zee_latown
JF-Expert Member
- Feb 21, 2026
- 521
- 917
Naona ni usiku tulivu na mujarabu kabisa kuweza kuelezea hiki kitu kidogo lakini chenye impact kubwa sana kwenye industry ya uhandisi magari.
kama tulivyo sisi binadamu, tuna mfumo wa mawasiliano(coordination system) ambayo nodes kadhaa zinaunganishwa na zinakuwa zinawasiliana. Na mfumo wa electronic wa gari nao upo hivyo hivyo.
CAN Bus ni kifupi cha Controller Area Network Bus.
gari lolote hasa hizi modern cars ambazo zinatumia mfumo wa obd 2 ku manage shughuli za kielectroniki za gari zima, ni lazima liwe na huu mfumo wa CAN Bus.
zamani kabisa kila sensor kwenye gari ilikuwa inaungwanishwa na nyingine kutumia wire to wire connection. ila CAN Bus imeleta revolution kubwa na leo hii hatutumii tena hicho kitu.
modern car lina control units (cu) nyingi na baadhi ya magari zinafika mpaka 70.
hizi control units ni lazima ziwasiliane na kupeana taarifa kwa sababu kila cu inapokea taarifa kutoka kwenye sensor na kutoka kwenye cu nyingine.
mfano, ecu inapokea taarifa kutoka kwenye Air Conditioner switch katika mfumo wa volt, then nayo inatuma taarifa hizo kwenda kwenye control modules zingine mfano ABS, TCU, BCM na nyinginezo.
Hivyo, unapowasha ac ya gari, ecu inapata taarifa kupitia voltage signal kutoka kwenye switch ya ac, kisha ecu inatuma taarifa hizi kwa control units nyigine zote za gari. na ndiyo maana ukiwasha ac kuanzia kiwango cha mafuta kinachotumika kinaongezeka, pia hata utaratibu wa kubadili gia kwa gearbox za automatic unabadilika. hii ni kwa sababu tcu ya gearbox nayo inapata taarifa kutoka kwenye ecu.
sasa, cu zote zinaunganishwa na CAN Bus, ambazo ni nyaya zilizokuwa twisted, na zipo mbili tu. hizi nyaya ambazo ndizo CAN Bus lenyewe zinapita kwa kila cu na kusambaza na kuchukua taarifa. zimekuwa twisted ili kuzuia efi yanani electromagnetic frequency interference.