January Makamba: Mzee anieleza siri juu ya mzee Nnauye, mzazi wa Nape

Mzee Nape senior alikuwa msema kweli angekuwa kama hawa wanasiasa wa kisasa angemtosa Mzee Makamba mtoni.
 
Ile hotuba kali ya Nape bungeni dhidi ya gesi huko kusini inawafanya kuweweseka,hapo anatafuta cheo kwa kuonyesha Nape ni mfitini kwa serikali na watu kama baba yake mzee Nnauye.
Sad!
Rudia kuisoma simulizi utamuelewa ndugu!
 
Jamani muwe mnasoma kwanza huku mmetulia hapo kamuabishaje Mzee Nnauye? soma taratibu anamaanisha ushahidi wa Mzee huyo marehemu ndio ulimfanya baba yake arudishwe kazini. Maana nyingine ni kuwa mzee huyo hakuogopa lile genge lilitaka kumfutilia mbali Mzee Makamba anachojaribu kutuambia January ni kuwa Nape ni jasiri, msema kweli na haogopi kuudhi makundi mengine ya kinafiki na hii tabia karithi kwa baba yake.Sina ushabiki na mwanakijani yyt.
Huyu mzee mwenye nundu usoni ni mchawi na mnafiki,huyo ndio alimfukuza nape ccm akadai amemfungia ahera na mbinguni,kma angekua anakumbuka msaada wa mzee nnauye asingefanya jambo hilo kwa mwanae..hicho kizee kichawi tu kinaroho mbaya kma ccm wenzake.alihusika kumfukuza mzungu wa binti yke ili wabaki na mali zke
 
Huyu mzee mwenye nundu usoni ni mchawi na mnafiki,huyo ndio alimfukuza nape ccm akadai amemfungia ahera na mbinguni,kma angekua anakumbuka msaada wa mzee nnauye asingefanya jambo hilo kwa mwanae..hicho kizee kichawi tu kinaroho mbaya kma ccm wenzake.alihusika kumfukuza mzungu wa binti yke ili wabaki na mali zke
Inawezekana sikatai CCM kama ilivyo vyama na taasisi nyingine fitina haikosekani na wakati mwingine maamuzi ya kumkata mtu hayafanywi na mtu mmoja Mzee inawezekana hakuwa mzuri lakini hapa tunajadili yaliyomo kwenye ujumbe wa Jan. yawe ya ukweli au uongo.
 
Who fights for food?
Makamba already has some food
Having food is not a reason to not fight for food.

Just as having money is not a reason to not fight for money.

Your suggesting otherwise is logically flawed.

It is a logical non sequitur.
 
baba yake alifukuzwa kwa tuhuma mbili kula ng'ombe wa wizi na kudaiwa masurufu lakini aliandika barua kwa kamati kuu kuwa hakupewa nafasi ya kujitetea baada ya Mwenyekiti wa wakati huo kupata barua yake alimwita ili ajitete kwenye kamati kuu.
Alipofika alimwuliza Moses Nauye yule ng'ombe tuliyekula alikuwa mtamu, Moses Nauye hakujibu kitu akawa amemaliza.
Kuhusu masurufu aliuliza naomba humu ndani mnieleze nani hadaiwi masurufu hakuna aliyenyoosha mkono kueleza kuwa hadaiwi masurufu akamaliza.
Hoja yake ya kwanza kama kweli alikuwa amekula ng'ombe wa wizi mbona aliokula nao hawajachukuliwa hatua badala yake yeye pekee ndiye aadhibiwe.
Hoja yake ya pili kama kudaiwa masurufu ni kosa mbona wote wanaodaiwa masurufu wako kazini ila yeye ndio anafukuzwa
Baada hizo hoja alirudishwa kazini hivi ndivyo ilivyokuwa
 
mzee-makamba-620x308.jpg


JANUARY Makamba, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira ametoa madai mazito kwa chama chake, kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemtelekeza baba yake Mzee Yusuph Makamba akiwa mgonjwa.

Makamba ameandika ujumbe huyo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook, akielezea hali ya baba yake kiafya na kusema pamoja na kupitia hali hiyo lakini CCM hakimpi stahiki zake kama mstaafu wa chama hicho.

Mzee Makamba ameshika nafasi mbalimbali katika chama lakini kikubwa zaidi ni kuwa Katibu Mkuu cha chama hicho, pamoja na nafasi mbalimbali serikalini ikiwemo Mkuu wa mikoa mbalimbali ukiwemo Dar es Salaam.

Katika taarifa hiyo ya January pia imeeleza tuhuma za wanasiasa aliowalea Mzee Makamba ambao mmoja wao kwa sasa anasema maneno mabaya dhidi ya mzee huyo.

Soma andiko la January hapa chini:

Majuzi nilienda kumjulia hali Mzee Makamba ambaye anaumwa. Mazungumzo yake yalihusu watoto wake aliowalea kisiasa, ambapo mmoja wapo, pamoja na kumhifadhi na kumfariji wakati kasahaulika, sasa anasema maneno mabaya dhidi yake.

Tukazungumzia subira na uvumilivu kwenye siasa. Akaamua kunipa kisa kifuatacho:

Mwaka 1980, baada ya kutoka vitani, alipangwa kuwa Katibu Msaidizi wa CCM Dodoma. Mwaka 1982, wakati wa kuadhimisha miaka 5 ya kuzaliwa kwa CCM kimkoa kule Mvumi, alitumwa mnadani Mwitikira kununua kitoweo (ng’ombe na mbuzi) kwa ajili ya sherehe.

Baada ya muda, akiwa kahamishiwa Monduli, akapewa barua ya kusimamishwa utumishi na uongozi (u-NEC) wa CCM kwa tuhuma kwamba wale ng’ombe na mbuzi wa sherehe aliwaswaga kwetu Bumbuli badala ya kuwapeleka Mvumi.

Tukafungasha mizigo na kurudi kijijini. Wakati Mzee anaendelea kutafuta maisha kijijini alikuwa anaandika barua kila siku Ikulu kwa Mwalimu Nyerere kueleza kwamba ameonewa. Baada ya barua kadhaa, Mwalimu akaagiza aitwe kwenye kikao cha Kamati Kuu Chamwino Dodoma. Mzee aliwasili Dodoma akiwa kachoka sana, amebeba makabrasha yake kwenye mfuko wa rambo.

Kikao kilipoanza, Mwalimu akampa nafasi Mzee Makamba ya kujieleza. Mzee akaanza kwa kusema ana hoja nyingi kuonyesha kaonewa lakini angependa kuanza na swali dogo: “Kwenye ile sherehe, Ndugu Moses Nnauye alikuwa mgeni rasmi na alikula ubwabwa. Ndugu Mwenyekiti, naomba aulizwe iwapo ubwabwa ule aliokula ulikuwa na nyama au la.” Mwalimu akamgeukia Nnauye na kumuuliza “Moses, Yusuf anauliza iwapo ubwabwa uliokula ulikuwa na nyama.” Nnauye akasimama na kujibu “Mwenyekiti, ubwabwa ulikuwa na nyama.” Mzee akaendelea “iwapo niliswaga ng’ombe kijijini kwetu, hiyo nyama kwenye ubwabwa ilitoka wapi?” Mwalimu akawageukia watendaji waliotengeneza mashtaka ili watoe majibu. Kukawa hakuna jibu. Baada ya Mzee kujieleza tena kwa kifupi ikadhihirika wazi kabisa kwamba kulikuwa na uonevu mkubwa. Akarudishwa kazini.

Wakati Mzee ananipa kisa hiki, alikuwa anajichoma sindano ya “insulin” kudhibiti kisukari, huku akigusa jicho lake moja ambalo linakaribia kuwa pofu. Amegoma kabisa kutibu jicho akisema “hata likiacha kuona, sio tatizo kabisa; limeshaona mengi humu duniani”

Kwa sasa Mzee hali yake kiafya sio nzuri chama cha mapinduzi hakimpi stahiki zake kama mstaafu.
January Makamba
 
Huyu si ndo alitetea ccm iliyoko madarakani??wakt rasimali zinatumika vibaya si alikuwa anapiga vigelegele?muda wote huo hajajiwekeza vizuri?au uroho tyu alipwe mpaka uzeeni ??je sisi nan anatulipa ??mbn mnajiona ninyi ndo watu pambana na hali yako sinaga huruma na ma ccm
 
Huyu si ndo alitetea ccm iliyoko madarakani??wakt rasimali zinatumika vibaya si alikuwa anapiga vigelegele?muda wote huo hajajiwekeza vizuri?au uroho tyu alipwe mpaka uzeeni ??je sisi nan anatulipa ??mbn mnajiona ninyi ndo watu pambana na hali yako sinaga huruma na ma ccm
anavuna alichopanda
 
Back
Top Bottom