Jaribio lingine la Clouds kutaka kumshusha Diamond na WCB

Jaribio lingine la Clouds kutaka kumshusha Diamond na WCB

fasiliteta

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2014
Posts
2,598
Reaction score
4,471
Niwe wazi kabisa kuwa Clouds ni watu hatari sana katika tasnia ya habari na ukandamizaji wa mafanikio ya watu mbalimbali pindi wanapokosa maslahi yao, ni watu wenye uchu wa unyonyaji haswa na kutumia vyombo vyao vya habari vibaya mno, nawasihi wizara wawaangalie sana hawa jamaa kwa unafiki wao na majungu wakiyatumia katika vipindi vyao kuwakandamiza wengine.

Ikumbukwe kua mwishoni mwa mwaka jana hawa jamaa walianza kutokupiga nyimbo zinazowahusu WCB, kama ilivyo desturi yao pindi wanapohitaji kulambwa unyayo na binadamu wenzao, mlolongo wa matukio wa umungu mtu huu unaonekana umegonga mwamba katika ulimwengu wa hawa WCB kwani mpaka watu wanakuja kugundua hili mwanzoni mwa mwaka huu kumbe nyimbo hazipigwi muda mrefu na jamaa bado walikua wanaendelea kutusua katika anga la burudani.

Ujio wa station ya redio na TV ya WCB imeonekana ndo kuwachanganya zaidi mpaka sasa kuonyesha chuki za wazi wazi huku pasi na shaka wenzao wakiendelea kunyamaza na kukaa kimya kabisaa.

Sasa wamemzuia hata huyo Millard Ayo ambaye habari zake nyingi za WCB zilikua zinampa view nyingi na kumuongezea mapato yake binafsi na kuonekana sasa naye si mwana habari huru kama alivyokua akichukuliwa na jamii kubalance habari, ati hata Diamond kupokea nafasi ya kutumbuiza world cup hajawahi kuitangaza(maajabu ya ulimwengu wa sasa haya, atangaze ndondo cup waache world cup, nacheka sana)

Hapo Clouds wamekua kama misukule ya bwana Ruge Mutahaba, kila anachotaka wao ni kufuata tu.

Walijaribu pia mwezi wa pili kumbeba na kumpromote sana Aslay kwenye show yake, lakini hasara waliyokula nafikiri imewazidishia machungu sanaaa, sasa hivi naona wamepunguza hiyo ujinga yao na maskini mtoto wa watu uwezo wake bado unakua ukambebeshe mzigo wa kumpiganisha na mtu ambaye amekomaaa barabara katika muziki na very talented kama Diamond (naona wamemshindwa tena).

Wamejaribu kumuandika kwenye page zao za kike za kina Soudy brown, zaidi ya matusi hakuna walichofanikisha. Kimsingi wamegonga mwamba na sasa hili la kuletwa Zamaradi na kina mama Wema WCB TV/redio limewazidishia donda ndugu kabisa.

Sasa juzijuzi wameona BASATA kujitokeza kufungia nyimbo za wasanii, wameona kama chance sasa na kinachowashangaza watu ni kushadadia watu kufungiwa wakimlenga Diamond kumbe kuna wengi zaidi wanaumia(unafiki wa Clouds ni waajabu sana, ukianza kula nyama za watu always hutoacha).

Huku wasanii wenyewe wakihitaji kwenda kuonana na wahusika kujua hatima ya nyimbo zao walizozipambania, Clouds wakatarget ambayo Diamond anazindua album yake wakamualika naibu waziri huku wakimuuliza maswali ya kitoto/kinafiki kabisa.

Yaani mpaka inachekesha hawa Clouds na ukubwa wao wanaojitapa wanahenyahenya. Hata mtoto mdogo angemuuliza naibu waziri, mna mchango gani kwao zaidi ya kufungia nyimbo zao tu, na mmetumia maudhui gani kuzifungia na si kurekebisha?.

Wamekaa wanajichekesha, ati waziri kasema nyimbo hairuhisiwi kupigwa hata nje ya nchi, wao wakijua msanii mpiga nje ya nchi zaidi ni Diamond, basi wamesambaza sana kwenye page zao za social media(njia ya mnafiki ni ndogo sana, kamwe haichukui muda kumgundua) tena wakaona hasimu wa Diamond kibiashara katajwa basi wamesambaza mno.

Wenye akili wanaelewa kinachoendelea, watu wanajiuliza huku kutapatapa kwa Clouds nini maana yake, mbona wamewafanyia figisufigisu nyingi wasanii wengi huko nyuma lakini haikua namna hii, wana ajenda gani zaidi?

Huyo Mwarabu fighter (mlinzi wa Diamond ndo muda wake sasa wa kutoa ulinzi haswa)

Jamaa nasikia wana madeni lukuki wanadaiwa na Serikali, mishahara nayo imekua mtihani sasa kwa wafanya kazi wao, matangazo nayo yamekua mtihani sasa, hata zile tenda za dezo walizokua wanazipata toka Serikalini naona zimekata. Kila mtu akomae na hali yake.

Ushauri wangu kwao tu, kabla hawajaelekea shimoni zaidi panapoonekana wazi kwa sasa, basi wajitathmini sana katika kuact kama kituo cha habari na si genge la wanyonyaji na wanachuki, wana baadhi ya vipindi kama sport extra, ni kizuri japo shafii naye hulalamikiwa lakini bado ni kizuri sana

Huyo Millard Ayo anajitahidi kujitengenezea jina yake vizuri, basi wamuache awe huru kwa namna yake na si kuonekana ameshikiwa akili pia na Ruge.

Zaidi ya yote niwakumbushe hadithi ya mua uliozamisha meli kisa nahodha kanogewa, Ruge fanya tathmini usinogewe sana, jahazi linazama.
 
Na diamond kawajibu kuwa yeye ni mma kama si kuyaoga basi utayanywa binafsi nimependa sana mondi coz ameonyesha kujiamani kwake...mwache ruge aendelee kujifanya" God father" ila ajue kila kitu kina mwanzo na mwisho wake ....
 
Si mnasemaga diamond ni mkubwa kuliko iyo redio pili anaanzisha radio yake hapo tatizo liko wap na je kwani lazima clouds wapige nyimb za diamond mbona kuna radio huku zinapiga nyimbo za huyo msanii kila dk mbona sioni mkizisifia??
INAMAANA HUONI FITNA ZA NJE SASA NA KUTUMIA WATU,USIPIGE NYIMBO SWA.HYA UTUMIE NA MBINU NYINGINE KUMDESTROY MWINGINE HAPO NDIPO TATZO
 
Acha kulialia Kama Clouds wanagoma kupiga nyimbo za WCB tatizo liko Wapi?

Pelekeni huko Wasafi TV and Radio zikapigwe 24hrs/7days
Hahahaaa kawaambie ndugu zako fitna zinamwishooo,wanatafuta refa wa Pili hao clouds uwanja umewashinda
 
Hiyo inaitwa NGUMU KUMEZA,
Mbona mashabiki wa lady jaydee hawalalamiki kulikoni nyie Wcb
Tatizo mlishazoea promo sana dadeki zenu ngoja tu wawapige pini hivyo hvyo
Halafu Nyie Mna radio na tv station jipigieni promo kene vituo vyenu kenge wa blue ninyi mnaleta mashauzi kumbe bado mnahitaji kubebwa
 
Jana kapeform wakawaka sasa sijui yula Dada waziri atasemaje,ila Millard wanamharibia kwa sababu yeye anategemea sana view alafu inamfanya kuwa sio mwanahabari huru.
 
Hiyo inaitwa NGUMU KUMEZA,
Mbona mashabiki wa lady jaydee hawalalamiki kulikoni nyie Wcb
Tatizo mlishazoea promo sana dadeki zenu ngoja tu wawapige pini hivyo hvyo
Halafu Nyie Mna radio na tv station jipigieni promo kene vituo vyenu kenge wa blue ninyi mnaleta mashauzi kumbe bado mnahitaji kubebwa
Wanabebwa hawa wc si lolote
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom