Jaribio la kugawanya vyama vya siasa Tanzania kutokana na misimamo ya siasa

bahati93

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
1,131
2,008
Mwanadamu kama mwanadamu waweza mtafsiri kama mnyama anayefanya siasa. Binadamu na maisha yake hapa duniani lazima afanye siasa, kwasababu siasa haikwepeki. Hii siasa yatokana na asili ya mwanadamu kushirikiana katika mambo tofauti. Hivyo, ili mwanadamu kuepusha kuishi kama wanyama pori wanaoishi mwituni bila sheria analazimika kukabidhi nafsi yake chini ya mamlaka ya serikali.

Serikali kazi yake kuu ni kutunga sheria na kuzisimamia kuhakikisha hamna mwanadamu ambaye anaishi nje ya sheria hizo tugwa. Na sheria hizo lazima ziwe na lengo la kuongeza au kutunza uhuru wa mwanadamu. Kwa sababu kazi kuu ya serikali ni kutunga sheria basi hamna mwenye mamlaka dhidi ya sheria hizo tungwa, endapo ikatokea mtendaji wa serikali ambaye anatenda bila kujali sheria zilizopo basi pole yake kwa kutokufahamu jinsi ujinga wake unavyobomoa Badala ya kujenga.

Sasa kutokana na binadamu kuwa na hulka tofauti, kuwa na katiba tofauti za akili zetu katika swala la siasa tumekuwa tukipishana namna ambavyo tungependa serikali tuliyomo iongozwe. Ili kuondoa confunsion kutokana na matwakwa yetu kuwa mengi kupita kiasi ni vyema vyama vyetu vya siasa kujifafanua vinapigania nini haswa katika siasa.

Hapa duniani watu waweza kugawanywa katika makundi mawili juu ya matwakwa yao kwa serikali. Kwa mtizamo wango hapa Tanzania nagawa kama ifuatavyo:

- Conservative. Hawa bila shaka ni CCM, ukiangalia misingi ya chama hiki ilikuwa ya kwamba serikali ndio kila kitu, serikali ilikuwa ipo juu ya mwananchi ambaye inamwongoza, sasa kutokana na pressure kutoka MABEBERU ya kwamba wanataka uhuru wa vyama vya siasa, hapa tanzania hamna jambo lililowatatiza wanasiasa kama kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa ilikuwa haingii akilini kuwepo kwa vyama vingi kutokana kwamba waliamini katika misingi ya umoja/ ujamaa tulionao sisi Watanzania hawakumini kwamba kutakuwa na watanzania wengine wenye msimamo tofauti na wao juu ya kufikia malengo ya maendeleo. Hii kasumba mpaka leo nadhani wazee wengi wa CCM wanayo ya kuchukulia vyama vingine tofauti na chao kama wasaliti/ wanatumwa na mabeberu wamekuwa na wasiwasi juu ya hivyi vyama tofauti navyo. Na CCM wengi wanapendelea serikali kuwa na nguvu kulika mwananchi.

- Liberal. Hapa ndo mahala kwa utitiri wa vyama vyote vilivyobakia tukianza na CHADEMA, CUF, ACT, TLP, NCCR nk. Hivyi vyama vyote vinataka Tanzania ikuwe kisiasa kuwe na serikali inayofuata mawimbi ya siasa kwa kuongeza uhuru kwa wananchi, hivi vyama ukivichunguza vinalenga mambo tofauti tofauti ambayo vinataka yaboreshwe kutoka kwenye mfumo mama tulioanza nao wa siasa za kijaamaa.

Kutokana na hivi vyama kukosa ungozi madhubuti, vinashindwa kuunganisha sera zao na kuwa chama kimoja ambacho kinaeleweka nini kinataka kufanya kwa wananchi. Hivyo kutokana na kuwepo kwa vyama vingi vyote vinaonekana vipo kwa ajili ya watu Fulani ambao wananufaika na vyama hivyo.

Siasa zetu zitakuwa TAMU sana endapo maoni yangu yatafanyiwa kazi na wahusika tajwa hapo juu. Kwani wananchi wataweza kujigawa vizuri kwa kujipima katika mzani wa siasa ni upande upi wanaegemea kama ni conservative au liberal. Hivyo suala hili litaongeza idadi ya wapiga kura na maoni mengi wananchi wataweza funguka juu wataka serikali yao iwe. Kwa sasa kilichopo ni confusion, anahitajika mmoja kusimamisha mara moja mvurugano huu.
 
Back
Top Bottom