pia magar matoleo ya karibun yamepunguza fuel consumption ya compressor na kuna baadhi yanatumia umeme tu kuendesha compressor zake so hayagusi mafuta kabisa. Sasa huku sisi magari yetu mengi ya 2001 mpk 2010 (ya zamani).
 
Naombeni kueleweshwa ni kwanamna gan AC ya gar inatumia mafuta

Mfano nikiwa nimeweka gar on bila kuliwasha kabisa alafu nikawasha AC mafuta yanatumika?
Kuweka switch on bula ku ignite/kuwasha injini mafuta yatatumikaje wakati hayaendi kwenye engine kuchomwa? Sana sana utauwa betri tuu.

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Kama hujui kitu ni vema kunyamaza , maelezo yako yanapotosha
Mimi gari yangu sihitaji kuwasha ili kutumia AC ,labda gari yako ipo tofauti. ukisema napotosha unakosea.
 
Katika majibu ya wadau kuna mambo yanachanganya

Je ac inazungushwa direct na injini au ac inazungushwa na umeme?

Je unapo zima injini lakini funguo ikawa on, ukiwasha ac inayofanya kazi muda huoni ni feni tu au na ac?
 
Mimi gari yangu sihitaji kuwasha ili kutumia AC ,labda gari yako ipo tofauti. ukisema napotosha unakosea.
Huwezi kutumia AC Kama gari imezimwa , labda Kama unatjmia gari za kisasa sana amabazo pia ni ghali sana anyway sijui hilo
Ipo hivi Air condition ni hewa inayotokana na feni kupuliza hewa ya kawaida kwenye barafu, kinachotokea hapo ni obvious utakuwa hewa ya baridi yenye unyevu Fulani, pamoja na Maji ambayo yanayokana na barafu kuyeyuka.

Kitaalamu Air condition ,fridge freezer, zote zinatumia mfumo mmoja, lazima kuwe na compressor, hizi zipo Mara mbili kwa majumbani , huwa ni motor inayotumia umeme,kwenye magari compressor huendeshwa kwa mfumo wa mikanda kupipita engine,

Kiufupi huwezi kupata hewa ya baridi Kama hakuna compressor movements.
 
Kuna baadhi ya magari compressor zake zinatumia umeme so hazihitaji engine. Sema ni model za hivi karibuni
 
Katika majibu ya wadau kuna mambo yanachanganya

Je ac inazungushwa direct na injini au ac inazungushwa na umeme?

Je unapo zima injini lakini funguo ikawa on, ukiwasha ac inayofanya kazi muda huoni ni feni tu au na ac?
Compressor ya AC inazungushwa direct na engine kupitia belt. Kuna baadhi ya magari mapya (newer models) compressor zao hazitumii engine, zinatumia umeme tu so hili linaweza fanya kazi hata gari likiwa kwenye ON position na haitumii mafuta.
Kwa yanayotumia engine kuzungusha compressor ni lazima gari liwe started kabisa na engine inaguruma, ikiwa kweny ON tu ni feni inayofanya kazi na AC iko off
 
Nimekuelewa mkuu na upo sahihi kabisa. Gari za kisasa huitaji umeme tu kuendesha AC kama ilivo kwa friji na AC za majumbani na ndicho nilichomaanisha hapo juu.
Gari yangu imetengenezwa 2016
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…