January Makamba: TANZANIA hatujafikia kunufaika na Gas

Pascal Ndege

JF-Expert Member
Nov 24, 2012
2,977
1,897
Kwa wale waliyofuatilia siku January Makamba alipokuwa akitangaza nia alisema Tanzania hainufaiki na gas na haitanufaika na gas ndani ya miaka 20 ijayo! Katika hotuba yake aliianisha vyanzo vyote vya mapato isipokuwa gas na kusema kwa mikataba hii Tanzania haitanufaika na gas kwa miaka 10 atakayokuwa madarakani sasa ameona hana haja ya kuweka kama kipaumbele!

Huyu Makamba amewahi kuwa mwenyekiti wa nishati na madini sasa leo tunaanzisha mfuko wa gas wa nini? Kwa mapoto gani? Mbona haukushirikisha wananchi? Mbona wabunge wengi hawapo bungeni? Mimi naona kuna watu wanakimbia kufungwa sasa wanaleta hii sheria ili kupata mwavuli mpya na kuziba madhambi Yao.
 
Yaani bado unadanganywa kwa peremende kama mtoto!

Kama kweli January anaamini hicho anachokisema basi aende bungeni akayaseme hayo. Sio kuyasemea cho.oni kama anavyofanya sasa.
 
Tafadhali kuwa na staha kidogo...Makamba hakusemea chooni...alisema hilo akiwa live kwenye TVs wakati akitangaza nia kama alivosema mleta uzi....Kumbuka huyu ni waziri katika hii serikali....jiulize mara mbili what is going on?...well labda wanataka kuweka basis ya hayo mambo......swali jingine linakuja ....kwanini lazima katika bunge hili tena kwa hati ya dharura?!?
 
Natamani katika mdahalo wao leo kungekuwa na waandishi huru wa habari na wawaulize hawa wagombea wa urais kupitia CCM haya mambo!
 
Nazani January alikuwa sahihi tatizo la watu ni kutafuta namna ya kujiimalisha kisiasa
 
nazani january alikuwa sahihi tatizo la watu ni kutafuta namna ya kujiimalisha kisiasa,

Laana iliyowakumbwa Wanaigeria ilikuwa ya kutengeza mezani, na kama tutakubaliana na hoja ya Makamba kwa ujumla wake na sisi tutajikuta na laana kama hiyo ya Nigeria.

Kwa kifupi, shughuli nyingi kwenye sekta ya gesi ni wakati wa UTAFUTAJI na UENDELEZAJI. Hapa ndipo makampuni yanatumia fedha nyingi. Mfano kampuni inatumia takribani Dola million moja kwa kila meter moja. Sasa kwenye hayo matumizi ni kiasi gani kinabaki/kitabaki Tanzania, inategemea sana kama nchi tumejipangaje.

Lakini kubwa ni hili, wakati wa Utafutaji na Uendelezaji, Makampuni haya makubwa wana tabia ya kuzidisha gharama kwa makusudi na baadae wakati wa uzalishaji wanatachukuwa mapato kiasi kikubwa (kama sio yote kabisa) kwa kwa hoja kwamba wanarejesha gharama zao walizotumia wakati wa Utafutaji na Uendelezaji. Ni hii ndio LAANA iliyozikuta nchi nyingi za Afrika ikiwemo Nigeria kwamba wamejikuta hawana chao kwa sababu makampuni kama Shell walisema wanarudisha gharama zao.

Natambua Makamba amesomea mambo ya Usuluhishi wa Migogoro (conflict resolution) hivyo kuna fani nyingine bado ana kazi ya kujifunza. Tanzania Sekta ya gesi na mafuta inatakiwa iongelewe sasa sio baadae. Na tujue ni kiasi gani kinabakia Tanzania kipindi hiki cha Utafutaji na Uendelezaji?
 
Kwa wale waliyofuatilia siku January Makamba alipokuwa akitangaza nia alisema Tanzania hainufaiki na gas na haitanufaika na gas ndani ya miaka 20 ijayo! Katika hotuba yake aliianisha vyanzo vyote vya mapato isipokuwa gas na kusema kwa mikataba hii Tanzania haitanufaika na gas kwa miaka 10 atakayokuwa madarakani sasa ameona hana haja ya kuweka kama kipaumbele!

Huyu Makamba amewahi kuwa mwenyekiti wa nishati na madini sasa leo tunaanzisha mfuko wa gas wa nini? Kwa mapoto gani? Mbona haukushirikisha wananchi? Mbona wabunge wengi hawapo bungeni? Mimi naona kuna watu wanakimbia kufungwa sasa wanaleta hii sheria ili kupata mwavuli mpya na kuziba madhambi Yao.

Kazi ipo
 
Magufuli mwenyewe alisema gesi si yetu. Na hukuona akihangaika na gesi. Hili suala nafikiri bunge limatakiwa kutupa majibu. Mkataba gani uko kwenye gesi yetu.
 
Duh JF

Ni kwa sababu na yeye alishiriki kupitisha ile mikataba kwa hati ya dharura akiwa sehemu ya Wabunge wa ccm na Waziri! Tena ilikua ni usiku wa manane! Wapinzani walipiga kelele weeeh kuipinga ile mikataba!! Wakaonekana kama wana nongwa vile!

Miaka kadhaa baadae, ukweli umejulikana. Mabeberu ndiyo wamiliki wa gesi yetu.
 
Back
Top Bottom