Pascal Mayalla Haya Mataifa hayawezi kuunga mkono juhudi za Mh. Rais, hasa pale ambapo tunaanza kufanikiwa katika kuwabana wanyonyaji wa maliasili zetu. Watakuja na kila aina ya propaganda, na watatumia vyombo na taasisi zao kutuchafua. Mambo ya aina hii yamekua yakitokea sio tu kwa Tanzania, tumeona propaganda za namna hii zikienezwa kwa nchi nyingine zilizokataa unyonyaji wa mataifa ya maghalibi na zilizoamua kusimamia usawa katika kusimamia maliasili za nchi.
Sisi watanzania hatupaswi kurudishwa nyuma na propaganda dhaifu kama hizi, inafaa tusimame kwa pamoja, tumuunge mkono Mh. Rais wetu, na tuendelee mbele. Tanzania ki uhalisia tulihitaji kiongozi wa kaliba ya Mh. Magufuli, sasa tumempata tumtumie katika kipindi hiki cha miaka 10 na tutafikia pazuri.