Japhet M Kayungi is no more

mashikolomageni

JF-Expert Member
Jan 5, 2010
1,570
187
Aliyekuwa Mshauri wa Uvuvi Mkoa wa Kagera hadi 2007 Japhet M. Kayungi (1947-2011) amefariki leo katika hospitali ya Mugana Bukoba(V) alikokuwa anapatiwa matibabu. Kayungi atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa wa kulinda mazingira ya Ziwa Victoria kwa nguvu zake zote wakati akiwa mtumishi wa serikali. Alikuwa akiuchukia uvuvi haramu kwa dhati na hakuwa na mzaha dhidi ya wote waliokuwa wakijihusisha na uvuvi huo.
Ameacha watoto wanne.
Mungu ampumzishe kwa amani shujaa huyo wa mazingira
 
RIP KAYUNGI.lakini jamaa alikua mkorofi sijawi hona maishani,alidiliki ata kupiga watu risasi wale wavuvi haramu.da jamaa huyu hakika sitamsaau! Alitamani kulia hakiona visamaki vidogo vimevuliwa.
 
Rip kiongozi! Jamaa alikuwa hana kujuana katika kazi, tumepoteza boat yetu moja ya uvuvi pale, tulikamatwa na nyavu zenye matundu madogo, japokuwa jamaa tunamfahamu, alitupeleka mahakamani na mali zetu zote tukakosa
 
ifike hatua tusedisplay our true color, sio kafa basi wanamsifia, jamaa alikuwa anafanya kazi ka robbot, mkorofi, mnyanganyi na alikuwa na roho mbaya sana, ni vijana wengi mitaa ya kigarama, kashenye kabambiro huko kanyigo kawaachia umaskini kwa kuwanyanganya nyavu zao, samaki na kuzipeleka kusikojulikana, ni mengi amefanya akishirikiana na polisi kituo kidogo cha kishaka, HII NDO INATAKIWA ITUPE FUNDISHO KWAMBA HAKUNA MWANADAMU HATA KUFA PAMOJA NA MABAVU TUNAYOTUMIA KWA WANANCHI WETU! MUNGU AMREHEMU!ILA WATU WENYE KUFANYA KAZI KAMA HUYU JAMAA NAWAOMBA WAACHE MARA MOJA!
 
kwakweli uongo mbaya jamaa alikuwa na roho mbaya kama muuza sumu! Amewafilisi wengi,kapoteza uhai wa watu wengi sana. Kweli kila nafsi itaonja mauti,najua huko kwetu kuna watu hawaamimini kifo chake.R.i.p kayungi.
 
Back
Top Bottom