Jasusi Honda ndani ya mpango wa Congo

Duh hongera sana hii kitu ni balaa
Riwaya: Mpango wa Congo


Sehemu ya kumi na moja



Mtega nyoka akavuta hatua kujipitisha karibu yao, lakini kabla hajawafikia tayari walikuwa wamekwisha kuongozana kutoka eneo lile.

“una nini Malima!!” alijisemea Mtega nyoka huku akiangaza huku na huko ili aone kama kulikuwa kuna mtu mwingine aliekuwa anafuatilia nyendo za kijana yule.

Alimuona!!

Macho ya Mtega nyoka, yalibahatika kuona muinuko wa kijana mwingine ambae kwa macho yake yaliozoea wahalifu, haraka akabaini yule hakuwa mwema kimtazamo.

Nae hakutaka kungoja akainuka na kufuata ulekeo alioona kijana mtanashati ambae alimtambua kama Malima akielekea na binti mwingine ambae hakumjua.

Macho ya Mtega nyoka yalikuwa sambamba kabisa na kijana mwingine aliekuwa akifuatilia hatua za Malima.
Kila kilichofanywa na kijana yule kilionwa vyema kabisa na Mtega nyoka.

Mazungumzo Kati Malima na binti, yalikuwa yanedumu kwa zaidi ya dakika nne kisha Malima akatoa ufunguo wa gari mfukoni mwake na kumuita kijana mwingine aliekuwa karibu na pale walipokuwa na alipofika akamkabidhi ufungo kisha akampa maelekezo kijana yule alieonekana kuwa ni dereva wa Malima.

Malima alipokwisha kutoa maelekezo, akaanza kurudi alikoacha wenzie wamekaa na dereva wake na yule binti wakapanda gari na kuondoka pale.

Yote yalitizamwa vyema na Mtega nyoka na pia hakuacha kutazama nyendo za kijana alieonekana kumfuata Malima.

Wakati Malima akiungana na wenzie na yule kijana akarudi kukaaa alipokuwa awali huku macho yake ya wizi yakiwa hayabanduki kwa Malima.

Muda si muda ukafika muda wa kuaga marehemu na ni muda huo ambao Mtega nyoka aliona unamfaa zaidi kumtumia yule kijana kuliko kumsubiri Malima.

Haraka akamsogelea na taratibu akamfikia yule kijana na kwa upole tu akamwambia;

“Tafadhali ndugu naomba msada wako”

“msada gani” aliuliza kijana kwa mashaka.

“aah ni pale kwenye gari yangu kuna kishida kidogo, yani dakika moja tu ndugu” alizidi kubembeleza na kusihi Mtega nyoka.

Kijana bila kujua hila alizowekewa akakubali huku akitoa tahadhari ya kuwa isizidi dakika moja.

Waliongozana kuelekea kwenye sehemu kulipokuwa kumepakiwa magari mengi zaidi, na Mtega nyoka ndie alitangulia ili kumpa kujiamini yule kijana.

Mtega nyoka alipohakikisha wamepotelea katikati ya magari akageuka gafla na bastola mkononi na kumstua kijana aliebaki ameganda kwa sekunde kadhaa bila kuamini anachokiona.

“Geuka bila ubishi la sivyo kunageuka msiba wa pili hapa” akaamuru Mtega nyoka na kijana akatii bila shuruti huku nae akipiga hesabu za kumvaa mtu yule asie mjua.

Kugeuka kwake likawa kosa!!
.
Kwa kasi ya aina yake, Mtega nyoka akaachia pigo kwa kutumia ubapa wa kiganja na kumpiga nyuma ya kisogo na kijana akaenda chini akiwa hana fahamu.
Mtega nyoka akatazama kushoto na kulia asione mtu aliemuona, haraka akaingiza mkono mfukoni na kutoka na waya mwembamba akaingiza kwenye kitasa cha mlango wa gari nao ukaachia bila kupenda haraka akajitosa ndani na alichofanya huko anajua yeye na punde gari likawaka na akashuka na kumuingiza yule kijana kisha akatokomea na gari la watu huku akiwa na mateka wake.

Akiwa njiani alituma ujumbe kwa Kinyonga ambao ulisomeka;

“Kitalu gani kina mwanya?”
Punde akapokea ujumbe kutoka kwa Mzee Kinyonga.

“Kitalu 1b G” akausoma na hapo alijua anapaswa kuelekea Gedeli kulikokuwa na nyumba ya usalama wa Taifa maalumu kwa kazi za dharura.

Aliamua kupitia mitaa ya Neshino kisha akaipata Gedeli na huko akanyoosha hadi alipokutana na kibao kilichoonesha mbele kuna nyumba inayotumika kufundishia watoto.

Akafika hadi kwenye nyumba hiyo kisha akapiga honi mbili na kusubiri.
Punde akatokea kijana aliekuwa na vitabu na chaki mkononi ikionesha ametoka kufundisha muda si mrefu.

Walitazamana kwa muda kisha Mtega nyoka akasema kwa lugha tata kueleweka.

“Nina guta hapa linahitaji kushushwa oili chafu tafadhali”

Kijana aliekuja akawa makini kidogo kisha akaangaza kushoto na kulia afu akasema;
“Sukutua tafadhali” akiwa na maana apewe utambulisho.

“Siku ya mwisho ndio kwanza” akasema kwa kujiamini Mtega nyoka.

Haraka kijana yule akampa ishara na ya yeye akatangulia kufuangua mlango ulikouwa umejengwa kienyeji tu ambapo ulitumika kuficha geti kubwa lillokuwa linaingia kwenye nyumba kubwa iliokuwa imepakana na lango la kuingilia kwenye darasa la watoto lililokuwa linafundishwa na yule kijana

Haraka haraka Mtega nyoka akaingiza gari na geti likafungwa kisha haraka haraka wakasaidiana kumtoa kijana ambae bado alikuwa hana fahamu na kumuingiza ndani.

Bada ya kuhakikisha Mtega nyoka amepata kila zana alioihitaji,kijana yule akaondoka na kurudi kuendelea na darasa la watoto ambao wakati huo walikuwa wameanza kupiga kelele.

Baada ya kupata kila alichokihitaji, Mtega nyoka akafungua kisanduku kidogo kilichokuwa na zana kadhaa za kutesea na dawa za hapa na pale kisha akachukua kichupa kidogo na kukizungusha juu kwenye mfuniko na kikatoka kitu kidogo mfano wa kidole cha mtoto na kilipotoka kiasi alichotaka akapiga hatua na kumfikia kijana ambae hadi wakati huo hakuwa amerejewa na fahamu.

Kile kichupa akakisogeza hadi karibu na pua za yule kijana na hazikupita sekunde kadhaa kijana akapiga chafya mfululizo kisha akatulia kujipa utulivu na alipotulia akakutana macho na Mtega nyoka ambae muda wote alikuwa kimya akimtizama.

“Hizi silaha ulikuwa nazo za nini?” lilikuwa swali la kwanza la mtega nyoka huku akimwonesha bastola na kisu kidogo cha kukunja.

Kijana akabaki kimya bila kujihangaisha kumjibu.

“Je unazimiliki kihalali au unazitumia kimagumashi?” akauliza tena Mtega nyoka.

Kijana akabaki kimya tu.

Hakujua akili ya mtu alie mbele yake ni ya aina gani.

Haikumchukua muda akatambua mtu aliembele yake ana akili gani.

Kwa kutumia kisu kile kidogo alichokichukua kwa yule kijana wakati alipomkagua akakishindilia kwa nguvu kwenye upaja wa mguu wa kushoto wa kijana yule na kufanya apige kelele ya maumivu huku akifurukuta kwenye kiti alichokuwa amefungwa bila mafanikio.

Na haikuishia hapo akamchana suruali na kufanya kijana abaki na pensi tu huku damu zikizidi kutiririka kama bomba la mvua.

Mtega nyoka alikisogeza kisanduku na kutoa kichupa kingine kilichokuwa na dawa ya unga na akaimiminia kwenye jeraha.

Dawa ile ilipokutana na damu ikaibadilisha kuifanya iwe kama ya njano na kutoa povu na ilipoingia kwenye jereha sawa sawa ikawa kama inachemka na kitendo hicho kilipelekea maumivu makali kwa yule kijana alijikunja huku akipiga ukunga kama mwanamke bikira akibikiriwa na mkuyenge inchi kumi na mbili.

“Haya sasa nambie unamiliki vipi hizi silaha” aliuliza tena Mtega nyoka.

“Mi sijui bana” alijibu kwa maumivu makali yule kijana.

“kwani sio zako?” alisaili tena Mtega nyoka.

“Nimepewa tu!” alijibu

“na nani”

Akaendelea kukugumia bila kujibu.

“Nani kakutuma na kwa kazi gani?” aliendelea kuuliza na hakupata majibu.

Kama kawaida yake, yeye huwa si muongeaji sana zaidi hufanya vitendo tu.

Akachukua praizi na kukishika kidole cha mwisho mguuni mwa yule kijana kisha akakibana na kukipasua katikati.

Mamumivu aliyayapata kijana yule hayaelezeki, alilia kwa uchungu bila kupata wa kumsaidia na bado aliziona harakati za Mtega nyoka aliekuwa anajiandaa kumwekea dawa ile ya unga ikabidi aombe kusamehewa.

“haya bwana mdogo sema na usijaribu kunidanganya kabisa huwa siongei wala kubembeleza” Alitahadharisha Mtega nyoka.

“Nilipewa na Amokachi!” akajibu kijana.

“Amokachi” akarudia kulitaja lile jina.

“kakutuma uifanyie nini”aliuliza tena Mtega nyoka..

“kujilinda wakati nikimfuatilia Malima”


“Alikwambia kwanini umfuatilie?”


“Hapana hajawahi nambia”

“Umefanya nae kazi muda gani?”

“Hii ni mara ya pili”

“Mara mbili;hivyo inaamana mmejuana muda si mrefu”

“ndio”


“Nani kawakutanisha?”

“Sukuna ndie alietukutanisha”

“kwa hiyo wewe upo chini ya Sukuna na unaripoti kwa Amokachi”

“ndio”

“Kati ya hao ni nani rahisi kumpata?”


“Wote sio rahisi”

“kwanini?”

“kwa sababu wanaishi kama Muhanga”

Mtega nyoka akaguna kisha akamtazama yule kijana aliekuwa amekaa kwenye kiti kwa kujipinda kwa sababu ya maumivu pajani na kidoleni.

“unazijua tabia za Muhanga kweli?”
Aliuliza kwa kustajabu kidogo.

“Muhanga ni mnyama asieogopa chochote katika maisha yake,huishi kwa kuvizia makazi ya wengine kisha hujitosa jumla jumla, Muhanga haogopi kabisa hatari yoyote,lakini sifa yake kuu ni kutokuonekana hovyo na anaweza kuishi Mwanza huku akiwa na choo Bariadi sasa ni juhudi zako kumtafuta” alifafanua kijana.

Mtega nyoka alimtizama tena bwana mdogo kisha akatikisa kichwa.

“Kwa hiyo maeneo yenu ya kukutana ni wapi?”


“tunapokea simu tu bro lakini mara chache sana huwa tunafika Club D!”

“iko wapi?”

“Hata mimi sijui kwa sababu huwa tunafika tukiwa tumezibwa macho na masikio, tunapokea oda kisha tunarudishwa hivyo hivyo”

Alipigwa na butwaa Mtega nyoka kisha akazunguka kidogo ndani ya chumba walichokuwamo na alipotulia aliuliza;

“kwa hiyo huwa mnatumwa kazi gani”

“Tumegawanywa na kila mtu na kazi yake na haturuhusiwi kuingiliana kikazi, mimi ni Tracer,lakini kuna Transporter, kuna Helper na kuna killer”


“kwanini mnafanya yote haya?”

“Huwa haturuhusiwi kuuliza, sisi tunafanya tu na pesa inaingia”

Mtega nyoka alimtizama kijana yule mdogo kisha akashawishika kuuliza jambo.

“kwanini wewe umenambia haya mana nikikutazama naona ulikuwa tayari kabisa kufa ila si kusema haya wala sitaki kuamini ni kwa sababu ya mateso yangu”

Kijana akatabasamu kisha akaongea kwa upole.


“kwa sababu nataka kutoka kufanya kazi hii, siipendi ila Sina namna imenilazimu”

Mtega nyoka akamtazama tena kijana yule na hapo akaona jambo lingine tena ambalo mwanzo hakulitilia maanani.

“wewe ni Mtanzania?”

“Hapana mi nilikuwa Mkimbizi tu vita ya Burundi, baba na mama walifia njiani wakati tukija Tanzania na mimi na mdogo wangu tulichukuliwa na kutenganishwa ambapo yeye alipelekwa kituo cha wakimbizi Kigoma na mimi ndo nikaishia kuwa mfanyakazi wa ndani wa Sukuna na badae nikafunzwa utracer yani mimi kazi yangu ni kufuatilia nyendo za mtu anaeshugulikiwa na kikundi cha sukuna na nikishapata habari na nyendo za kutosha basi kazi inaweza kuishia kwa killer au ikiwa na mlolongo basi Transporter na Helper huhusishwa.”

Alisema kijana yule ambae alijitambulisha kwa jina la Zanu.

Zanu akaona mduao alionao Mtega nyoka na akaamua kuomba jambo.

“Kaka bila shaka wewe ni usalama wa Taifa,na najua kanuni zenu huwa ni kutokujulikana na kwa njia yoyote na first rule ni kuto attract attention lakini pia key rule ni kutokutoa taarifa ama kuvujisha taarifa zenu, hivyo kaka mimi nimefunzwa kama nyie hizo sheria zote ila nimevunja na kukwambia hayo hivyo sitaki wala sifikirii itokee ule msemo wa wanausalama kwamba “trust will get you killed” hivyo sitegemei kuuwawa na mkono wako ila naomba unisaidie nisirudi tena mikononi mwa Amokachi na Sukuna niweke hata gerezani ila si kunifanya nikarudi mikononi
Mwao.”

Mtega nyoka akamtazama Zanu na moyoni mwake akajiridhisha na maelezo ya Zanu japo nae moyoni alijiwekea tahadhari ya trust will get you killed.

“sawa utaendelea kuwa hapa hadi nitakapokupa maelekezo mengine ila utaendelea kuwa mateka japo hautafungwa” alisema Mtega nyoka huku akianza kutoka ndani ya chumba cha mateso ndani ya nyumba ile ya usalama wa Taifa.

Alifika hadi sebuleni na kumkuta kijana wa usalama aliempokea.

“utamhudumia yule dogo na umtoe kule na mpeleke room C ila kuwa makini nae si wa kuchekea kwa sasa and remember one thing trust will get you killed” alimalizia maneno yake kisha akaanza kutoka nje ila kabla hajaufikia mlango wa kutokea kijana yule akamwambia;

“Nipo makini pia komredi na akizingua nitamkumbusna kitu hiki “time spent in enemy hands is the same as becoming the enemy himself”

Huo msemo maarufu katika tasnia ya kishushu ulimfanya Mtega nyoka atabasamu huku akkmalizia kuufunga mlango huku lengo likiwa ni kuipeleka gari alioipora msibani kituo cha polisi ili irudi kwa mwenyew kisha aanze rasimi msako wa kumtafuta Sukuna kisha Amokachi na sehemu pekee ya kuwapatia watu hao ni Club D.

Tatizo sasa hajui ilipo.

****


Ahsanteni kwa Maoni yenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom