Jay Z Producer bora wa wakati wote

MR KADIDY

Member
Mar 26, 2021
67
114
STILL D.R.E - Ufundi wa Mikono ya Jay Z unaoishi tangu 1999 mpaka leo

#UZI

Tar. 13 Feb 2022 ilifanyika fainali ya American Football maarufu km Super Bowl kati ya Los Angeles Rams na Cincinnati Bengals.. Goma lilipigwa viwanja vya SoFi Stadium, Inglewood California.

Kwenye ile fainali kuna show inaitwa 'Super Bowl Half Time Show'

Mwaka huu ile show ilipigwa na wakali wa Hip Hop mainly kutoka West Side..

Kulikuwa na Dr. Dre, Snoop Dogg, Eminem, 50 Cent, Kendrick Lamar na Mary J. Blige.

Wakali kibao walikuwepo uwanjani, kina Meek Millz, Busta, Luda, Lebron na wengine kibao

Kanye pia alikuwepo uwanjani akiwa na mtoto wake North

Ye akili yake anaijua mwenyewe, ila alionekana aki-vibe na mdundo wa still D.R.E baada ya kina Snoop kuanza kukiwasha pale ndichi,

Wakati Snoop anapanda Dr. Dre alikaa kwenye Piano pale jukwaani, baadaye akachukua kipaza na likapigwa dude la 'Still D.R.E'

Uwanja mzima ukazizima kwa shangwe za hatari

Sasa moja ya vitu vilivyovuta macho ya watu, ni uwepo wa Jay Z na mkewe Beyonce pale uwanjani. Km hiyo haitoshi, wakati 'Still D.R.E' inapigwa kamera zikamnasa Jay Z akiimba neno kwa neno.. mkewe Be naye akifuatisha

Walikuwa VVIP km kawa (ki-CEO yaani)

Kitu unachohitaji kufahamu hapa ni kwamba ule mdundo wote uliandikwa na Jay Z tena kwa dakika 20 tuh..

Twende taratibu

Dec. 15 mwaka 1992 Dr. Dre alitoa album yake ya kwanza kwa jina 'The Chronic'

Hii ilikuwa album ya kwanza baada ya Dre kujitoa kundini N.W.A

Album ilikuwa na mafanikio ya kutosha ikifika namba 3 kwenye Billboard 200.. imeshakula platnum 3 (3 million units sold)

Baada ya ile kazi ambayo ilisimamiwa na label aliyoanzisha yeye na Suge Knight, yaani Death Row rec. kwa kushirikiana Interscope(km distributor), Dre aka-chill kidogo

1996 akajitoa Death Row na kuanzisha label yake mwenyewe yaani Aftermath Records..

Baada ya kuanzisha Aftermath Dre akaanza kutafuta gia ya kuondokea sasa (take off)

Akaanza kuandaa album yake ya pili kwa ajili ya kui-push presence ya record label yake mpya

Ukizingatia mafanikio makubwa ya 'The Chronic' Dre hakutaka kufanya kitoto.

Dre akaamua kutafuta manguli wa kuchora mistari mikali ya levo ya 'bazenga' km yeye

Kumbuka hiki ndo kipindi Jay Z alikuwa on fire kinoma baada ya kutoa 'Reasonable Doubt'

Japo Jay amekaa ki-East Coast ila hiyo haikumsumbua Dre.

Kutoka Santa Monica California yaliko makao makuu ya studio za Aftermath Records mpaka New York City katikati ya jimbo la New York yalipokuwa makao makuu ya Roc-A-Fela records ni takribani km 4516

Dre akampigia simu Jay, akamuomba amchoree ngoma kwa jina Still D.R.E,

Mwanetu Jay Z km kawaida kaweka punch za hatari zinazosifia ma-Bentley, ma-Diamonds and like staffs

Jay akadaka private jet iliyolipiwa na Dre kutoka New York mpaka Santa Monica, Los Angeles California kupeleka verse zake.

Jay anatua Los Angeles na moja kwa moja kwenda studio za Aftermath

Studioni anamkuta Snoop, Scott Storch na bazenga mwenyewe Dr. Dre

Snoop yuko kona moja akiwa high na mjani mkononi

Scott yuko kwenye machine anatengeneza beats

Dre yuko jikoni anatengeneza sandwich.

Scott anamwita Dre 'Oya Bazenga, huyu kijana wa New York amefika'

Dre anaitikia 'Poa, nakuja'

Snoop yeye yuko mbingu ya saba hata haelewi kitu, mineli imempanda kichwani

Dre anakuja na bila kupoteza muda Jay anachomoa karatasi kutoka kwenye 'black diary' yake na kumkabidhi, Ndio karatasi yenye verse zote, ya Dre na ya Snoop...

Dre anaiangalia akirejea jikoni chumba cha tatu kutoka studio..

Mpaka anafika jikoni hajaona cha maana kwenye zile lines..

Anamwita Jay na kumwambia 'hamna kitu humu dogo, haya ni mambo yenu ya New York sio Compton'.

Jay akachukua ile karatasi akaichana vipande vipande na kuitia kwenye waste bin ya pale studio

Akasogea kwenye kona moja ndani ya studio, akafungua daftari yake akatoa paper, akaketi, akavuta hoodie yake akafunika kichwa dizaini ile ya Konde boy, akakohoa kidogo ile koh koh koh.

Baada ya dk 20 na ushee hivi akanyanyuka kishujaa km Tyson Fury na kumkabidhi Dre ile karatasi

Dre akaketi kwa dk km 5 hivi, akanyanyuka akampa mkono Jay akisema 'wewe ndie Hov, umeua'

Siku ile ile Scott Storch akaanza kuinyongea ile ngoma beat yake kali,
Nov. 2 mwaka 1999 Still D.R.E ikaachiwa ikiwa km lead single kutoka kwenye album ya pili ya Dr. Dre kwa jina '2001' iliyoachiwa nov. 16 mwaka 1999 chini ya Aftermath Records

Baada ya show ya super bowl juzi, Still Dre imefikisha 1B views YouTube

Give Jay Z his flowers.
 
daaah nilikua naiona hio show kwa vipande tu umenifanya nkaicheki yote...... tukifuka huku bongo ntakua nahudhuria namimi
 
Stori yako nzuri Mkuu lakini Jay Z aliandika "reference track" yaani general idea ya wimbo na sio actual lyrics. Ndio maana kwenye writing credits wamo Yeye, Dre, Snoop and Mel Man.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom