JAPAN: Bunge laidhinisha Mfalme kung'atuka

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
_96409691_0e53e48f-97bf-45f2-9f2c-61b60f3bf3a6.jpg

Bunge la Japan limeidhinisha sheria itakayomuwezesha Mfalme wa nchi hiyo Akihito kuondoka madarakani, jambo ambalo litakuwa la kwanza kwa mfalme kung'atuka nchini humo kwa zaidi ya miaka mia mbili.

Zoezi la upigaji kura katika bunge la juu, limeoneshwa moja kwa moja na Televisheni.

Sheria hiyo mpya ilianza kupitishwa na bunge la chini wiki iliyopita.

Mfalme Akihito mwenye umri wa miaka 83 aliishangaza nchi hiyo, mwaka uliopita kwa kuelezea nia yake ya kung'atuka, kutokana na afya yake na umri.

Mwana wa Mfalme Naruhito anatarajiwa kushika nafasi hiyo.

Chanzo: BBC
 
Ni kweli kuna watu hawajutii kuwa duniani, ila kwa tz nahisi robo3 ya watu hawatamani kabisa kuwa tanzagiza hii waliyopo, hata mm pia
 
Bongo limama linateuliwa kuwa RC na bado linang'ang'ania uenyekiti wa chama pinzani bila hata ya kuwa na aibu.!
 
Nang'atuka, afya imeshakuwa doro,
Nang'atuka, ofisini nimekuwa mtoro,
Nang'atuka, sitaki leta mgogoro,
Nang'atuka, nikajafungwa na nyororo.
Nang'atuka.
 
Bunge la Japan limeidhinisha sheria itakayomuwezesha Mfalme wa nchi hiyo Akihito kuondoka madarakani, jambo ambalo litakuwa la kwanza kwa mfalme kung'atuka nchini humo kwa zaidi ya miaka mia mbili.

Zoezi la upigaji kura katika bunge la juu, limeoneshwa moja kwa moja na Televisheni.

Sheria hiyo mpya ilianza kupitishwa na bunge la chini wiki iliyopita.

Mfalme Akihito mwenye umri wa miaka 83 aliishangaza nchi hiyo, mwaka uliopita kwa kuelezea nia yake ya kung'atuka, kutokana na afya yake na umri.

Mwana wa Mfalme Naruhito anatarajiwa kushika nafasi hiyo.

Chanzo: BBC
na aka kabibi ka uingereza kangatuke
 
Bongo limama linateuliwa kuwa RC na bado linang'ang'ania uenyekiti wa chama pinzani bila hata ya kuwa na aibu.!
Alipoteuliwa alifurahi sasa ile kuona salary slip akaguna...! Posho za uenyekiti wa chama ni kubwa zaidi na tamu na hauna presha... wacha tuone movie
 
Ivi hawa jamaa wana raisi au mfalme sijaelewa hapo maana japani ni nchi ambayo sijawahi sikia kwenye matukio tangu nipo mdogo
 
Back
Top Bottom