JCB wa Arusha awaomba msamaha waislamu duniani kote.

Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Nov 27, 2010
2,591
1,599
Msanii wa kizazi kipya kutoka Arusha maarufu kwa jina la JCB amewaomba msamaha waislamu wote kutokana na kutunga wimbo wenye baadhi ya mistari ya Quran. Kitendo hicho kiliwaudhi waislamu na kusababisha kuwafanya wamtafute popote alipo kwa kuwatumia polisi. Baada ya kusikia ivo, msanii huyo aliamua kujipeleka mwenyewe msikitini na kukutana na viongozi wa dini hiyo ambayo walimuonya na kumtaka amulete mtu aliyemshirikisha kwenye wimbo huo ambaye ndiye aliyeweka hiyo mistari ya quran.
anasema alipompleleka huyo msanii mwenzake, waislamu walimtaka atangaze wimbo huo kuwa ni batili na ni dhambi kuendelea kuusikiliza huo wimbo na ni kinyume na dini ya kiislam.
Kupitia east african radio, msanii huyo amewaomba watu wote wenye huo wimbo waufute na usipigwe popote pale redioni. Pia amewaomba hata watu wenye huo wimbo kwenye simu zao waufute kabisa na wasiuzikilize tena!!!!
Bahati mbaya wimbo wenyewe umefutwa hata kabla mimi sijaupata kwa hiyo hata sijawah kuusikiliza.
Labda wenye wimbihuo wauweke hapa jamvini ili tuuage rasmi.
Source ni East African Radio....Zembwela na Baruti!!!
 
alikuwa anatafutwa na polisi kwa kosa gani? Walikuwa na rb?

Aseeee!!! Wapi Roma mkatoliki.........
alikuwa anatafutwa na polisi kila sehemu alipo...baadae akaamua kujisalimisha mwenyewe msikitini.....
wimbo wake ushawahi kuusiliza? kama unao weka verse zake hapa mkuu......
 
Hivi hizi nyimbo hazihakikiwi kabla ya kutoka? Au COSOTA wanafuatilia filamu tu?
 
ukisikia paa ujue imekukosa aliye lenga hana shabaa amefanya makosa. hizo ni style mya za wasanii wa bongo wanazotumia kujipa promo. hata chid benz alishawahi kusema anaacha mziki. mkuu hamna kitu kama hicho kama hauamin kamuulize baada ya wiki atakuambia hajui aliye sambaza hizo habari. anataka watu wautafute huo wimbo kwa udi na uvumba ili wasikie hiyo mistali. over
 
wimbo huo ni wa long time kidogo nafkiri uko ktk zile mixtape zao FULL ILE LAANA MIX TAPE VOL 3 ni Ibra da Hassla ndo aliyeweka baadhi ya maneno yaliyoko ktk Quran Tukufu ila JCB kaomba radhi na kuutaka ufutwe ila hata hivyo haujasambaa kihivyoo uko kwenye local radio stations kwenye vibanda vya cd studios na kwa baadhi ya watu waloweza kuzipata na kununua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom