white hat
JF-Expert Member
- Dec 16, 2016
- 3,321
- 2,490
Nilimpigia simu mwanamke mmoja niliyekuwa
namdai fedha zangu, lakini hakupokea simu
yangu.
Nilipiga mara 10 zaidi, akagoma kupokea.
Nikitambua mumewe alikuwa safari, nikaamua
kumtumia meseji hii:
"Halo dada, ninakupigia siyo kukukumbusha deni
langu. Nilitaka tu kukwambia kwamba wasichana
wawili walikuwa wakipigana kumgombea mumeo
leo hapa mjini. Ulikuwa ugomvi mkubwa na yeye
alikuwa akitazama tu, mpaka mmojawao
alipofanikiwa kuchoropoka mumeo na msichana
mwingine yule aliyebaki wakaondoka."
Baada ya dakika chache akanipigia lakini
sikupokea. Aliendelea kupiga karibu mara 21
kisha akatuma meseji hii:
"Ugomvi umetokea wapi?
Wameelekea wapi?
Umewatambua hao wasichana? Tafadhali
niambie, nimechanganyikiwa."
Nilisoma ujumbe wake nikaupuuza. Akapiga tena,
karibu mara tano na sikupokea, kisha akatuma
meseji nyingine:
"Ninazo pesa zako, tafadhali tunaweza kukutana,
ili unieleze zaidi?"
Mimi nikamjibu, "Sawa, unaweza kunitumia pesa
kwa simu ili nipite kituo cha mafuta niongeze
wese, halafu nitakupitia na kukupeleka nyumbani
kwa msichana kwa sababu najua aliko."
Dakika mbili baada, nikapokea ujumbe wa salio
langu kwamba amenilipa pesa zangu zote.
Nimeizima simu na sasa nimejilaza kitandani
nipate usingizi... Sipendi ujinga. Januari ni mwezi
Dume lazima ujiongeze