Jazanda ya Njozi: Wakiotacho hakina uhalisia

Kisai

JF-Expert Member
Apr 6, 2018
27,984
28,102
Naendelea kuwaamsha walio lala kwa ukelele wenye kukidhi haja.

Siku mbili nyuma nilihudhurisha uzi wenye kichwa au anuani isomekayo "Bahari imechafuka", yakasemwa yaliyosemwa,wengi wakasema nimevuta bangi,wengine nimekula nini ?, waliuliza,yaani wakawa na mshangao na kupuuza ila wapo walio elewa ambao hawa ni wachache na hili ndiyo lengo,waelewe wachache wakawafikishie wengine. Si lazima kila mtu aelewe kila kitu.

Leo nawazindua kwa mada hii yenye anuani "Jazanda ya Njozi". Tamko jazanda ni taswira,waweza kusema picha,yaani kinachoonwa,wapi ? Kwenye njozi yaani ndotoni. Yaani waweza sema "Taswira ya njozi/ndoto". Hapa waswahili tunajimwaya mwaya. Kwenye ndoto mengi ni ya uongo,yaani uongo juu ya uongo. Wakiotacho hakina uhalisia.

Leo hii nawazindua wale wanao ota mchana,tena katika jua la saa sita,sisi husema jua la utosi. Huwa linachoma sana jua hili,kwenye hili wahusika hawajali,wanapambana kwenye hakuna,wabinafsi sana watu hawa, wao ni wachumia tumbo kwa kauli za wengi wape,wao nyuma wameuza mbele wamekopesha,nasema tena nyuma wameuza mbele wamekopesha(mama yangu hupenda sana kusema msemo huu),Mola wangu mpe afya na salama mama yangu kipenzi. Wanapenda kulalamika sana,wengi wao ni wanaume ila wana tabia za kike. Lakini wanasahau ya kuwa kamwe huwezi kupata kivuli kilicho nyooka katika mti ulio pinda.

Nawasalimu sana...!!.
 
Nahisi hakuna nilichoelewa. Kama kuna mwenye uelewe zaidi atufafanulie. Nilichoona mimi ni mbele na nyuma kuuzwa na kukopeshwa.
 
Sidhani kama ni sawa kuweka ujumbe usioeleweka kwa kisingizio cha kukielewa Kiswahili.

Shuleni tulijifunza kuongea kulingana na hadhira, hapa nadhani hadhira uliyoilenga haipo humu
 
Sidhani kama ni sawa kuweka ujumbe usioeleweka kwa kisingizio cha kukielewa Kiswahili.

Shuleni tulijifunza kuongea kulingana na hadhira, hapa nadhani hadhira uliyoilenga haipo humu
Hujaelewa lusudio langu,sijaandika kwa lengo kuelewa Kiswahili,bali nilikusudia kuhusu msamiati mwingi wa Kiswhaili,kwa mfano wa tamko Jazanda la kuwa ni Taswira,yaani Waswahilo tunajimwaya kwa kuwa na msamiati mpana.
 
Back
Top Bottom