Jaribu kukua kifikra

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Wakati nasoma ushuhuda wa yule binti wa Mbinguni na kuzimu miaka 10 nyuma, kuna vitu viliniingia kichwani.

1. Kamwe usimwamini binadamu. Kitu cha kwanza unachotakiwa kujua binadamu si malaika. Kila binadamu ana maisha ya pande mbili, kuna upande wa kwanza unaoujua, upande mwema lakini pia kuna upande wa pili usioujua.

Niliangalia suala la Papa John Paul. Sikuweza kubishana nalo kwa sababu yule ni binadamu, ana tamaa ya madaraka kama binadamu wengine, ana tamaa ya pesa kama wengine, ana tamaa za kidunia na mambo mengine mengi tu.

Kuna wachungaji wengi, hujawahi kusikia kwamba mchungaji amefumaniwa anazini? Hujawahi kusikia mchungaji anashutumiwa kwa wizi? Leo mtu aliibuka na kusema ule ulikuwa mkono wa baunsa, waumini wakamwamini, lakini wakasahau kwamba yule alikuwa ni binadamu kama wengine.

Ukijiona huna tamaa, wewe bado hujakamilika, binadamu ni lazima uwe na tamaa, uwe na kiburi cha ndani. Wewe si malaika. Sasa kuna watu ukiwaambia mchungaji fulani ama shehe amefanya hivi na vile, mtu anashupaza shingo na kusema haiwezekani. Bro! Kwani yule si binadamu?

Ukisoma Biblia, shetani alimjaribu mpaka Yesu. Yaani Yesu alijaribiwa, vipi kuhusu wewe? Shetani atashindwa kukujaribu kisa papa ama mchungaji, ama shehe? Yesu aliyashinda kwa kuwa kulikuwa na nguvu kubwa sana ndani yake, je, nguvu aliyoishinda Yesu kuna binadamu anayo?

Mimi simwamini mtu yeyote yule. Hata mchungaji wangu simwamini. Siku hata nikiona mchungaji kafumaniwa wala sitoshangaa, kwa nini? Ni kwa sababu nao ni binadamu.

Kuna watu wana maisha ya siri ambayo ukiyasikia huwezi kuamini hata kidogo. Unaweza ukaambiwa ukasema haiwezekani, yule hawezi kufanya hivi. Ndugu yangu, acha kuwaamini sana viongozi wa dini, fungua akili yako uendelee kujua kwamba wale ni binadamu kama wewe, wanajaribiwa sana, kama Yesu alijaribiwa, wachungaji na mapapa akina nani hadi wasijaribiwe?

Ushuhuda wa yule binti ulinifungua vitu vingi sana. Nilipata shuhuda mbalimbali za hivyo, wote walioongea, yanafanana, yaani hakuna mtu ambaye alisema tofauti na mwenzake. Yapo vilevile.

Sasa mtu anashupaza shingo na kusema haiwezekani, kwa papa nakataa! Papa mmemuona ni Mungu? Papa na Yesu unadhani nani alikuwa na nguvu kubwa? Nani alikuwa na wafuasi wengi? Nani alikuwa na uwezo wa kutenda miujiza? Jibu lako litakuwa Yesu, sasa kama Yesu alijaribiwa na shetani, kwa nini papa asijaribiwe? Hebu fikiria kwa kutumia kichwa.

Acha kuabudu binadamu kwa kuwaona ni malaika. Nao ni binadamu, wanatenda dhambi, wanaanguka dhambini, na wanatubu dhambi zao.
 
Kama una link 🖇️ ya huyo binti nitumie boss ni vizuri na mm nikajifuza japo machache🙏🏿
 
Back
Top Bottom